Athari za unyonyaji kwa wasanii zinavyomtesa Bi Kidude | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athari za unyonyaji kwa wasanii zinavyomtesa Bi Kidude

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Sep 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]
  Bi Kidude​

  KUBADILIKA ya sanaa kutoka katika hali ya ridhaa kulikuja baada ya serikali kuzindua sera mpya ya Utamaduni mwaka 1999, ambayo ndani yake inatoa dhamana kwa watu binafsi (wadau) kujiingiza kwenye fani hiyo na serikali kubaki kama msimamizi mkuu.

  Hapa ,kulianza mfumuko wa wafanyabiashara wengi kujiingiza kwenye sekta ya sanaa, huku wasanii na wapenzi wao wakibaki kwenye mazingira ridhaa bila kipato. Fani hii ya sanaa imekumbana na changamoto nyingi zinazowakwamisha wasanii kufikia malengo na moja ya sababu ni kukithiri wizi wa kazi zao kunakofanya na wachache.Pia Mapromota wamekuwa wakiwarubuni wasanii kwa kuwafanyisha kazi zisizo na mikataba, lakini kwa upande wa pili kazi hizo zimekuwa zikiwanufaisha wao.Tabia hiyo ndiyo ambayo leo hii imewaacha wasanii wakidhalilika, na hapa ningependa kumtoea mfano mwimbaji mkongwe wa muziki wa Mwambao, Fatuma Baraka 'Bi Kidude'.

  Bi Kudude baada ya kusimama jukwaani kwa miaka mingi akitoa burudani, sasa ni wazi anaonekana kuchoka kwa jinsi hali yake ilivyo.Mwili unapochoka, mambo mengi yanaweza kujitokeza ikiwamo na magonjwa yanayotokana na umri. Ndivyo ilivyo kwa msanii huyu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

  Kwa sasa, msanii huyu mkongwe amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza fahamu, lakini kwa jinsi anavyoongea unaweza kudhani kwamba bado ana nguvu kutokana na ukali wa sauti yake.Sitaki kuingia ndani sana kuhusiana na maradhi yanayomsumbua, lakini ukweli ni kwamba maisha anayoishi kwa sasa ni kielelezo cha unyonyaji wa mapromota.

  Mapromota wamefanya kile walichokusudia, wamevuma mamilioni ya pesa kutoka kwake kwa kumtumia kwenye maonyesho mengi kwa ujira mdogo.Leo hii maisha yake yamefika mahali ambapo anahitaji msaada lakini hakuna kati ya wale waliovuna pesa nyingi kutoka kwake anayemkumbuka.

  Inasikitikisha kwa sababu, heshima kubwa aliyokuwa akiipata anapanda jukwaani na kuimba, leo haipo tena. Hana hata godolo la kuweka mbavu zake.

  Taswira ya haraka inayopatikana kwa sasa ni sawa na kusema: "Zimwi likujualo halikuli likakumaliza."
  Sikutegemea msanii kama Bi Kidude aliyejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi leo hii angeishia kuomba msaada wa matibabu kwa watu wake wa karibu.

  Pamoja na kusafiri nchi nyingi kufanya maonyesho, ukweli ni kwamba hakuna alichonufaika nacho. Kama kungekuwa na alichonufaika nacho, basi leo hii asingeomba msaada wa matibabu.

  Maisha yake kwenye nyumba chakavu yanasikitisha, huku walimtumia kuvuna mamilioni ya pesa wakiishi kwenye majumba ya kifahari na maisha yao yamejaa furaha kupindukia.

  Ni aibu kwa watu waliokuwa karibu na msanii huyu leo hii wameshindwa kabisa kumpa msaada. Kubwa walikofanya wakati huo ni kumnunulia sigala na pombe na kumpa fedha kiduchu.

  Kidude anayekadiliwa kuwa na miaka 100, leo hii hakupaswa kuwa msanii wa kuombaomba. Alipaswa kukaa chini na kula matunda ya utumishi wake wa muda mrefu kwenye sanaa ya muziki.

  Katika umri kama wake na namna alivyojituma ndani ya sanaa ya burudani, wengi walitarajia angekuwa na mahali pazuri pa kuishi na hii ingemsadia hata kuepukana na magonjwa mabayo yanaweza kutokana na umaskini.

  Nimesikitishwa kuona mkongwe huyu bado akiendelea kusotea matibabu bila msaada kutoka kwa watu wake wa karibu, yaani wale walimtumia kujinufaisha.

  Shukrani kwa rafiki wa mbali kutoka nchini Japani, ambaye ameamua kujitolea na kumpeleka hospitalini kwa ajili ya matibabu.Tumeshindwa kuwa na utamaduni wa uzawa na kuwathamini wale walioshiriki kuvuja jasho kukuza sanaa yetu ya muziki.

  Tumekuwa watumwa wa kupenda vitu vikiwa katika hali nzuri na kuvisahau kabisa pale zinapofikia hatua ya kuhitaji msaada. Haya ndiyo yanayomkuta Kidude leo hii.Ninachokiona kwa bi Kidude ni fundisho kubwa kwa wasanii wengine kuamka na kupambana kupigania haki zao wakiwa bado wana nguvu badala ya kusubiri liwakute kama ilivyotokea bibi huyu.

  Nionavyo mimi ni wakati wa wasanii sasa kupigana kufa na kupona kuhakikisha wanapata haki zao katika utaratibu unaostahili.Waepuke kuingia mikataba ya 'kichwakichwa' waombe ushauri mapema ili kuepukana na watu wenye nia mbaya na kazi zao.

  Vicky Kimaro ni mwandishi wa gazeti la mwananchi anapatikana kwenye namba 0715 08305[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  http://www.mwananchi.co.tz/uchambuzi/-/26027-athari-za-unyonyaji-kwa-wasanii-zinavyomtesa-bi-kidude
   
Loading...