ATM za kutolea mipira ya kiume 'Kondomu' zaja Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ATM za kutolea mipira ya kiume 'Kondomu' zaja Bongo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,171
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  ATM za kutolea mipira ya kiume 'Kondomu' zaja Bongo


  Wednesday, April 22, 2009 3:29 PM
  KUTOKANA na kampeni za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa la ukimwi, Watanzania wanatarajia kufungiwa mashine za kutolea mipira ya kiume 'Kondomu' nchini kote
  Mashine hizo zinatarajiwa kufungwa na Shirika la PSI- Tanzania ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa mipira hiyo kiurahisi.

  Taarifa zilizotoka Makao ya Makuu ya Shirika la PSI nchini zimesema kuwa mashine hizo zenye mfano kama wa kutolea fedha wanatarajia kufunga mapema mwezi ujao.

  Taarifa hizo zilisema kuwa mashine hizo zitaanza kufungwa Mkoani Morogoro katika baa mbalimbali zilizoko Mkoani humo.

  Meneja wa PSI Mkoani Morogoro, Godwin Msafiri alithibitisha na kusema mashine hizo zitaanza kufungwa mkoani humo.

  Alisema kuwa shirika hilo litaanza kufunga mashine hizo zipatazo 15 katika baa mbalimbali za mkoani humo na zingine kufungwa katika mji wa kitalii Mikumi mapema mwezi ujao.

  Alisema lengo la kuanzisha kufunga mashine hizo ni kuinua Waatanzania walio wengi ambao wanadharau matumizi ya mipira hiyo kwa kuwa janga la ugonjwa wa ukimwi umekuwa ni tishio nchini.

  Alisema kwa kuwa watu wengi huwa wanaona kazi kufika dukani na kununua zana hiyo ambayo ni muhimu kwa wale ambao wanafanya ngono zembe hivyo mashine hizo zitawarahisishia.

  Alisema Shirika hilo litasambaza mashine hizo nchini kote nzima ila wameanza Morogoro.
   
 2. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
Loading...