Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende


Moja ya gari ambalo ni noma barabarani basi ni hili ndinga,nakumbuka jana nikiwa natokea maeneo ya RUFIJI kuja DAR ilinipa hii gari kama nimesimama

Nikiwa kwenye mwendo wa speed 100 sehemu yenye mwinuko kidogo huku nikijiona mimi ni bingwa barabarani niliiona gari likija kwa nyuma yangu kwa kasi sana ilikuwa kama mita 130 nyuma yangu basi nikasema haiwezekani nikapitwa kijinga kiasi hicho nikachochea moto nikafikisha speed 125 hivi sasa nilichokuja kunishangaza ni namna yule jamaa wa crown alivyokuwa anaomba site apite yaani ilikuwa ni kitendo cha dk 6 ile gari ilinipita na sikuiona tena.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuendesha CARINA Ti lakini niliambulia patupu
Hizi crown ni gari za safari ingawa inameza mafuta kama jini ila ni chombo cha maana nami namuomba mungu huku nikijichanga nichukue hii ndinga

Hongereni wote mnaoendesha Athletes Crown au mnaomiliki hii ndinga hakika hamjakosea
Nimemkimbiza mmoja Chalinze Moro alianza kupita nikampa space afu nikasema ngoja nizibue nozel kwa kibaby walker changu nilimpita km kasimama akabaki ananishangaa...
 
Mkubwa, Volvo, VW, BMW, sahani inaenda hadi 260km/h mbaya zaidi unavyokanyaga wese ndio gari iko stable haitetereki.

Hapo itakua suala la ujasiri wa dereva, lakini kama tunaongelea uwezo wa gari, haziwezi kushindana.
European cars zipo hivi boss. Jaribu na Opel
 
Dah hongereni jf maana humu kila mtoa post ana ndinga
Jukwaa la mambo ya magari, atakujaje kuandika asiye na gari, wala kuwahi kumiliki.
Na wala siyo fundi.
Ingawa amenishangaza jamaa mmoja hapo juu, anamiliki gari aina ya Volkswagen, ila hajui ni apollo ama toleo gani, Sijui anaihudumiaje kwenye matengenezo.
 
Back
Top Bottom