Athari za Ukosefu wa Ajira na pia Elimu Bora inaonekana. Waliokuwa wafanyakazi Vumbi tumewajua pia

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
Ni mida ambayo kwa sisi wengine ndo tunatoka kazini kulijenga Taifa la Tanzania linalojengwa na wenye Moyo na Kuliwa na wenye Choyo.

Ni muda huu huwa naangalia nini kimekuwa posted JF. Ni kweli kuna ukosefu wa Ajira kwa kiwango kikubwa sana. Vijana wengi wapo masaa yote JF wakianzisha hata thread za kipuuz kabisa ambazo miaka yetu ile usingekuta mtu anawaza hivyo.

Lakini lingine unagundua wengi walikuwa wafanyakazi VUMBI ni kweli walipaswa kupanguswa aina ya threads wanazoanzisha zinaleta kichefuchefu na tumbo la kuhara linaloambatana na maumivu makali sana ya kichwa.

Aina ya maneno wanayotumia ni ya kipuuzi sana ya kitoto na pia hata threads zenyewe ni zenye hoja za kitoto na mchekea kabisa. Hawa waliiiwa wameajiriwa NSSF,Wizara mbalmbali na Kampuni za Kitapeli ambazo kwa sasa zimekufa. Hizi zilianzishwa na mafisadi kama namna ya kuchota pesa za watanzania maskini sisi ambao tunazidi kulimbikiziwa kodi mpaka sasa.

Lakin pia utagungua hata elimu ya wengi ni ya mashaka makuu. Yenye utata kuanzia kwa viongozi mpaka vilongozi.

Ni post za Mataptap tu na msongo wa mawazo zinazokuwa posted. Watu wanakosoa,wanahoji na kushangaa vitu vidogo sana.
 
Sasa na wewe mbona umepost mada ya ajabu hivo huoni aibu kwa ulichokianzisha hapa kuwa ni zaidi ya utoto au umepiga kiroba, wewe unalaumu vijana wasio na ajira kisa eti ufisadi mbona haviendani
 
Kweli sana mkuu, leo jukwaa limevamiwa kwa hoja na vihoja vya kipuuzi mno
 
:( "kilicho mkuta Kibeku na Ungo pia kitamkuta" :mad:

Sasa na wewe mbona umepost mada ya ajabu hivo huoni aibu kwa ulichokianzisha hapa kuwa ni zaidi ya utoto au umepiga kiroba, wewe unalaumu vijana wasio na ajira kisa eti ufisadi mbona haviendani
 
Unawaita wenzako wafanyakazi vumbi, nawewe unaweza kuwa MwanaJF Vumbi No 1.
 
Back
Top Bottom