zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,031
- 28,667
Mwanadamu kwa haiba yake akiwa kwenye changamoto ndio anapata wasaa mzuri wa kuchakata akili yake ili kupata suluhisho la matatizo yanayomzunguka. Na hili ndio lilimkuta Msanifu majengo na mhandisi wa kijerumani Herman Sorgel kuja kubuni mradi wenye maono makubwa uliohitaji wafanyakazi zaidi ya million moja na kukamilika baada ya miaka 150!!
Prologue
Herman Sorgel alikua msanifu majengo (Architect) aliyezaliwa mji wa Bavaria,ujerumani mnamo 1885 na kufariki mwaka 1952. Baada ya kushuhudia vita kuu mbili za dunia zikileta madhara makubwa na migogoro isiyoisha, mhandisi huyu ikabidi abuni mradi ambao ungeiunganisha ulaya kuwa kitu kimoja na kuepusha vita ya tatu ya dunia huku dunia nzima ikihakikishiwa amani milele sio kwa kutumia bunduki au siasa za majukwaani bali teknolojia.
Mpango wa Mradi:
Strait of Gilbraltar
Ningependa wasomaji mfahamu kuwa umbali kati ya ulaya na Afrika ni km 14 pekee kiufupi ukiwa morocco unaiona Hispania kabisa na katika historia kuna tukio linaitwa Messinian Salinic Crisis ambapo eneo hilo la ulaya lilishikamana na eneo la Afrika hivyo bahari ya Mediterranean ikazibwa jambo lililofanya maji yasiingie kutoka Bahari ya Atlantic. Ilichukua takribani miaka kadhaa kina cha maji kilipungua sana na bara la Afrika na ulaya yaligusana kabisa kwa nchi kavu. However mafuriko makubwa yalitokea huko mbeleni na kurudisha bahari hiyo mahala pake mpaka leo hii.
Dhana hii ilimfikirisha sana Mhandisi Sorgel kwamba kma ataweza kurudia tukio hilo la kijiografia kwa kutumia mbinu za kiuhandisi basi anaweza unganisha Ulaya na Afrika kuwa bara moja lenye nguvu na tishio kuliko yote.
Kiini cha mradi ingekua pale Gilbraltar ambapo ungejengwa bwawa la kufua umeme kubwa katika historia ya dunia ambalo lingefua megawatt elfu 50. Lingekua na urefu wa mzunguko km 34 na msingi wenye urefu wa km 2.5 kwenda chini ndani ya maji na 300 m juu ya maji.
Mpango ulikuwa, angeziba bahari ya Atlantic na mito inayozunguka kma Dardenelles kuleta maji kwenye bahari ya Mediterranean ili kupunguza kina cha maji hadi kufika Mt 200 magharibi na Mt 100 mashariki.
Bwawa hili lingezuia (Divert) maji kuingia bahari ya Mediterranean hivyo kina cha maji kingepungua kwa zaidi ya mita 200. Na maji mengine yangetumika kwenye kuzalisha umeme, mradi mkubwa wa kurutubisha jangwa la sahara kwa ajili ya kilimo cha kisasa pamoja na kutenga ardhi mpya ambayo ingeunganisha mabara ya Afrika na Ulaya ili kumaliza changamoto ya udogo wa ardhi.
Atlantropa ikikamilika mabara yangeungana hivi kwa nchi kavu
Mafanikio aliyotarajia
1.Kuwepo bara lenye nguvu kuweza kuchallenge nguvu ya America na Asia kama zingekuja kuwa tishio kiuchumi/Kisiasa.
2.Kumaliza tatizo la ajira ulaya maana wangetapakaa Huku Afrika kutafuta fursa mpya kma kilimo,madini n.k
3.Kungemaliza tatizo la ardhi ulaya maana aliona vita nyingi zilikua kugombania ardhi. Ulaya ingekua extended mpaka kusini mwa Afrika hivyo ardhi ingekua zaidi ya mahitaji.
4.Chakula kisingepungua maana ardhi mpya ingetumika kwa ajili ya kilimo na jangwa la sahara lingerutubishwa kwa mradi mkubwa wa umwagiliaji hivyo ardhi yake ingeanza kuwa na rutuba ya kukuza mimea. Yangejengwa mashamba makubwa kabisa ya kilimo cha kisasa hivyo chakula kisingewahi isha ulaya.
5.Nishati ingekuwa ya kutosha mfano huo mradi wote wa mabwawa ya umeme takribani 8 ungezalisha megawatts zaidi ya Laki moja hivyo umeme ungekuwa wa uhakika Atlantropa nzima hivyo kupunguza vita za kugombea nishati ndogo iliyobaki mfano mafuta na makaa ya mawe n.k
6.Mradi huu ungeunganisha mataifa yote ya Ulaya yaliyokua kwenye vuguvugu la vita kuu za dunia maana mradi ungehitaji ushirikiano wa mataifa yote kwenye utekelezaji na ukikamilika wangeishi kama familia moja na hivyo kusahau tofauti zao maana nishati ipo,chakula kipo,ardhi ya kumwaga!! Mpigane kwa lipi tena??!!
Utekelezaji Afrika
Afrika ingejengwa maziwa makuu mapya mawili pale DRC kwenye mto congo na ziwa Chad lingetanuliwa kina. Hapa pia yangejengwa mabwawa makubwa ya kufua umeme kulisha Afrika nzima. Maziwa haya yangefanya eneo lote la sahara ambalo ni jangwa kuwa sehemu ya kilimo maana yangeathiri uoto kutokana na unyevu unaoletwa. Pia hali ya hewa ingebadilika ambapo joto lingepungua na kufanya eneo kuwa zuri kwa makazi ya wazungu pia.
Gilbraltar na sicily pia kungewekwa daraja la magari na treni kuunganisha mabara haya mawili na watu wangevuka kwa urahisi tu kupitia Tunisia na Morocco. Kiufupi mabara yangeunganishwa na kuifanya ulaya nzima kuhamia Afrika na viceversa ili kupata bara moja lenye nguvu na maisha mazuri.
Aliamini kuwa amani ingeletwa sio kwa mitutu na kelele za wanasiasa majukwaani ila kwa teknolojia ambayo ingeleta maisha bora kwa watu wote hivyo amani ingepatikana. Alipanga mataifa yote Atlantropa yaunganishwe na hiyo "gridi ya taifa" ili akitokea mkorofi mmoja kutaka kuleta vita basi anazimiwa umeme ili kumdhoofisha so ingeleta discipline kwa mataifa yote ya ulaya na Afrika.
Matokeo
Mradi huu licha ya kupata support ya baadhi ya wahandisi na viongozi wa kisiasa ila mataifa ya ulaya hayakuutilia maanani. Alitumia nguvu kubwa hata ya kumshawishi Hitler kuutimiza ili agenda yake ya kutawala dunia itimie ila pamoja na udikteta wake bado aliikataa sababu mradi unawaza kuleta amani wakati ambao ujerumani ulihubiri vita ndio suluhu ya kuwakomboa watu wake kutoka mikono ya ''wazungu''. Mpaka anafariki mwaka 1952 mradi wake haukuwahi anza utekelezaji wake na toka azikwe hajapatikana bado mtu wa kuendeleza ndoto yake hiyo ya bara kuu.
Swali langu kwa Great thinkers humu
1. Je kwanini wazungu hawakusupport mradi huu??
2. Je nini hatma ya Afrika kujikomboa kwenye ukoloni huu??
3. Je mradi huu ungefanikiwa?
4. Nini madhara ya kimazingira?
5. Na je malengo kamili ya mradi huu kuleta amani ya milele ingetimia??
Naomba kuwasilisha