Emmanuel J. Buyamba
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 1,167
- 651
1.Yanachonifikirisha ndicho nilichokuuliza,sijui kwa nini unauliza swali ambalo jibu lake limo humohumo.Nilikuuliza hivi:
"Hayo mengine unayosema yapo automatic we unayaona ni ya kawaida tu na hayakufikirishi chochote,sasa hata kama tungekuwa tunamuona kabisa Mungu(achia kumjua tu automatically) ndio ingekuwa nini sasa?"
Unaacha kujibu halafu unakimbilia kuuliza maswali wakati umeacha kujibu swali muhimu katika tunachojadili.
Yamenifikirisha na ndipo nikakuhoji hivi,kwa nini Mungu wenu (iwapo kweli kaumba watu) kawawekea suala la kwenda haja kubwa liwe la automatic (pasina kuhitaji hadi padri ama shehe akwambie umebanwa nenda chooni) ila suala la uumbaji na uwepo wake lihitaji padri au shehe?
Je,kwake Mungu wenu suala la haja kubwa ndiyo la msingi zaidi, akatufunulia automatically ila la uwepo wake halina thamani sana akaacha kutupa u automatic wa kumjua?
2.Unaposena kumuona ingekuwa niñi sasa, hapo hujajibu swali.
Wala mimi sijataka hadi nimuone.
Nachotaka kujua toka kwako ni alishindwa kujidhihirisha ktk njia isiyoacha maswali kama ambavyo ilivyo leo, kiasi cha madhehebu kuwa mengi?
Naomba majibu,kama mjadala ni mzito kwako waweza potezea na kukaa tu pembeni kama alivyofanya Mr parasite (genious baraka ) hapo juu.