Ati! Q-Chilla kuimba Taarab! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ati! Q-Chilla kuimba Taarab!

Discussion in 'Entertainment' started by Ochu, Sep 8, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Baada ya kuanzisha bendi yake na hivyo kuwapa mashabiki moyo kuwa sasa msanii Q-Chillah ameamua kuupeleka muziki wa kizazi kipya katika level nyingine yaani(next level),msanii huyo amegeuka tena na kudai kuwa sasa anageukia muziki wa Taarab.
  Jambo hilo ambalo limeonekana kuwashangaza wengi kama sio wote,kwa msanii huyo ni kama sinema ya kuigiza kutokana na kauli yake kuwa....amefikia uamuzi huo baada ya kuona muziki wa kizazi kipya unafunikwa na ule wa Taarab kutokana na kuwa na mashabiki wengi zaidi.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya..Aboubakar Katwila maarufu kama Q-Chilla amesema sasa ameamua kufanya muziki wa Taarab kwa kuwa unalipa zaidi ukilinganisha na wa Bongo Flava.

  Akijitetea kuhusu hilo...Chillah alisema...unapokuwa kwenye fani ya muziki ni lazima uwe mjanja na kusoma vyema alama za nyakati na ndio maana akaamua kutoka kivingine..na kudai kuwa anaamini kutoka kwake kimwambao kutamtoa kiuhakika.

  Katika kudhihirisha nia yake hiyo,hivi karibuni alihudhuria tamasha moja la taarab hapa jijini na kukamua sambamba na wanamuziki wa kundi hlo stejini.
   
 2. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika maisha ni lazima kuwe na mambo ambayo kwayo unaamini,hii itakufanya kuwa na msimamo na kuwa na uwezo wa kukitetea kile unachaamini.Vinginevyo utajikuta unaangaika kila wakati,kila mahali kwani hujui unataka nini.Tunamtakia kila la kheri.
   
 3. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #3
  Sep 8, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Avator yako tu me hoi kwa kucheka. kwi kwi kwi kwi.
   
 4. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Usicheze na njaa.
   
Loading...