Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

Allaha katika Quran ametwambia ivi:

4:124. "Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende."
sasa hii ina uhusiano gani na kuonana na Mungu??ukiwa hapa duniani?
 
sasa hii ina uhusiano gani na kuonana na Mungu??ukiwa hapa duniani?
Hatujaja duniani kumuona Mungu, tumeletwa duniani kufanya mema ili tuingizwe peponi, huko tutatapata majibu ya maswali yote unayoyajua na usiyoyajua, huko ndio tutayajua yote kinaga ubaga.
 
Naona tayari umeanza kujishtukia kama nnakokupeleka utavurugika.

Mungu wetu ni perfect anajua mwisho wetu anajua lini nitakufa na hukmu yangu ya mwisho ni ipi. Haiwezekani mwanzo aone ivi na baadae ije itokee tofauti.

Sasa namie nakuomba basi unijibu? kama huna jibu sema tu. Kwani ukiamua kutomuamini huo ni uamuzi wako na uko huru.

Utajuaje kama maono yake yamebadilika baada ya kuacha kusali ikiwa hujui mwanzo maono yake ni yapi? Nasubiri jibu

Unajibu kwa kukurupuka hujui hata mantiki ya hilo swali nililokuuliza na sizani kama umelielewa

Mimi sijazungumzia kubadilika kwa maono au lah, na ndio maana nilikua nasisitiza kuuliza kua kama naye anatabia ya kukosea ili niweze kujenga hoja kupitia jibu utalonipa

Nimeuliza kama mungu anajua kila kitu na hakuna kitu utachokifanya leo hii kikawa kigeni machoni mwake kwasababu yeye ni mungu asiyekosea alichokiona ni lazima kiende sawa sawa. Sasa wewe leo hii ukiamua kutoenda kanisani au msikitini utakua umebadilisha chochote katika ujuzi wake kuhusu hatma yako???
 
Kutokujua kwangu hakubadilishi alilolipanga Mungu. Lakini vile vile kutojua kuwa kwangu ndio sababu ya mimi kufanya ibada kuomba kuwa alilolipanga ni jema. Kutokujua kwangu alilopanga Mungu kunanifanya nisijue kama amebadilisha maono. Sijui kitu gani huelewi.

Ukuta unajua kama hausogei, ukiusukuma itakuwa unajichosha, ila gari unaamini kuwa inaweza kusukumika, basi ukiisukuma hujichoshi, unafanya kitu ambacho kinawezekana.

Mungu akijua kua utaenda motoni, wewe ukiwa unafanya ibada kwasababu hujui alilolipanga mungu juu yako hakubadilishi chochote
 
Huyo Mungu hawezi kujitetea mwenyewe mpaka wewe ukauke sauti humu !!!
Kwani mbona wewe unatokwa mishipa humu kusema hakuna Mungu kwani kama kitu hakipo si hakipo na kila mtu anaona kiwa kweli hakipo sasa kuna haja gani wewe kutwa kubishana na watu kuwa hakuna Mungu?
 
Hehehe, em soma ulichoandika mara mbili mbili kama hata we mwenyewe unaweza kukielewa.
Seems to me ambaye hajui anachokitafuta wa kwanza ni wewe, washika dini tunajua wanachokitafuta, hawatokipata lakini sababu hakipo, sio wa kwanza kufa, mtakufa mungu hajarudi, watoto wenu na wajukuu watakufa hajarudi, miaka elfu ijayo watakuwepo wengine watakufa hajarudi tu. Endeleeni kumsubiri. Hamuelewi atheists msijifanye mnawaelewa, atheists wengi walianzia kwenye dini wakakua wakaona ni upuuzi wakatupa pembeni, wanajua dini ilivyo, nyie msiojua u-atheist ulivyo coz hamjawahi kua msijifanye mnajua zaidi.
Unaweza kuwa muaminii Mungu kwa sababu umezaliwa na kukuzwa na hiyo imani ya Mungu kama ambavyo huko china au korea watu wengi huzaliwa na kukuzwa na hali ya kutokuwa na imani ya dini wala Mungu,hivyo kwao hawaamini Mungu kwa sababu ndivyo walivyo lelewa hadi kukulia katika mazingira hayo.

Hivyo suala la atheists kwamba walikuwa wakiamini Mungu mwanzoni si jambo la kuwafanya kuwa wana hoja za msingi maana wapo pia wanaomini Mungu sasa ambao nao walikuwa atheists hivyo kungekuwa na hoja za msingi basi wasingeacha huo msimamo na kuja kuamini uwepo wa Mungu.

Tatizo watu wangekubali kuwa suala la uwepo wa Mungu ni imani hivyo tungejadili kwa kuangalia sababu za msingi zenye kuwapelekea watu kukubali imani ya uwepo wa Mungu basi tungepiga hatua kwenye hii mijadala.
 
Tatizo ndo hilo, kila kitu mnaishia kusema imani, ukweli ni kua watu mpo dini flani kwankua mlizaliwa huko, exactly kama ulivyosema, inakua ngumu kuacha kitu ambacho ulikua brain washed toka utotoni. Miungu ipo zaidi ya 3,000 na mingi inapingana hehehe anayeamini wa kwake ndiye wa kweli anajidanganya.
Mungu kama yupo basi kafeli, yeye kila kitu analaumu shetani tu huku kamtengeneza mwenyewe hehehe mara mia niamini Thor. Ukweli ni kua hakuna mwenye proof yoyote ile ya uwepo wa mungu, tutaongea wee miaka nenda rudi hajawahi prove mtu hata moja, hata vitabu vya dini ni ambiguous mno. Total waste of time nafurahi sana niliachana na huo upuuzi
 
Sio tunaishia kusema tu bali huo ndio ukweli kwamba suala la uwepo wa Mungu ni jambo la imani,tusipoelewana hapa huko hakuna kitakachoeleweka na ndiyo maana unakuja na za et hakuna proof ya uwepo wa Mungu kitu ambacho inaonesha tatizo ninalolisema hapa. Kuna watu walikuwa kama wewe wenye misimamo ya kuwa Mungu hakuna na hakuna proof ya uwepo ila sasa wamekubali uwepo wa Mungu na si kwamba walipata proof ya uwepo wa Mungu.

Kwahiyo mie mtu kama wewe unayejiona uko sahihi kwa huko kwako kusema hakuna Mungu naona kawaida tu najua ni misimamo tu kama ambayo wengine walikuwa nayo na sasa wamebadili,na si kwamba una sababu au hoja za msingi sana maana ingekuwa basi tusingeona watu kama nyie kuja kukubali uwepo wa Mungu bila hata proof. Ukweli ni kwamba wote sie(waamini Mungu na wakana Mungu) misimamo tuliyonayo ni zaidi ya hoja tunzotoa hapa,na ndiyo wewe unaona sawa tu kwamba hakuna Mungu na kuona ajabu inakuje wengine hawaoni unachokiona wewe na wengine pia tunaona hivyohivyo ni vp mtu inawezekana kusiwe na Mungu na vp wewe unashindwa kuona dalili na sababu za uwepo wa Mungu? Na ndiyo maana si ajabu atheist kuja kuamini Mungu na muamini Mungu kuja kuwa atheist ni kawaida tu.
 
Sijaona swali la kiranga lisilojibika. Kikubwa ni kwamba yeye hajibu maswali ukimuuliza.
mfano mkuu ukiulizwa kwanini Mungu ameamua kujificha kabisa na hakuna ambaye amewahi kumuona.

Hilo ni moja ya swali la.kiranga

Hebu tupe wewe jibu sahihi sio tu ujibu swali tupe jibu sahihi na uthibitishe pia mkuu

Note : am not an atheist
 
Unapouliza maswali kama haya, basi ukubali majibu ya mtu kwa mujibu wa yule Mungu amjuae yeye na sio kulazimisha kwa mungu umtakae wewe. Wakina Kiranga hawajui jinsi gani ya kuhoji uwepo wa Mungu, na wao huwa tayari kichwani mwao wanafikra zao juu ya Mungu yupi wanafikiri kila mtu anamuamini.

Mfano, ukitaka kujadiliana na mimi suala la uwepo wa Mungu basi ujue mimi Namuamini Allah, sasa ili upinge uwepo wake, basi tumia imani yangu ya Allah kuuliza swali. Mfano ukija ukanihoji uwepo wa Mungu ikiwa reference yako ni ng'ombe basi ntakwambia kawaulize wanaomuabudu huyo ng'ombe.

Sasa swali kama hilo ulilouliza;

- Mungu wangu hajaamua kujificha. kujificha ni kitendo cha kutaka usionekane na yoyote.
So kuna allah

So Mungu wetu sisi wakristo si wa kweli

Mambo kama haya ndo hufanya wakina kiranga kutuona sisi waamini Mungu watu tusiojitambua

Tukianza kutetea uwepo wa Mungu tunaungana

Ila sasa baada ya hapo utasikia mkristo ni kafiri

What the fvck !
 
Binaadamu hatuna uwezo wa Kumuona Mungu.

Hata katika Bibilia sababu ya Mungu kutomuona limetajwa. huwa nashangaa kwanini huwa hamkisomi kitabu chenu wenyewe mkakielewa vizuri?

Exodus 33:20 But He said, "You cannot see My face, for no man can see Me and live!"
Hapa wakristo na waislamu tutaungana subiri baadae

Aisee ... Hizi issue ni complicated sana ukubali au ukatae

Nashangaa sana ani .. Tunatumia Nguvu nyingi kumtetea mtu ambaye hajaokba tumtetee

Hivi ni wapi aliwahi tuombe tumthibitishe kama yupo
 
Uzi ni mzuri lakini hauna uhalisia
Mtu anaamini Mungu ni mjuzi wa kila kitu ila et kuna watu Mungu hajui hatima zao kwa sababu hao watu hawajajikabizi kwake hivyo Mungu hajui hatima zao,sasa hapo utasemaje Mungu anajua kila kitu!
 
Mshahara wa dhambi ni mauti ni mtoto mdogo kazaliwa na kufa kapata mshahara wake kwa dhambi ipi aliyoifanya....?
Hivi pale edeni simba nae alikula tunda maana naye anakufa wakati aliykula tunda na mwanadam
Aaah kwanza inachosha vingine ni uchwara tu
Mungu hakunaga kitu kama hicho popote pale
Duh hatari sana mkuu
 
Kiukweli wanaojiita hawaamini uwepo wa Mungu hawajui wanachokitafuta.Na shida ni kwamba wanaowajibu pia hawajui wanachokijibu.
.
Uwepo wa Mungu upo ndani ya Mtu. Na ili Mungu awepo kwako ni lazima utimize mapenzi yake.

Sasa inashangaza anatokea kiumbe anasema " Mungu hayupo" na kwa wakati huo hatimizi mapenzi ya Mungu na wala hajishughulishi kuyajua mapenzi ya Mungu Bali anafuata mapenzi yake mwenyewe.

Halafu wanatokea watu wanaowajibu kuwa Mungu yupo,huku watu hao wakiwa hawayatimizi mapenzi ya Mungu yaani na wenyewe wanafuata mapenzi yao tu!

Mungu anadhihirishwa kwa matendo mema na kuishi vyema. Wote tunaoamini uwepo wa Mungu tungeishi kwa mapenzi ya Mungu hawa wanaojiita Atheists wala hata tusingewasikia.

Tujitahidi jamani kuwasaidie wenzetu kwa matendo yetu mema na upendo ili tuwajibu kwa tunayoyafanya.

Na kizuri zaidi tunajua Cha kufanya yaani tumpende Mungu,tujipende na kuwapenda wote Kama tujipendavyo
Matendo mema sio tafsiri ya uwepo wa Mungu.

Ipo hivi, uwepo wa Mungu ni project kama ilivyo project ya kuweka mipaka na kugawa majina yaa nchi.
Au kama ilivyokua project ya kuunda herufi na kuzipa majina
Au kama ilivyokua project ya kuunda namba na mengi kadharika.

Ukiangalia lengo la hayo yote, ilikua ni kuifanya dunia iishi kwa utamaduni mmoja.

Nitaendelea....
 
Unapouliza maswali kama haya, basi ukubali majibu ya mtu kwa mujibu wa yule Mungu amjuae yeye na sio kulazimisha kwa mungu umtakae wewe. Wakina Kiranga hawajui jinsi gani ya kuhoji uwepo wa Mungu, na wao huwa tayari kichwani mwao wanafikra zao juu ya Mungu yupi wanafikiri kila mtu anamuamini.

Mfano, ukitaka kujadiliana na mimi suala la uwepo wa Mungu basi ujue mimi Namuamini Allah, sasa ili upinge uwepo wake, basi tumia imani yangu ya Allah kuuliza swali. Mfano ukija ukanihoji uwepo wa Mungu ikiwa reference yako ni ng'ombe basi ntakwambia kawaulize wanaomuabudu huyo ng'ombe.

Sasa swali kama hilo ulilouliza;

- Mungu wangu hajaamua kujificha. kujificha ni kitendo cha kutaka usionekane na yoyote.
Kwanin uamin Allah na sio ng'ombe
 
Back
Top Bottom