Athumani Nyamlani ateuliwa kukaimu nafasi ya Wambura TFF

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
1,595
Points
2,000

beth

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
1,595 2,000
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumapili imemteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi makamu wa rais wa shirikisho hilo.

Nyamlani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Wambura kufungiwa maisha kujihusisha na soka.

Wambura amefungiwa na kamati ya maadili ambayo imeeleza kumtia hatiani na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi.

Hata hivyo, tayari Wambura amekata rufaa kupinga hukumu hiyo akisisitiza hakubaliani nayo.

pic+nyamlani.gif
 

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Messages
15,611
Points
2,000

Sibonike

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2010
15,611 2,000
Kwenye post moja niliwahi kuhoji kama Wambura atamaliza mwaka akiwa chini ya mtu.

Huenda Karia kabaini uchaguzi ujao Wambura angemugeuka kuutaka urais wenyewe. Si zambi, lakini atakubali upuuzi huo?

Nafasi ya Makamu Rais TFF haina tija, ifutwe mara moja. Awepo jogoo mmoja tu TFF awajibike yeye tu.

Nyamlani ana historia ya kumnyenyekea boss wake. Wambura hawezi. Atajiona boss ni yeye.
 

Mr.Junior

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Messages
10,052
Points
2,000

Mr.Junior

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2013
10,052 2,000
Kwa huu upuuzi unaoendelea tusahau soka letu kukua.

Karia hana tofauti na Malinzi.

Wanapambana kuwekana ili wajihakikishie upigaji hapo TFF.

Matokeo yake vilabu na timu ya taifa ni mwendo wa vipigo tu halafu tunaanza kutafuta mchawi wakati mchawi ni viongozi wa soka waliokuwa bize kupambana kupiga pesa, kupeana madaraka kinyume na taratibu, kufungia wengine wasijihusishe na soka.

Tanzania tuna bahati mbaya kila sehemu.
 

kidudukuntu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2017
Messages
289
Points
250

kidudukuntu

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2017
289 250
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumapili imemteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi makamu wa rais wa shirikisho hilo.

Nyamlani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Wambura kufungiwa maisha kujihusisha na soka.

Wambura amefungiwa na kamati ya maadili ambayo imeeleza kumtia hatiani na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi.

Hata hivyo, tayari Wambura amekata rufaa kupinga hukumu hiyo akisisitiza hakubaliani nayo.

View attachment 724736
Shida ni kuwa wambura alikuwa timu malinzi hayo mengine mtajazia wenyewe
 

korojani

Senior Member
Joined
Dec 17, 2016
Messages
194
Points
250

korojani

Senior Member
Joined Dec 17, 2016
194 250
Hivi pale TFF hakunaga watu wengine wenye uwezo wa kuongoza soka? Hivi sisi Watz wengine hatuwezi kuongoza soka letu zaidi ya wale waliopo pale TFF miaka yote. Maana miaka yote majina ya viongozi ni yaleyale ila inayobadilika ni nafasi wanazoziongoza tu.
Mimi nimeanza kumsikia Karia, Nyamlani tangu enzi hizo Tff ikiwa FAT enzi za uongozi wa Muhidin Ndolaga na katibu wake Ismail Rage.
Ama kwa hakika TFF na soka letu kwa Ujumla linanuka rushwa tupu.
 

kamba0719

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2018
Messages
289
Points
500

kamba0719

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2018
289 500
"Nyamlani sikiliza sauti za wapenda soka na urudi ukasome article 50-1 katika msahafu wa maadili ya TFF.

TFF ni taasisi ya umma yenye misingi ya maadili na utawala bora (good governance) haiwezi kutumika kama kichaka chako cha kujifichia.

Tanzania inajuwa ulipotoka umeondolewa kwa ukosefu wa maadili (integrity) katika chombo cha umma chenye hadhi ya juu sana nchini mahakama.

Mwerevu asingekubali hata uteuzi wa kuwa mjumbe wa kuteuliwa wa kamati ya utendaji TFF, ukiachilia mbali hiyo ya kuwa makamu wa rais cheo cha pili kwa ukubwa.

Katika kanuni za maadili, uadilifu ni dhima ya juu kabisa katika kada yoyote ile duniani. Leo hii kuna watu hatunao tena katika medani ya soka kwa kukosa uadilifu (Integrity), iweje wewe unarudi huku??.. Tunaomba ukae pembeni usituchafulie taasisi na watu tuliowachagua kwa umakini mkubwa. "A questionable integrity is a serious problem"
"
Maneno ya Shaffih sasa huyu mpaka mahakama ishamuhukumu,kwa ukosefu wa maadili leo unampa umakamu wa rais.
Pole wambura tatizo haupo ktk system,ila kwangu hauna makosa kwani wamekuhukumu kwa hila na hawakufuata utaratibu.
29088268_2080981262216013_3035855718591758336_n.jpg
 

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Messages
832
Points
1,000

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2014
832 1,000
Sasa hapo si amesha ingilia shauri la wambura? wamejuaje wambura hatashinda?
Ni kama Siasa tu Braza,
CUF Lipumba waliwafuta uanachama baadhi ya wabunge wao wa Viti maalum, hali iliyopelekea kupoteza Ubunge huo,
Sasa basi inagawa shauri lilifika Mahakamani lakini CUF Lipumba na Tume waliteua wabunge wengine bila kusubiri shauri lililoko mahakamani kuisha.
 

Betterhalf

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Messages
2,833
Points
2,000

Betterhalf

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2016
2,833 2,000
Makamu wa Rais is just a ceremonial leader tu.Kwa hiyo,kikubwa ni kwa Rais wa TFF awe na uwezo mkubwa wa kufanya na kusimamia delegations alizozifanya.
 

Forum statistics

Threads 1,390,490
Members 528,186
Posts 34,052,419
Top