Ati mimi tu ndiye mwenye nywila za maendeleo!!!

soine

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,113
2,329
Habarini wanazuoni,

Hongereni kwa weekend murua kabisa, na karibuni kuwajibika ktk juma hili kama ilivyo ada yenu.

Nirukie hoja yangu ingawa mimi sio mwandishi mzuri.

Maneno au kauli za viongozi wetu wanapokuwa wanatoa hotuba majukwaani mara nyingi zinaacha maulizo mengi vichwani mwa wengi. Inafika mahali wanajivika mamlaka ya "umilele" na nguvu za "uungu" ambazo ni nadra kama sio haiwezekani mwanadamu kuwa nazo. Kiongozi anafika mahali na kuona pasipo yeye kamwe ng'ambo ya mto hatutavuka, kesho hatutakula chakula wala kuwa na mavazi. Kwa mantiki hii, hawa viongozi wamekuwa ndio "nywila" (password za maendeleo...bila uwepo wao hakuna mwingine wa kufungua (unlock codes) hizi codes za maendeleo...hivyo inabidi wawepo na waendelee kuwepo ila tuvuke ng'ambo.

Majigambo haya yamenipa maswali mengi. Kumbe wengi wetu tunapopewa nafasi iwe makazini au popote huwa tunajisahau na kuona hakuna mwingine wa kuifanya vema kazi au kufit kwenye nafasi husika....kumbe ukiondoka tu aweza kuja mtu akafanya maajabu hadi ukashangaa!!!

Niliwahi kuwa mwanafunzi wa mwalimu mmoja ambaye alikuwa mwaminifu sana pale alipoona na kutambua vipaji vya wanafunzi wake. Mwalimu wangu aliniambia kuna nyakati huwa anatumia wanafunzi wake kujifunza, na baadhi ya wanafunzi wake wamekuwa msaada kufanya kazi yake vizuri sana. Kumbuka huyu ni mwalimu ambaye wengi wetu tulimuona ndiye anayejua kila kitu anachofundisha kwa undani zaidi, kumbe naye anaona faida na mchango wa wanafunzi wake!!

Tusijibeze kuwa sisi ndio sisi, bila ya sisi hakuna mwingine awaye yeyote. Tukiwa na mawazo mgando ya namna hii twajidanganya bure. I tell you, ndani ya nchii hii, ndani ya CCM/CHADEMA/CUF/ACT wako watu wanaweza mambo ambayo yazidi haya yatupayo kiburi.

Hongera viongozi wangu kwa SGR, Stieglers Gorge, Midege na viwanda kibao! But ukweli ni kwamba bado hatujawa na viwanda vyenye tija kama alivyoanzisha Baba wa Taifa
 
Back
Top Bottom