Athari za uongozi dhaifu zilizoletwa na Uchama kuanzia Wenyeviti wa vitongoji hadi madiwani zinavyokinzana na maendeleo

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,753
7,075
Athari za uongozi dhaifu zilizoletwa na uchama kuanzia wenyeviti wa vitongoji hadi madiwani zinavyokinzana na maendeleo.

Tafiti ndogo niliyoifanya mikoa mbalimbali hasa mkoa wa Kagera nimegundua kwamba mwaka wa ushindi wa kishindo ambao wapinzani walisusa uchaguzi viongozi wa CCM wengi wao waliteuliwa kwa mashinikizo bila kujali weledi wa uongozi kati ya mtu na mtu, hata kama mtu apendwi waliletewa tu hata kama alikuwa na tabia chafu.

Hii imeleta mahusiano mabaya kiasi kwamba wanaongoza kwa shida, hawapati taarifa nzuri za kuleta maendeleo kwani watu wamewazira. Mkoa wa Kagera wizi wa mifugo, pikipiki, mazao kama vanila, kahawa, mahindi umezidi wananchi wamekata tamaa. kwa sasa ukilima vanila ni kesi, utavamiwa kipindi cha mavuno mwezi wa sita wanangoa vanila ambayo ina zao pamoja na marando yake.

Vanila emeleta hatari zaidi ya albino maana inabidi uilinde usiku na mchana. Nilipopeleleza nikaambiwa" matatizo yetu tumpelekee nani, "viongozi wenyewe walikuwa wezi, wengine walikuwa vinara wa kununua mali ya wizi.

Mfano,ukienda tarafa ya mshamba wezi walikuwa wanakodi bunduki ya CRDB wanaenda kuteka, mpaka siraha hiyo ilivyokamatwa mlinzi kafungwa mwaka mmoja, inasemekana mlinzi ni kakayake na mwenyekiti na mwenyekiti alifanya mipango na hakimu akamfunga miaka kidogo kwa kesi ya unyanganyi wa kutumia siraha.

Lakini haya yote yanasababishwa na polisi wa kituo cha nshamba kuandaa kesi dhaifu. Nshamba na Kishanda kimekuwa kitengo cha waarifu wanaolindwa na police, wananchi wanapeleka orodha ya waarifu lakini haifanyiwi kazi,nilipokuja kushangaa hata aliyekuwa mkuu wa police dar A.

Tibaigana ameibiwa mara kibao! na tena akiwepo nyumbani. ulegevu wa uongozi wa vitongoji hadi diwani ndio chanzo. wanadhauliwa kuwa hawakuchaguliwa.. mwenyekiti mmoja alinisurika kuchapwa makofi na muhanga aliyeibiwa mbuzi na wezi akawatambua na hakuchukua hatua.

Nilipoenda kwa mtendaji wa kata kumuuliza kulikoni, nilijibiwa wananchi wenyewe ukiitisha mkutano wa kupigia kura waarifu wanawajaza viongozi hivyo niliamua kuacha.

Suluhisho kwa Mama Samia kuondoa tatizo hili, asijali uchama wa kushinda kwa kishindo, ikitokea wananchi wanamkataa kiongozi awe mbunge, diwani, wenyeviti wanakataliwa waitishe chaguzi wasijari pesa itakayopotea.
 
Mama samia ni kweli viongozi wengi wa serikali za mitaa hawana ushirikiano mzuri na wananchi maana wananchi wengi wanasema hawawatambui hebu hili suala litafutie suluhisho
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom