Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Wewe aliyekwambia hizi ni hadithi za watu ni nani? Hivyo vitabu vya wanasayansi unavyotumia kupinga uwepo wa Mungu ni nini kama si hadithi zao pia?

Kama Mungu hayupo hilo neno Mungu umelitoa wapi?
Hujajibu swali langu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo, na si hadithi za watu tu?
 
Hujajibu swali langu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo, na si hadithi za watu tu?
Ni jinsi binadamu na viumbe wengine wanavyoumbika kutoka katika mfumo wa mbegu na kuwa kiumbe kamili -huo ni uthibitisho tosha kuwa Mungu yupo.

Nimeshakuthibitishia: Nakuuliza na wewe unijibu,kama Mungu hayupo hilo neno Mungu umelitoa wapi?
 
Kama kitu kisichokuwepo hakijulikani, wewe umejuaje hakijulikani?

Unajua kujua kitu hakijulikani ni kujua?

Unajua ukisema umejua kitu hakijulikani unaji contradict kwa sababu ukishajua kitu hakijulikani umeshajua hicho kitu na hakiwezi tena kuwa hakijulikani?

Unajua kitu kinaweza kutajwa kwa hadithi tu, bila kuwapo?

Unajua characters wa hadithi za kutunga kina James Bond, Willy Gamba, Kipepe, Ndumilakuwili, Lodi Lofa, Madenge, etc wanajulikana lakini hawapo kiukweli nje ya hadithi?

Sasa mtu akikwambia Mungu naye ni character wa hadithi tu kama hao, na kiukweli hayupo, utasema kwa vile Willy Gamba kaandikwa kwenye hadithi za Aristablus Elvis Musiba, utasema ni lazima yupo vile vile, kwa sababu huwezi kufikiria kitu ambacho hakipo?
Mimi najua kipo(yupo) nakuuliza hilo swali wewe na wenzio mnaopinga uwepo wake! Halafu umejiona ukwepaji wako wa maswali!? Wewe ndo unaleta hadithi sasa.....badala ya kujibu swali unakuja na swali na hiyo ndiyo tabia yenu.
 
Ndege ikiwa angani ikipata msukosuko, Atheist anakuwa wa kwanza kutamka..Ooh my God..... ukweli ni kuwa hakuna Atheist hata mmoja duniani, kingunge ngombale alikuwa na maswali yasiyokuwa na majibu juu ya imani yake,, tukakurupuka ni Atheist,, na ili imani iwe thabiti lazima ikuachie wasiwasi mahali, ukielewa kila kitu, then utofauti wako na Mungu uko wapi
 
Hakuna tofauti hapo kwa sababu kujadili usahihi wa mambo tu pasina kueleza hayo mambo yenyewe ni yapi hakuna tofauti na kujadili tu mambo.
😆😆😆 Kiranga hapo atakuzungusha kibishibishi akishakosa jibu,hiyo ni kawaida yake na ndiyo njia yake rahisi aipendayo kukwepa maswali yanayomshinda.
 
Mimi najua kipo(yupo) nakuuliza hilo swali wewe na wenzio mnaopinga uwepo wake! Halafu umejiona ukwepaji wako wa maswali!? Wewe ndo unaleta hadithi sasa.....badala ya kujibu swali unakuja na swali na hiyo ndiyo tabia yenu.
Hujajibu swali langu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo, na si hadithi za watu tu?
 
😆😆😆 Kiranga hapo atakuzungusha kibishibishi akishakosa jibu,hiyo ni kawaida yake na ndiyo njia yake rahisi aipendayo kukwepa maswali yanayomshinda.
Hujajibu swali langu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo, na si hadithi za watu tu?
 
😆😆😆 Kiranga hapo atakuzungusha kibishibishi akishakosa jibu,hiyo ni kawaida yake na ndiyo njia yake rahisi aipendayo kukwepa maswali yanayomshinda.
Sifa za kusifiwa kuwa ni mbishi ndizo zinazomfanya kulazimisha ubishi hata usio na maana,haoni tabu hata kubishana jambo ambalo halihusiani kabisa na mada.
 
Kiranga nimeshakuthibitishia tayari swali lako mbona!! Soma post 849#

Kuna swali lako unatakiwa kujibu kwenye hiyo post.
Huo si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Hiyo ni logical non sequitur.

Unajua logical non sequitur ni nini?
 
Kiranga nimeshakuthibitishia tayari swali lako mbona!! Soma post 849#
Kuna swali lako unatakiwa kujibu kwenye hiyo post.
Atakusumbua tu huyo ana miaka na miaka yeye anadai kuthibitishiwa Mungu na ndiyo silaha yake nje ya hapo hana kujadili humu ataongea utumbo hadi utamshangaa msomaji vitabu huyo. Mimi huwa namwambia tu siwezi kuthibitisha basi.
 
Nimeona pia na namjua kwa kumsoma humu. Aisee nami inabidi nimuage tu kwa kweli..
 
Kwa jamii iliyostaarabika atheists ni watu wa kawaida, anaesema Mungu hayupo na yule anaeamini yupo, hakuna mwenye uhakika, hivyo ngoma draw!! Binadamu tuheshimiane tu!! Imani weka pembeni
 
Kiranga bye bye! Huna majibu kaka ni ubishi ubishi tu na usumbufu,kuzungushana kama watoto👋👋
Huo si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Hiyo ni logical non sequitur.

Unajua logical non sequitur ni nini?
 
Kiranga bye bye! Huna majibu kaka ni ubishi ubishi tu na usumbufu,kuzungushana kama watoto
Wewe sio tu hujui uchambuzi na mambo kwa kina, hata mtu akitaka kukuletea uchambuzi ujue mambo kwa kina huna utashi wa kutaka kujua mambo kwa kina.

Umetoa jibu.

Jibu lako lina makosa ya kimantiki.

Lina kosa ambalo kimantiki kwa Kiingereza kosa hilo linaitwa "logical non sequitur".

Nakuuliza kama unajua kwamba jibu lako lina kosa la kimantiki la logical non sequitur, nakuuliza unajua logical non sequitur ni nini.

Unakimbia.

Sio tu huna jibu.

Huna hata utashi wa kujua jibu.

Ungekuwa na utashi kidogo tu, ungeniuliza nikujuze ulipokosea.
 
Nimeona pia na namjua kwa kumsoma humu. Aisee nami inabidi nimuage tu kwa kweli..
Suala la uwepo wa Mungu ni pana sana ila mtu anakulazimisha uthibitishe nia kwamba ushindwe na yeye kwake ndio ushindi.
 
Hujajibu swali langu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo, na si hadithi za watu tu?

Hivi unajua nini maana ya HADITHI ?

Na wewe unawezaje kutofautisha kati ya "Hadithi za watu" na kinyume chake ?
 
Similar Discussions

34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom