Athumani iddi chuji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athumani iddi chuji

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Swahilian, Oct 19, 2009.

 1. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CHUJI

  Athumani Idi chuji, mwanasoka Tanzania.
  Amejaliwa vipaji, nashindwa kuelezea.
  Kakosa tu uchugaji,kondoo wangemezea.
  Hiki kipaji cha chuji, ni matatizo makubwa.

  Mpira kakomalia, shule hakupendelea.
  Mama alikubalia,kandanda we endelea.
  Wengi akawavutia ,nyotaye kuongelea.
  Hiki kipaji cha soka,au cha kusingizia.

  Ikawa chuji na Simba,wafurahi kidedea.
  Ukuta kashika nyumba, msimbazi kupepea.
  Sokani walikukumba, bado uliwachekea.
  Hivi soka ikipanda , akili zenu huruka?

  Mara ukaaanza kuponda, sekeseke za chakula.
  Ugomvi na wako nyanda, kisa chenu ni Jamila.
  Huna raha ukakonda, Simba ikawa madhila.
  Hiki kipaji cha Idi, kina wingi wa vituko.

  Usajili tafrani, hutaki tena nyumbani.
  Wasema huna amani,wataka kwenda jangwani.
  Wang’ang’ania benchini, nyumba mpya twigani.
  Kipaji cha Brambati, sijaona duniani.

  Kifungo kikawa mwisho, ukarudi uwanjani.
  Tuliona zako jasho, ulijituma dimbani.
  Walikwongeza na posho, washinda mwao vinywani.
  Athumani wa kipaji, mwige nduguyo Pius

  Taifa zima gumzo, madebe ukapigiwa.
  Maximo akwite mwanzo, kiungo bora kaitwa.
  Ukaanza zako bezo, dole kati likasutwa.
  Chuji hiki kipaji, kutukana mashabiki?

  Tamati yanigongea ,sifaze nisiandike.
  Sisahau ya Songea, yachekesha ya Mwandike.
  Soka hawakuchelea, miezi sita wamweke.
  Idi kipaji tumia, u’huru sasa tulia.

   
 2. chishango

  chishango JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Swahilian acha majungu tuletee tungo za kuamsha mioyo ya uzalendo kwa taifa letu linalodidimia, hicho si kitu muhimu ambacho watu tungependa kujishughulisha kufikiria kwa sasa
   
 3. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Pole sana Ndugu yangu!!1. jifunze kufikiri zaidi na ujue yapi majungu na zipi ni sifa na ipi ni hali halisi, je! haya hayatuhusu wanajamii,au weye si kati ya wanajamii? mie si mwanamajungu kama ufikiriavyo na hata siku moja sifundishi kuandika kama wewe usivyofundishwa kunishuku! amani iwe kwako, majibizano na ubishani ni hamasa kwa wasaka ukweli! japo si siku zote!! rudia tena na tena!!
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa hapo
   
 5. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  stuing artism
  kipaji kizuri endelea hivyohivyo na utunzni mzuri
  mependa sana jinsi ulivyoweza kufikiria na kutunza ujumbe wako hasa kwa mtu kama chuji mwenye majimambo na kipaji
  tuletee nyingine basi
  Great
   
 6. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ukuta kashika nyumba, yamaanisha sehemu ya ulinzi alikwepo Victor Costa a.k.a nyumba. Nafkiri umenipata hapo. Poa kakaa!
   
Loading...