Athumani Idd (CHUJI) amefichua mambo mazito!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,269
KIUNGO mahiri wa Bongo, Athumani Idd amefichua mambo mazito. Mchezaji huyo ametamka mambo ambayo kwa mtazamo wake anaona ndiyo yanayoifanya Yanga kupepesuka lakini amewasifu mastraika wa Simba.
Mchezaji huyo ambaye amewahi kuichezea Yanga misimu miwili na ikatwaa ubingwa, ametamka ya moyoni kwamba kwenye klabu hiyo kuna tatizo la umri, kujituma, hamasa na wachezaji kuogopana.

"Ukiangalia usajili wa Yanga msimu huu kwenye kiungo wapo vizuri sana, lakini Simba wametimia mbele. Simba inaonekana kufanya vizuri zaidi kwavile kuna utofauti mkubwa sana na Yanga kwa mchezaji mmoja mmoja hasa wale wa kigeni ambao wameletwa kubadili mchezo na kuzikwamua hizo timu," alisema kiungo huyo ambaye amewasifia wachezaji wawili tu wa kigeni Yanga ambao ni kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima na kipa Mghana Yaw Berko na kusisitiza kuwa hao ndio wanaostahili.

Wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga ambao Chuji anahoji viwango vyao ni Davies Mwape wa Zambia, Mghana Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza wa Uganda.

"Wachezaji wengi wa kigeni waliosajiliwa na Yanga wana umri mkubwa tofauti na wale wa Simba, hiyo inamaanisha kwamba asilimia kubwa ya wachezaji hao wanacheza kutimiza wajibu na kuendesha maisha yao, hawana malengo kwamba waongeze nguvu ili wanunuliwe na timu nyingine zaidi.
Tofauti na wenzao wa Simba ambao mtu kama Okwi (Emmanuel), Sunzu (Felix),Kago (Gervais) ni watu ambao wako njiani kuondoka muda wowote na umri unawaruhusu kufanya hivyo.

"Hivyo unakuta Yanga, mtu anacheza tu kwavile analipwa mshahara basi, lakini hawana uchungu kama walivyo wazalendo. Kuna wachezaji wengi sana wa hapa Tanzania ambao wangesajiliwa Yanga wangekuwa na msaada zaidi kwa timu kwavile wana uchungu,"alisema.

"Halafu kwa upande wa kujituma Simba wachezaji wanajituma sana na kuhamasishana kama timu, tofauti na Yanga ambako kuna wachezaji fulani ambao kila mmoja anaangalia mambo yake hata kama ni kuhamasishana hakufikii kiwango cha Simba.

"Simba kwa mfano mchezaji akikosea anakosolewa kabisa na wenzake na kila mtu waziwazi anaambiwa tatizo lako ni hili na lile jirekebishe, lakini kwa Yanga hicho kitu kipo kwa mbali sana. Sasa kwa timu ambayo inahitaji ushindi hakupaswi kuwa na tofauti kati ya mchezaji na mwingine.

"Simaanishi kwamba wachezaji wa Yanga hawapendani lakini ninaelezea hali halisi ambayo ipo kuwa watu ambao hawahangaiki na mambo ya wenzao kabisa, lakini mi naamini bado kuna muda na Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo kama wachezaji wakiamua kujituma zaidi na kujitolea kama familia moja,"alisisitiza mchezaji huyo wa zamani wa Polisi Dodoma.

Chuji aliichezea Yanga misimu miwili kabla ya kurejea Simba mwanzoni mwa usajili wa msimu huu lakini ghafla akatemwa kwa maelezo kuwa kocha Moses Basena hajaridhishwa na kiwango chake ndipo alipotimkia Villa Squad ambako hata hakucheza akaachana nayo na kuendelea na mambo yake.
 
Sielewi sana mambo ya ndani ya klabu hizi ila nadhani chuji kahit facts
 
Yanga Na Simba naona wanatia kichefuchefu tuu. Hizi timu zife tu. watu binafsi waanzishe timu zao km Azam ndo zitakuwa na mafanikio lkn hizi za kumilikiwa na wanachama waliobeba tofali wakati jengo sijui linajengwa mwaka 1954, hakutakuwa na maendeleo mpaka dunia itaisha. mmeona TP Mazembe juzi tu hapa wamenunua Ndege yao mpyaaa. Azam ana uwanja wake mzuri tu, hebu ona jengo la Simba mpaka aibu. Yanga pale Jangwani masikini kila siku ni story tu uwanja wa kisasa! fukuza wanachama wote wakalime vijijini huko hatutaki kuona watu wanaganga njaa kwenye viwanja vya klabu husika wakisubiri wafadhili mbuzi wapite waombe buku buku na kuendeleza majungu.
 
Mimi huwa sifuatilii mamipira yenu ya Bongo. Huwa naangalia EPL tu
 
Japo na-enjoy EPL kama walivyosema wengine hapo juu, bado nina concern na soka letu la bongo....

With all due respect, pasipo kujali chuji ni nani kwenye macho ya wengi, naweza kusema amenena mambo ya msingi ya kutiliwa umaanani na viongozi wa soka la bongo......

Hakika soka la nyumbani linatia aibu..............aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!
 
KIUNGO mahiri wa Bongo, Athumani Idd amefichua mambo mazito. Mchezaji huyo ametamka mambo ambayo kwa mtazamo wake anaona ndiyo yanayoifanya Yanga kupepesuka lakini amewasifu mastraika wa Simba.
Mchezaji huyo ambaye amewahi kuichezea Yanga misimu miwili na ikatwaa ubingwa, ametamka ya moyoni kwamba kwenye klabu hiyo kuna tatizo la umri, kujituma, hamasa na wachezaji kuogopana.

"Ukiangalia usajili wa Yanga msimu huu kwenye kiungo wapo vizuri sana, lakini Simba wametimia mbele. Simba inaonekana kufanya vizuri zaidi kwavile kuna utofauti mkubwa sana na Yanga kwa mchezaji mmoja mmoja hasa wale wa kigeni ambao wameletwa kubadili mchezo na kuzikwamua hizo timu," alisema kiungo huyo ambaye amewasifia wachezaji wawili tu wa kigeni Yanga ambao ni kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima na kipa Mghana Yaw Berko na kusisitiza kuwa hao ndio wanaostahili.

Wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga ambao Chuji anahoji viwango vyao ni Davies Mwape wa Zambia, Mghana Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza wa Uganda.

"Wachezaji wengi wa kigeni waliosajiliwa na Yanga wana umri mkubwa tofauti na wale wa Simba, hiyo inamaanisha kwamba asilimia kubwa ya wachezaji hao wanacheza kutimiza wajibu na kuendesha maisha yao, hawana malengo kwamba waongeze nguvu ili wanunuliwe na timu nyingine zaidi.
Tofauti na wenzao wa Simba ambao mtu kama Okwi (Emmanuel), Sunzu (Felix),Kago (Gervais) ni watu ambao wako njiani kuondoka muda wowote na umri unawaruhusu kufanya hivyo.

"Hivyo unakuta Yanga, mtu anacheza tu kwavile analipwa mshahara basi, lakini hawana uchungu kama walivyo wazalendo. Kuna wachezaji wengi sana wa hapa Tanzania ambao wangesajiliwa Yanga wangekuwa na msaada zaidi kwa timu kwavile wana uchungu,"alisema.

"Halafu kwa upande wa kujituma Simba wachezaji wanajituma sana na kuhamasishana kama timu, tofauti na Yanga ambako kuna wachezaji fulani ambao kila mmoja anaangalia mambo yake hata kama ni kuhamasishana hakufikii kiwango cha Simba.

"Simba kwa mfano mchezaji akikosea anakosolewa kabisa na wenzake na kila mtu waziwazi anaambiwa tatizo lako ni hili na lile jirekebishe, lakini kwa Yanga hicho kitu kipo kwa mbali sana. Sasa kwa timu ambayo inahitaji ushindi hakupaswi kuwa na tofauti kati ya mchezaji na mwingine.

"Simaanishi kwamba wachezaji wa Yanga hawapendani lakini ninaelezea hali halisi ambayo ipo kuwa watu ambao hawahangaiki na mambo ya wenzao kabisa, lakini mi naamini bado kuna muda na Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo kama wachezaji wakiamua kujituma zaidi na kujitolea kama familia moja,"alisisitiza mchezaji huyo wa zamani wa Polisi Dodoma.

Chuji aliichezea Yanga misimu miwili kabla ya kurejea Simba mwanzoni mwa usajili wa msimu huu lakini ghafla akatemwa kwa maelezo kuwa kocha Moses Basena hajaridhishwa na kiwango chake ndipo alipotimkia Villa Squad ambako hata hakucheza akaachana nayo na kuendelea na mambo yake.

Kumbe bangi sometime inapoa, leo chuji kaongea maneno ya kitafakuri sana. Nijuavyo kuhusu usajili kwa kalabu ya Yanga, ni dili ya viongozi kutamka bei kali za wachezaji lakini pesa hiyo huishia mifukoni mwao na hata hao wanachama huwa hawajui kuwa wamepigwa changa la macho. Ni uchafu mtupu uliopo Yanga hasa linapokuja suala la utawala, pale hakuna soka ni genge la wahuni kuwezeshana kuishi mjini, hawaishi kuanzisha bifu na TFF eti wanaonewa, oneni haya kushindwa hata kujenga uwanja wa maana, mnashindwa na hata Azam ya juzi tu. Hebu fikirieni jamani lau wangeamua kujenga nguzo moja tu kwa mwezi, leo wangekuwa na majukwaa mangapi uwanja wa shamba la mbu. Shame on them kwa kuwaghilibu watu eti wanafanya usajili kabambe. Louis sendeu unajitafutia dhambi kwa kuwasemea matapeli
 
Back
Top Bottom