Elections 2010 Ati hii (Picha) imekaaje?

katika pita pita zangu nimeaona niiposti hii:

38967_411141341155_687191155_5323021_3318516_n.jpg

Ujumbe haujatulia, unaonyesha as if Dr Slaa anapaswa kuwa Rais 2010 kwa minajiri tu ya kupokezana kijiti.
 
katika pita pita zangu nimeaona niiposti hii:

38967_411141341155_687191155_5323021_3318516_n.jpg

kasoro hakuna neno chadema, LAZIMA KUWE NA NENO CHADEMA KWENYE HIYO PICHA AU HATA ALAMA YA VIDOLE VIWILI

NA PIA NENO SURA SIYO NENO ZURI KUTUMIKA KWA AJILI LINAWEZA LIKAGEUZWA NA KUTUMIKA AGAIST YEYE IN SO MANY WAYS ie "MUUZA SURA"
 
Kukipiku Chama Cha CCM inataka kazi tena kazi yenyewe iwe nzito sana, sio mchezo jamani kusema ukweli CCM imeota mizizi ndani ya Serikali. Kuking'owa CCM itachukuwa muda mrefu sana itabidi vyama vya upinzani viwe kitu kimoja Viungane pasipo na kuungana hakuna chama chochote cha Upinzani kinachoweza kukishinda CCM. mimi naombea Dr Slaa awe Rais wetu wa Mwaka 2010 Mungu amsaidie Ameen.

Ninaamimi CCM haimpikii chai MUNGU.....si lazima ichukue muda kuing'oa madarakani kwa sababu huenda mashabiki wengi wapo ccm kwa sababu ni chama tawala hao hao wakiona upepo umebadilika wanahamia upinzani ......uchaguzi wa ghana uliopita rais aliyekuwepo madarakani kufour alimshabikia profesa john alta mills wa upinzani....hakumshabikia mgombea wa chama chake mwenyewe.....
Mix with yours
 
Tunaruhusiwa ... Kuna kikundi kimeanzishwa cha Friends of Slaa (FOS) nikipata taarifa zaidi nitakuPM
Tandao jipya.

Kikwete amejuta na mitandao mpaka sasa amempa mwanae asimamie uchaguzi wake.

Nyinyi mnachukua ukurasa kutoka kwenye tabu la siri za Kikwete ambalo mwenzenu keshalitupa.
 
CHADEMA inayo kazi kubwa tena nzito sana mbele yake, hii ni dhahili wala haifichiki. At the end, itafanikiwa kukiimarisha chama and "maybe" kuongeza idadi ya wabunge japo wawili, kama watakuwa wamejipanga vema. All in all,CCM bado inanguvu sana hasa kwa wananchi wa kawaida na Vijijini ambako ndio kunawapigakura wengi. Kuwageuza fikra, hiyo ndiyo kazi inhitaji nguvu za ziada.
But tumempoteza mpigaji mzuri sana Bungeni.
All the Best Hon. Dr. Slaa !!!!!! :doh:
 
hiyo picha hapana ..............haiuziki kwa wapiga kura. Charm and Charisma sells...............hiyo picha kwa undecided voters watapiga kwa kikwete tu.

(wapiga kura hasa wa kike wanakuwa influenced na sura ...........just sayin')
 
Kwa nini watanzania tunakuwa waoga eti ni vigumu sana kuing'oa CCM madarakani... why not kwani walizaliwa na hii nchi.. Watatolewa tu.. Marekani na Ulimwengu mzima ulifikiri Obama anapoteza muda wake lakini Historia ilikamilika iwe Tanzania nani kasema haiwezekani inawezekana tena kwa urahisi tu.. CCM CCM mpaka lini. Muda wao umekwisha..
Nashangaa watu wenye fikra potofu eti kwa vile alikuwa padri basi ataigeuza Tz. iwe ni chi ya kikristu huku ni kutaka kuleta vurugu za kidini. Mbona juzi mgombea mwenza wa CCM alipoteuliwa wakristu hawakubeba bango. Nyerere alikuwa mcha mungu sana mbona hakuigeza Tz ikawa ya wakristu tu. Acheni kuongea kama msiofahamu ukweli wa watanzania. Tz. imeongozwa na Kikwete, Mwinyi kwani waliigeuza nchi ikawa ya kiislamu? Wewe mwenye chuki na imani ya kikristu nadhani hapa si mahali pake siasa ni siasa na dini ni dini period usituletee kwikwi isiyo na mpango
 
Ahsante sana Pakawa. Udini na ukabila vitatumika sana na CCM katika kampeni hii ambavyo havina ukweli wowote ili kumzuia Dr Slaa asishinde, lakini tumuombee Mungu amsaidie katika kazi iliyoko mbele yake, kama chama chake kitampitisha rasmi kama mgombea wa Urais ni kubwa mno, lakini hakuna lolote la heri ambalo linashindikana hapa duniani.
 
Kwa nini watanzania tunakuwa waoga eti ni vigumu sana kuing'oa CCM madarakani... why not kwani walizaliwa na hii nchi.. Watatolewa tu..

CCM inang'oleka. Hakuna cha ajabu. Ni situation is permanent!!!!!!!!!!
 
katika pita pita zangu nimeaona niiposti hii:

38967_411141341155_687191155_5323021_3318516_n.jpg

Picha halisi ni hii hapa! Hii sijui MMJJ ametoa wapi! Inaweza kuwa hata yeye mwenyewe katengeneza kuwaponda Chadema tu! Haina nembo ya Chama wala nini! It's definitely not the official campaign poster!Kwa hiyo achane papara...
here is the original:
untitled63.jpg
 
Mh mbona naona km kuna mkono wa Chama Cha Mafisadi... Ingawa ni nzuri kwa Dr Slaa kugombea but nadhani kazi aliyonayo ni ngumu mno!!!!! Isije ikawa ni mapandikizi ya CCM yenye mpango wa kuzorotesha bunge lijalo coz km Dr SLaa atakosa urais, na ubunge ndiyo hivyo tena... Asubiri 2015 kuingia tena mjengoni..Ohoooo... mapambano yatakuwa yamezoroteshwa kwa kiasi kikubwa!!!!

Watanzania tubadilike, tubadilishe kufikiri kwetu, tubadilishe imani zetu, Mabadiliko ya kweli yako ndani ya mtu mmoja mmoja, tukiamini pamoja kwamba tunaweza, tutaweza, Tukishirikiana wote pamoja tutaweza, Tukiungana wote pamoja tunaweza, Tukiamua Pamoja tunaweza. Tusikate tamaa, Sote PAMOJA tunaweza.
 
MKJJ;

Kwa maoni yangu, bango au posta hili linatakiwa libebe ujumbe mfupi wa matumaini au mageuzi other than "Rais Mpya" and "Sura Mpya". something relating to Matumaini Mpya or Maisha Mapya . . . .

Also the use of Mpya . . Mpya looks like copying from Kasi Mpya, Nguvu Mpya and Ari Mpya slogan.

More creativity is required.

Super.
 
.Ukiangalia kwa makini wanachi bado wapo usingizini tena huo usingizi ni mzito sana itabidi waamke wananchi wenyewe waone ukweli wa mambo kuwa Chama cha CCM hakina mpango wowote..

Lakini ukiangalia kwa makini zaidi wengi wao wamefungua macho sema hawajaanza kunyanyuka toka kwenye matandiko yao...
 
Kukipiku Chama Cha CCM inataka kazi tena kazi yenyewe iwe nzito sana, sio mchezo jamani kusema ukweli CCM imeota mizizi ndani ya Serikali. Kuking'owa CCM itachukuwa muda mrefu sana itabidi vyama vya upinzani viwe kitu kimoja Viungane pasipo na kuungana hakuna chama chochote cha Upinzani kinachoweza kukishinda CCM. mimi naombea Dr Slaa awe Rais wetu wa Mwaka 2010 Mungu amsaidie Ameen.

remember what happened to KANU hapa jirani tu Kenya? Jamani CCM inaondoka mwaka huu tukizingatia tu kuwa kila kura itakayopigwa ni muhimu. tusiishie kwenye jamvi hapa, hata mliopo majuu octoba 31 mrudi kupiga kura kwa maslahi yenu.
 
Back
Top Bottom