Wakuu nimeukuta huu mjadala kwenye blog ya Mjengwa nikaupenda, nimeona niulete hapa tuutajirishe zaidi. Wapo wanaodai kuwa baada ya kuyaona ya Lowassa sasa wanahisi kumbe Sumaye hakuwa fisadi, vinginevyo angeshaanikwa kama sasa wanavyoanikwa kina Balali, Lowassa na hata Mkapa. Pia wanadai mambo aliyotuhumiwa Sumaye kama kukopa sh mil 50 NSSF (ambazo atalipa) na kuwa na mashamba (ambako watu wanafanya kazi halali ya kulima kwa nguvu zao) ni tuhuma ndogo kulinganisha na hela zilizochotwa BoT ambazo zimepotea na makampuni ya Richmond, IPTL nk ambayo yanakula bila jasho! Yuko aliyedai kuwa Sumaye kumbe alikuwa Premier mzuri sana! Details za mjadala wenyewe hizi hapa: http://mjengwa.blogspot.com/2008/02/fikiri-wangepewa-mtihani-huu-fred-na.html#comments
Wakuu mnasemaje?
Wakuu mnasemaje?