Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
KIUNGO mahiri wa Bongo, Athumani Idd amefichua mambo mazito. Mchezaji huyo ametamka mambo ambayo kwa mtazamo wake anaona ndiyo yanayoifanya Yanga kupepesuka lakini amewasifu mastraika wa Simba.
Mchezaji huyo ambaye amewahi kuichezea Yanga misimu miwili na ikatwaa ubingwa, ametamka ya moyoni kwamba kwenye klabu hiyo kuna tatizo la umri, kujituma, hamasa na wachezaji kuogopana.
"Ukiangalia usajili wa Yanga msimu huu kwenye kiungo wapo vizuri sana, lakini Simba wametimia mbele. Simba inaonekana kufanya vizuri zaidi kwavile kuna utofauti mkubwa sana na Yanga kwa mchezaji mmoja mmoja hasa wale wa kigeni ambao wameletwa kubadili mchezo na kuzikwamua hizo timu," alisema kiungo huyo ambaye amewasifia wachezaji wawili tu wa kigeni Yanga ambao ni kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima na kipa Mghana Yaw Berko na kusisitiza kuwa hao ndio wanaostahili.
Wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga ambao Chuji anahoji viwango vyao ni Davies Mwape wa Zambia, Mghana Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza wa Uganda.
"Wachezaji wengi wa kigeni waliosajiliwa na Yanga wana umri mkubwa tofauti na wale wa Simba, hiyo inamaanisha kwamba asilimia kubwa ya wachezaji hao wanacheza kutimiza wajibu na kuendesha maisha yao, hawana malengo kwamba waongeze nguvu ili wanunuliwe na timu nyingine zaidi.
Tofauti na wenzao wa Simba ambao mtu kama Okwi (Emmanuel), Sunzu (Felix),Kago (Gervais) ni watu ambao wako njiani kuondoka muda wowote na umri unawaruhusu kufanya hivyo.
"Hivyo unakuta Yanga, mtu anacheza tu kwavile analipwa mshahara basi, lakini hawana uchungu kama walivyo wazalendo. Kuna wachezaji wengi sana wa hapa Tanzania ambao wangesajiliwa Yanga wangekuwa na msaada zaidi kwa timu kwavile wana uchungu,"alisema.
"Halafu kwa upande wa kujituma Simba wachezaji wanajituma sana na kuhamasishana kama timu, tofauti na Yanga ambako kuna wachezaji fulani ambao kila mmoja anaangalia mambo yake hata kama ni kuhamasishana hakufikii kiwango cha Simba.
"Simba kwa mfano mchezaji akikosea anakosolewa kabisa na wenzake na kila mtu waziwazi anaambiwa tatizo lako ni hili na lile jirekebishe, lakini kwa Yanga hicho kitu kipo kwa mbali sana. Sasa kwa timu ambayo inahitaji ushindi hakupaswi kuwa na tofauti kati ya mchezaji na mwingine.
"Simaanishi kwamba wachezaji wa Yanga hawapendani lakini ninaelezea hali halisi ambayo ipo kuwa watu ambao hawahangaiki na mambo ya wenzao kabisa, lakini mi naamini bado kuna muda na Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo kama wachezaji wakiamua kujituma zaidi na kujitolea kama familia moja,"alisisitiza mchezaji huyo wa zamani wa Polisi Dodoma.
Chuji aliichezea Yanga misimu miwili kabla ya kurejea Simba mwanzoni mwa usajili wa msimu huu lakini ghafla akatemwa kwa maelezo kuwa kocha Moses Basena hajaridhishwa na kiwango chake ndipo alipotimkia Villa Squad ambako hata hakucheza akaachana nayo na kuendelea na mambo yake.