Athari za sasa na za baadae za viongozi wa BAKWATA kuchochea uhasama dhidi ya CHADEMA...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
7,288
Ni bayana kuwa katika kipindi cha takribani mwaka mmoja viongozi wa baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislamu, wamekuwa kwa namna tofauti, na wakati tofauti wakichochea chuki kwa waislamu dhidi ya CHADEMA.

Sio lengo la makala yangu kueleza chimbuko ama namna ambavyo viongozi hawa wamekuwa wakijenga uhasama huo kwani naamini wananchi wengi hayo wanayajua. Naomba nieleze kwa maoni yangu na kwa kuzingatia yale ninayoyaona athari za hatua hii inayochukuliwa na viongozi wa waislamu.

Naamini kama watu wenye akili timamu wanazo sababu zao za kujenga mazingira ya kuikosashe CHADEMA nafasi za kuongoza wananchi. Hilo sina tatizo nalo, ila wasiwasi wangu ni yatokanayo na hatua hizi walizochukua ndugu zetu. Sio sahihi kusema Tanzania hatujawahi kuwa na chembechembe za chuki za kidini, zimekuwepo lakini katika level ndogo isiyo na madhara makubwa (naamini kuna watu wenye maoni tofauti katika hili, nayaheshimu). Hata hivyo katika miaka ya karibuni, kwa kiasi kikubwa watanzania tulikuwa tunaaminiana licha ya kuwa na dini tofauti.

Ni jambo la kusikitisha kuwa chuki iliyojengwa na viongozi wa kiislamu dhidi ya CHADEMA imeanza, tena kwa kasi ya kutisha kurudisha chokochoko na chuki za kidini. Ingawa sio rahisi sana kuligundua hili, lakini siku hizi katika makundi ya watu, tayari kuna asilimia kubwa ambao wanaamini mtu anayeitwa Abdalah ni lazima atakuwa anashabikia chama fulani, na mtu anayeitwa Peter, anashabikia chama fulani. Kwa bahati mbaya zaidi kumekuwa na asilimia inayoongezeka kila kukicha ya watu ambao wanawa-treat watanzania wenzao kwa kuzingatia itikadi zao za kisiasa, ambazo 'wanazijua' kutokana na dini ya mtu. Miaka michache iliyopita ilikuwa ni nadra sana mtu kupewa au kunyimwa ajira, kwa sababu wa dini yake. Amini msiamini, kwa kipindi cha mwaka mmoja tu tangu viongozi wa waislamu walipoanza kuhubiri chuki dhidi ya CHADEMA, ubaguzi wa kidini umeshaanza kurudi tena kwa kasi ya ajabu.

Kwa mfano zipo taarifa za uhakika kuwa siku hizi kuna wahadhiri wa vyuo ambao mwanafunzi mwenye jina linaloashiria dini fulani hawezi kupata A kwenye somo lake. Mbaya zaidi wapo wengine wanadiriki kujitahidi kuwafelisha wanafunzi wanaodhaniwa kuwa wafuasi wazuri wa dini zao ama kwa mavazi wanayovaa, au matendo mengine. Wapo mabosi wengi ambao kama upo uwezekano, basi watajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa mtu mwenye jina linaloashiria dini fulani hatakuwa mfanyakazi wake. Mnaweza mkadhani kuwa naongeza chumvi katika hili lakini kama unaweza kusoma 'mioyo' ya watu, yapo maeneo mengine hata ile kusalimiana kwa 'moyo', kushirikiana kaitka mambo ya kijamii na kadhalika kumeshaathiriwa vibaya sana na itikadi za kisiasa, zinazotokana na udini. Ubaguzi umeshaanza kuota mizizi mahospitalini, mashuleni, wapo wanaoamini hata selection ya wanafunzi inaangalia dini, selection ya wanaokopeshwa kusoma vyuo vikuu inaangalia dini n.k, kisa kwa sababu dini yako ndiyo imefanya mbunge niliyemtaka asichaguliwe na mambo kama hayo.

Tunaweza tusikatane kwa mapanga kwa sasa, lakini athari za tatizo hili endapo likiendelea kufumbiwa macho na viongozi wetu wa dini na siasa, kama ilivyo sasa zitakuwa kubwa zaidi ya kukatana mapanga. Sitaki kuamini hivyo, lakini kama ni kweli kuna kundi moja la dini lililo na nafasi zaidi katika huduma za jamii, basi ni dhahiri kuwa kundi jingine lenye nafasi ndogo katika huduma za jamii litaumia. Kama walimu wakiamua kupendelea wanafunzi kwa imani zao, kama madaktari wakiamua kupendelea huduma kwa waumini wenzao, kama wahadhiri wakiamua kufaulisha au kufelisha wanafunzi kulingana na dini zao, kama waajiri wakiamua kuajiri watu waumini wenzao, mwisho wa siku viongozi wa dini au viongozi wa siasa hawataumia moja kwa moja, bali wananchi na waumini wa kawaida ndio watakaoumia.

Najua waislamu wamekuwa na madai kadhaa wanayotaka serikali iwatekelezee kama waislamu. Sioni namna yeyote ambayo madai hayo yatatekelezwa kwa kuwachukia CHADEMA, japo kwa maoni yangu. Siku zote nimekuwa nikiamini katika diplomasia na mazungumzo. Ni matumaini yangu kuwa ili mengi ya madai ya waislamu yaweze kutekelezwa, yatahitaji kuridhiwa katika vyombo vya maamuzi vya nchi hii, ambavyo bila shaka vinaundwa na watu wenye itikadi tofauti za kisiasa. Sioni sababu yeyote ya waislamu kukata tamaa ya kushawishi na kuamua kutumia mbinu ya kuwagawa watoa maamuzi kwa itikadi ya dini.

Nini kifanyike...
Naamini katika mazungumzo. Hakuna njia ya mkato zaidi ya viongozi wetu wa kiislamu kuamua kuacha kujenga chuki za kisiasa. Lakini pia nadhani viongozi wa CHADEMA wana jukumu la kufanya katika hili zaidi ya kupuuzia. Ni kweli kuwa CHADEMA kinaweza kutimiza malengo yake ya kuchaguliwa kuongoza nchi 'katikati' ya juhudi hizi za kuipaka matope lakini, kwa maoni yangu haitakuwa na maana hata kama wakiingia madarani. Viongozi wa CHADEMA wanatakiwa 'KUWAONYESHA' waislamu kwa maneno na vitendo kuwa sio chama chenye dhamira yeyote mbaya kwa maslahi halali ya waislamu. Simaanishi kuwa kwa sasa CHADEMA inaonyesha kinyume chake, bali nadhani kwa kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA ambao wapo njia panda kutokana na kupewa 'maagizo' au kushawishiwa na viongozi wao kuwa CHADEMA hakifai. Najua ni vigumu kuwaondoa watu katika imani zao ndiyo maana inabidi CHADEMA ikubali kubeba vyote, watu, itikadi zao za kisiasa na imani zao.

Upo umuhimu wa viongozi wa CHADEMA kuonyesha 'heshima' kwa viongozi wa waislamu, sio tu kuwarudhisha viongozi hao, bali pia kutoa ujumbe kwa wanachama na wafuasi wao kuwa CHADEMA kinatambua na kuheshimu imani zao. Viongozi wa CHADEMA wamekuwa 'kimya' au wamekuwa nao wakijibu katika vyombo vya habari baadhi ya shutuma na lawama za viongozi wa waislamu. Sio vibaya, lakini kwa namna fulani inajenga picha ya 'bifu' ambayo madhara yake ndiyo hayo watu kuchotwa kisiasa, kwa imani za dini zao.

Naomba niishie hapa, nikiamini kuwa katika mazingira ambayo tumeshaanza kujengewa, michango 'negative' dhidi ya maoni na mapendekezo ya makala hii yatakuwepo. yapo mengi ya kujadili na kuelezana ili Tanzania iweze kuwa mahali pa amani...
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Udini hauondolewe kwa unafiki na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa lazima kuwe na mjadala wa haki na wazi kitaifa kuhusu mambo hayo yaliyoanza si kwa chadema au CUF yalianza toka wakati wa nyerere..ni kwamba sasa hivi yameji-manifest..
 
danielwc

Member
Mar 9, 2007
12
3
Uchambuzi mzuri, mwenye akili ataelewa. gharama za chuki za namna hii ni kweli zipo. na ndugu zetu waislam wanapaswa kuwa makini na viongozi wanaotumia taasisi zao kwa manufaa ya chama flani. huwezi kuusemea moyo wa mtu na ni ukweli usiopingika kwamba hata wakristo wapo wengi tu waliokwazika kwa hayo matamshi na kwa kukaa kimya inaweza kumaanisha ni kinyongo au hata vinginevyo. nawaomba brothers and sisters toka jamii ya kiislam muwe mnajitokeza mapema kulaani na kupinga kauli zinazoweza kuleta mfarakano katika jamii yetu. au kama vipi mtumie vifungu vya katiba yenu muung'oe utawala wa BAKWATA uliopo now
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu ndio maana nikasema kuna haja ya kureview namna mambo haya yalivyoji-remanifest. Kujenga chuki dhidi ya chama fulani, sio tu haitamaliza tatizo, bali itakuwa kama unalichochea tatizo...
 
Ni sawa kabisa lakini pamoja na viongozi wa waislamu ambao sio rahisi kutafuta muafaka katika hili (inavyoonekana wananeemeka na mgogoro huu), lakini viongozi wa kisiasa kwa maana ya CHADEMA kama 'unnecessary victims' na CCM kama washika dola, wanatakiwa watumie busara zao kulinusuru taifa...
 
Yale yale ya chadema..unaanza na accusation halafu unataka kumaliza tatizo..inabidi stakeholders wote wajitazame wao ni source kwa kiwango gani?
 
Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
67
Umeandika sana kaka lakini chadema wamedhihirisha na kujinasibu kuwa ni chama kristo...hata ukiangalia nyadhifa za viongozi wake mf. kina mchungaj,maeneo ambayo chadema inakubalika na hata michango ya wana jf hapa..angalia matukio wakati wa uchaguz mkuu 2010,matamko mbalimbali ya viongoz wa makanisa yalidhihirisha hilo.waislam wanalalamika wana mashiko.ni vyema chadema warekebishe dosari hii.si nzuri.watabisha but ukweli unaonekana.niko tayari kukosolewa.
 
Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,740
742
Hivi viongozi wa kikristo ni wapi walisema au walichochea udini na ni nani huyu coz sijawahi kuona kama tulivyoona hata juzi tu Igunga, hebu twambieni ni nani huyu kwani naona hapa tunaendesha visa vya kitoto waislam hamuwezi pata haki zenu kwa kukipigia kampen ccm ila chama kinachotetea haki na maslahi ya wanyonge na Taifa na hii ndo iwe misingi ambayo tunatakiwa kupigania ila siasa za kusema fulani kusema hivi na mimi nasema hivi huu ni utoto hebu tubadilike. Nawasilisha nipo tayari kurekebishwa
 
danielwc

Member
Mar 9, 2007
12
3
chadema na kanisa!! does that mean ccm na miskiti!! thats so low, hii point ni nzuri na haiko biased kivile kwa mtu mwenye mtazamo chanya! infact mleta hoja ni kama yuko sympathetic zaidi kwa waislam kama majeraha ya uchaguzi wa igunga hayatatibiwa na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. wanaonufaika na hii gap ya udini ni watu wachache sana katika hizi taasisi za dini! ni kwa nn watanzania zaidi ya 40 mil tuisambaratishe amani yetu kwa manufaa ya viongozi wachache wa dini?
 
Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,271
531
Mdini namba moja na mchochezi wa jambo hilo ambaye naamini ndiye aliyewalisha viongozi wa BAKWATA sumu ni mkuu wa nchi pale alipotoa kauli tata wakati wa kampeni mwaka jana. Naamini alifanya hivyo kupata kura bila ya kujali madhara yake. Kiongozi wa nchi anapotoa matamko ya kisiasa bila kuyapima na chama chake kuyabeba kana kwamba ndiyo ukweli pasi uthibitisho na kueleza mkakati au hatua anazoweza kuchukua kwa wanaoeneza udini huo ili tu kujipatia kura za kundi fulani la jamii...naona huyo ndiye hatari zaidi ya yale yanayozungumzwa na BaKWATA. Namchukia kiongozi yeyote anayetumia munipulation ili kutimiza ajenda yae bia kujali madhara yake kwa jamii nzima na JK ameonyesha njia na chama chake na wengine wanafuata kwa sababu za either upendeleo au rushwa fulani wanazopewa na wenye hoka
 
segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Aliyetufikisha hapa tulipo nadhani anajulikana.Najua hata yeye nafsi yake huwa inamsuta anapokuwa amekaa peke yake na kufikiria mstakabali wa taifa hili ndio maana alipofanikisha lengo lake la kujipatia nafasi aliyokuwa akiitafta alisema ni wakati wa wandishi wa habari kutibu majeraha ya uchaguzi,udini ukiwa ni jeraha kubwa.Nawaomba ndg zetu waislam watambue kuwa bakwata inatumika kisiasa na ni chombo cha ccm kufanikisha mambo yake na kuwaacha solemba.Watawachonganisha na vyama vya siasa na siku ccm itakaposhindwa kwa ngazi za juu na chama kingine kutawala,hamtakuwa na amani kwa sababu mtajua ndio wakati wa adui yenu kutekeleza yale ambayo mlikuwa mnahisi atayatenda dhidi yenu
 
Apr 11, 2011
20
0
Ni kweli kabisa viongozi wa kikristo kama vile maaskofu walitoa matamko kipindi cha uchaguzi 2010, lakini watu walipaswa kujua yale matamko yalikuwa yanasisitiza kitu gani, sio vema kuanza kuangalia aliyetoa tamko ni nani bali tuangalie tamko lilihusu nini? matamko yale yalihusu mwongozo wa kuwapata viongozi bora sio vinginevyo! bahati mbaya watu wengi hawakuelewa kilichoongolewa na sasa wote (waislamu na wakristo) tunaona matokeo ya kuwa na viongozi wabovu! tunapaswa kuwa makini kwenye mambo ya msingi!
 
Maengo

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
280
29
Ni bayana kuwa katika kipindi cha takribani mwaka mmoja viongozi wa baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislamu, wamekuwa kwa namna tofauti, na wakati tofauti wakichochea chuki kwa waislamu dhidi ya CHADEMA.

Sio lengo la makala yangu kueleza chimbuko ama namna ambavyo viongozi hawa wamekuwa wakijenga uhasama huo kwani naamini wananchi wengi hayo wanayajua. Naomba nieleze kwa maoni yangu na kwa kuzingatia yale ninayoyaona athari za hatua hii inayochukuliwa na viongozi wa waislamu.

Naamini kama watu wenye akili timamu wanazo sababu zao za kujenga mazingira ya kuikosashe CHADEMA nafasi za kuongoza wananchi. Hilo sina tatizo nalo, ila wasiwasi wangu ni yatokanayo na hatua hizi walizochukua ndugu zetu. Sio sahihi kusema Tanzania hatujawahi kuwa na chembechembe za chuki za kidini, zimekuwepo lakini katika level ndogo isiyo na madhara makubwa (naamini kuna watu wenye maoni tofauti katika hili, nayaheshimu). Hata hivyo katika miaka ya karibuni, kwa kiasi kikubwa watanzania tulikuwa tunaaminiana licha ya kuwa na dini tofauti.

Ni jambo la kusikitisha kuwa chuki iliyojengwa na viongozi wa kiislamu dhidi ya CHADEMA imeanza, tena kwa kasi ya kutisha kurudisha chokochoko na chuki za kidini. Ingawa sio rahisi sana kuligundua hili, lakini siku hizi katika makundi ya watu, tayari kuna asilimia kubwa ambao wanaamini mtu anayeitwa Abdalah ni lazima atakuwa anashabikia chama fulani, na mtu anayeitwa Peter, anashabikia chama fulani. Kwa bahati mbaya zaidi kumekuwa na asilimia inayoongezeka kila kukicha ya watu ambao wanawa-treat watanzania wenzao kwa kuzingatia itikadi zao za kisiasa, ambazo 'wanazijua' kutokana na dini ya mtu. Miaka michache iliyopita ilikuwa ni nadra sana mtu kupewa au kunyimwa ajira, kwa sababu wa dini yake. Amini msiamini, kwa kipindi cha mwaka mmoja tu tangu viongozi wa waislamu walipoanza kuhubiri chuki dhidi ya CHADEMA, ubaguzi wa kidini umeshaanza kurudi tena kwa kasi ya ajabu.

Kwa mfano zipo taarifa za uhakika kuwa siku hizi kuna wahadhiri wa vyuo ambao mwanafunzi mwenye jina linaloashiria dini fulani hawezi kupata A kwenye somo lake. Mbaya zaidi wapo wengine wanadiriki kujitahidi kuwafelisha wanafunzi wanaodhaniwa kuwa wafuasi wazuri wa dini zao ama kwa mavazi wanayovaa, au matendo mengine. Wapo mabosi wengi ambao kama upo uwezekano, basi watajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa mtu mwenye jina linaloashiria dini fulani hatakuwa mfanyakazi wake. Mnaweza mkadhani kuwa naongeza chumvi katika hili lakini kama unaweza kusoma 'mioyo' ya watu, yapo maeneo mengine hata ile kusalimiana kwa 'moyo', kushirikiana kaitka mambo ya kijamii na kadhalika kumeshaathiriwa vibaya sana na itikadi za kisiasa, zinazotokana na udini. Ubaguzi umeshaanza kuota mizizi mahospitalini, mashuleni, wapo wanaoamini hata selection ya wanafunzi inaangalia dini, selection ya wanaokopeshwa kusoma vyuo vikuu inaangalia dini n.k, kisa kwa sababu dini yako ndiyo imefanya mbunge niliyemtaka asichaguliwe na mambo kama hayo.

Tunaweza tusikatane kwa mapanga kwa sasa, lakini athari za tatizo hili endapo likiendelea kufumbiwa macho na viongozi wetu wa dini na siasa, kama ilivyo sasa zitakuwa kubwa zaidi ya kukatana mapanga. Sitaki kuamini hivyo, lakini kama ni kweli kuna kundi moja la dini lililo na nafasi zaidi katika huduma za jamii, basi ni dhahiri kuwa kundi jingine lenye nafasi ndogo katika huduma za jamii litaumia. Kama walimu wakiamua kupendelea wanafunzi kwa imani zao, kama madaktari wakiamua kupendelea huduma kwa waumini wenzao, kama wahadhiri wakiamua kufaulisha au kufelisha wanafunzi kulingana na dini zao, kama waajiri wakiamua kuajiri watu waumini wenzao, mwisho wa siku viongozi wa dini au viongozi wa siasa hawataumia moja kwa moja, bali wananchi na waumini wa kawaida ndio watakaoumia.

Najua waislamu wamekuwa na madai kadhaa wanayotaka serikali iwatekelezee kama waislamu. Sioni namna yeyote ambayo madai hayo yatatekelezwa kwa kuwachukia CHADEMA, japo kwa maoni yangu. Siku zote nimekuwa nikiamini katika diplomasia na mazungumzo. Ni matumaini yangu kuwa ili mengi ya madai ya waislamu yaweze kutekelezwa, yatahitaji kuridhiwa katika vyombo vya maamuzi vya nchi hii, ambavyo bila shaka vinaundwa na watu wenye itikadi tofauti za kisiasa. Sioni sababu yeyote ya waislamu kukata tamaa ya kushawishi na kuamua kutumia mbinu ya kuwagawa watoa maamuzi kwa itikadi ya dini.

Nini kifanyike...
Naamini katika mazungumzo. Hakuna njia ya mkato zaidi ya viongozi wetu wa kiislamu kuamua kuacha kujenga chuki za kisiasa. Lakini pia nadhani viongozi wa CHADEMA wana jukumu la kufanya katika hili zaidi ya kupuuzia. Ni kweli kuwa CHADEMA kinaweza kutimiza malengo yake ya kuchaguliwa kuongoza nchi 'katikati' ya juhudi hizi za kuipaka matope lakini, kwa maoni yangu haitakuwa na maana hata kama wakiingia madarani. Viongozi wa CHADEMA wanatakiwa 'KUWAONYESHA' waislamu kwa maneno na vitendo kuwa sio chama chenye dhamira yeyote mbaya kwa maslahi halali ya waislamu. Simaanishi kuwa kwa sasa CHADEMA inaonyesha kinyume chake, bali nadhani kwa kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA ambao wapo njia panda kutokana na kupewa 'maagizo' au kushawishiwa na viongozi wao kuwa CHADEMA hakifai. Najua ni vigumu kuwaondoa watu katika imani zao ndiyo maana inabidi CHADEMA ikubali kubeba vyote, watu, itikadi zao za kisiasa na imani zao.

Upo umuhimu wa viongozi wa CHADEMA kuonyesha 'heshima' kwa viongozi wa waislamu, sio tu kuwarudhisha viongozi hao, bali pia kutoa ujumbe kwa wanachama na wafuasi wao kuwa CHADEMA kinatambua na kuheshimu imani zao. Viongozi wa CHADEMA wamekuwa 'kimya' au wamekuwa nao wakijibu katika vyombo vya habari baadhi ya shutuma na lawama za viongozi wa waislamu. Sio vibaya, lakini kwa namna fulani inajenga picha ya 'bifu' ambayo madhara yake ndiyo hayo watu kuchotwa kisiasa, kwa imani za dini zao.

Naomba niishie hapa, nikiamini kuwa katika mazingira ambayo tumeshaanza kujengewa, michango 'negative' dhidi ya maoni na mapendekezo ya makala hii yatakuwepo. yapo mengi ya kujadili na kuelezana ili Tanzania iweze kuwa mahali pa amani...

Naona unafanya jitihada kubwa kuuimarisha udini! Wewe unawezaje kusoma mioyo ya watu kama sio uongo ni nini? Tena unaongea kwa ujasiri na kuusimamia uongi wako, ila ni kwa nini unajihisi? Kwanini unahisi watu watakataa unachokisema, kwanini unawahi kujitetea? Bila shaka wew ni muislamu mwenzangu kwa sababu sisi hatujaanza leo kulalamika! Haya yote unayosema wenzangu wamekuwa wakiyalalamikia tangu zamani ila ukiangalia kwa makin unaona tatizo ni kwamba sisi tunashindwa kwenda na kasi ya wenzetu, ndo maana tunabaki kulalamika tu wakat wenzetu wanafanya mambo ya msingi wala hawana time na sisi! Suala la udini mimi siliamini kabisa ila ni kelele za mfamaji.....!
 
Halfcaste

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
972
214
Ni bayana kuwa katika kipindi cha takribani mwaka mmoja viongozi wa baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislamu, wamekuwa kwa namna tofauti, na wakati tofauti wakichochea chuki kwa waislamu dhidi ya CHADEMA.

Sio lengo la makala yangu kueleza chimbuko ama namna ambavyo viongozi hawa wamekuwa wakijenga uhasama huo kwani naamini wananchi wengi hayo wanayajua. Naomba nieleze kwa maoni yangu na kwa kuzingatia yale ninayoyaona athari za hatua hii inayochukuliwa na viongozi wa waislamu.

Naamini kama watu wenye akili timamu wanazo sababu zao za kujenga mazingira ya kuikosashe CHADEMA nafasi za kuongoza wananchi. Hilo sina tatizo nalo, ila wasiwasi wangu ni yatokanayo na hatua hizi walizochukua ndugu zetu. Sio sahihi kusema Tanzania hatujawahi kuwa na chembechembe za chuki za kidini, zimekuwepo lakini katika level ndogo isiyo na madhara makubwa (naamini kuna watu wenye maoni tofauti katika hili, nayaheshimu). Hata hivyo katika miaka ya karibuni, kwa kiasi kikubwa watanzania tulikuwa tunaaminiana licha ya kuwa na dini tofauti.

Ni jambo la kusikitisha kuwa chuki iliyojengwa na viongozi wa kiislamu dhidi ya CHADEMA imeanza, tena kwa kasi ya kutisha kurudisha chokochoko na chuki za kidini. Ingawa sio rahisi sana kuligundua hili, lakini siku hizi katika makundi ya watu, tayari kuna asilimia kubwa ambao wanaamini mtu anayeitwa Abdalah ni lazima atakuwa anashabikia chama fulani, na mtu anayeitwa Peter, anashabikia chama fulani. Kwa bahati mbaya zaidi kumekuwa na asilimia inayoongezeka kila kukicha ya watu ambao wanawa-treat watanzania wenzao kwa kuzingatia itikadi zao za kisiasa, ambazo 'wanazijua' kutokana na dini ya mtu. Miaka michache iliyopita ilikuwa ni nadra sana mtu kupewa au kunyimwa ajira, kwa sababu wa dini yake. Amini msiamini, kwa kipindi cha mwaka mmoja tu tangu viongozi wa waislamu walipoanza kuhubiri chuki dhidi ya CHADEMA, ubaguzi wa kidini umeshaanza kurudi tena kwa kasi ya ajabu.

Kwa mfano zipo taarifa za uhakika kuwa siku hizi kuna wahadhiri wa vyuo ambao mwanafunzi mwenye jina linaloashiria dini fulani hawezi kupata A kwenye somo lake. Mbaya zaidi wapo wengine wanadiriki kujitahidi kuwafelisha wanafunzi wanaodhaniwa kuwa wafuasi wazuri wa dini zao ama kwa mavazi wanayovaa, au matendo mengine. Wapo mabosi wengi ambao kama upo uwezekano, basi watajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa mtu mwenye jina linaloashiria dini fulani hatakuwa mfanyakazi wake. Mnaweza mkadhani kuwa naongeza chumvi katika hili lakini kama unaweza kusoma 'mioyo' ya watu, yapo maeneo mengine hata ile kusalimiana kwa 'moyo', kushirikiana kaitka mambo ya kijamii na kadhalika kumeshaathiriwa vibaya sana na itikadi za kisiasa, zinazotokana na udini. Ubaguzi umeshaanza kuota mizizi mahospitalini, mashuleni, wapo wanaoamini hata selection ya wanafunzi inaangalia dini, selection ya wanaokopeshwa kusoma vyuo vikuu inaangalia dini n.k, kisa kwa sababu dini yako ndiyo imefanya mbunge niliyemtaka asichaguliwe na mambo kama hayo.

Tunaweza tusikatane kwa mapanga kwa sasa, lakini athari za tatizo hili endapo likiendelea kufumbiwa macho na viongozi wetu wa dini na siasa, kama ilivyo sasa zitakuwa kubwa zaidi ya kukatana mapanga. Sitaki kuamini hivyo, lakini kama ni kweli kuna kundi moja la dini lililo na nafasi zaidi katika huduma za jamii, basi ni dhahiri kuwa kundi jingine lenye nafasi ndogo katika huduma za jamii litaumia. Kama walimu wakiamua kupendelea wanafunzi kwa imani zao, kama madaktari wakiamua kupendelea huduma kwa waumini wenzao, kama wahadhiri wakiamua kufaulisha au kufelisha wanafunzi kulingana na dini zao, kama waajiri wakiamua kuajiri watu waumini wenzao, mwisho wa siku viongozi wa dini au viongozi wa siasa hawataumia moja kwa moja, bali wananchi na waumini wa kawaida ndio watakaoumia.

Najua waislamu wamekuwa na madai kadhaa wanayotaka serikali iwatekelezee kama waislamu. Sioni namna yeyote ambayo madai hayo yatatekelezwa kwa kuwachukia CHADEMA, japo kwa maoni yangu. Siku zote nimekuwa nikiamini katika diplomasia na mazungumzo. Ni matumaini yangu kuwa ili mengi ya madai ya waislamu yaweze kutekelezwa, yatahitaji kuridhiwa katika vyombo vya maamuzi vya nchi hii, ambavyo bila shaka vinaundwa na watu wenye itikadi tofauti za kisiasa. Sioni sababu yeyote ya waislamu kukata tamaa ya kushawishi na kuamua kutumia mbinu ya kuwagawa watoa maamuzi kwa itikadi ya dini.

Nini kifanyike...
Naamini katika mazungumzo. Hakuna njia ya mkato zaidi ya viongozi wetu wa kiislamu kuamua kuacha kujenga chuki za kisiasa. Lakini pia nadhani viongozi wa CHADEMA wana jukumu la kufanya katika hili zaidi ya kupuuzia. Ni kweli kuwa CHADEMA kinaweza kutimiza malengo yake ya kuchaguliwa kuongoza nchi 'katikati' ya juhudi hizi za kuipaka matope lakini, kwa maoni yangu haitakuwa na maana hata kama wakiingia madarani. Viongozi wa CHADEMA wanatakiwa 'KUWAONYESHA' waislamu kwa maneno na vitendo kuwa sio chama chenye dhamira yeyote mbaya kwa maslahi halali ya waislamu. Simaanishi kuwa kwa sasa CHADEMA inaonyesha kinyume chake, bali nadhani kwa kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA ambao wapo njia panda kutokana na kupewa 'maagizo' au kushawishiwa na viongozi wao kuwa CHADEMA hakifai. Najua ni vigumu kuwaondoa watu katika imani zao ndiyo maana inabidi CHADEMA ikubali kubeba vyote, watu, itikadi zao za kisiasa na imani zao.

Upo umuhimu wa viongozi wa CHADEMA kuonyesha 'heshima' kwa viongozi wa waislamu, sio tu kuwarudhisha viongozi hao, bali pia kutoa ujumbe kwa wanachama na wafuasi wao kuwa CHADEMA kinatambua na kuheshimu imani zao. Viongozi wa CHADEMA wamekuwa 'kimya' au wamekuwa nao wakijibu katika vyombo vya habari baadhi ya shutuma na lawama za viongozi wa waislamu. Sio vibaya, lakini kwa namna fulani inajenga picha ya 'bifu' ambayo madhara yake ndiyo hayo watu kuchotwa kisiasa, kwa imani za dini zao.

Naomba niishie hapa, nikiamini kuwa katika mazingira ambayo tumeshaanza kujengewa, michango 'negative' dhidi ya maoni na mapendekezo ya makala hii yatakuwepo. yapo mengi ya kujadili na kuelezana ili Tanzania iweze kuwa mahali pa amani...
Well done JK u need a PHD on this.ili swala linaratibiwa na Jk pamoja na Iranian in diaspora Rostam ambaye kikiwaka hatakuwa Tanzania!!Mungu yu wapi,ona hawa viongozi wanavyotugawa,pliz wewe ni jibu!!
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Ni kweli kabisa ndugu yangu ndio maana nikasema kuna haja ya kureview namna mambo haya yalivyoji-remanifest. Kujenga chuki dhidi ya chama fulani, sio tu haitamaliza tatizo, bali itakuwa kama unalichochea tatizo...

At least we see some sense. Kwa muda mrefu sana mjadala wa humu ndani kuhusu udini ulikuwa biased. Lakini sasa tunapojadili au kukemea basi tuwe kama panga lenye makali kote kote maana ilivyo sasa, viongozi wa dini fulani waki-endorse chama fulani inaonekana ni sawa lakini wale wa dini nyingine wakifanya hivyo unaitwa udini. Selective memory au justice haitamaliza tatizo.
 
Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
255
Yale yale ya chadema..unaanza na accusation halafu unataka kumaliza tatizo..inabidi stakeholders wote wajitazame wao ni source kwa kiwango gani?
Wakati Mwenyekiti wa ccm alipokuwa mkristo, sisi woote tulikimbilia cuf kwa kuwa kinaongozwa na muislam mwenzetu. Alipokuja kushika uongozi muislam mwenzetu ccm, sisi wale wale tukaiua cuf kurudi ccm kwa muislam mwenzetu. Hiyo ndiyo siri ya kifo cha cuf mnayoiona huku bara. Sijui akija mwenyekiti mgalatia tena ccm, tutakimbilia wapi! Au tutaifufua UPDP ya Abubakar Olotu?
 
Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,316
Ni bayana kuwa katika kipindi cha takribani mwaka mmoja viongozi wa baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislamu, wamekuwa kwa namna tofauti, na wakati tofauti wakichochea chuki kwa waislamu dhidi ya CHADEMA.

Sio lengo la makala yangu kueleza chimbuko ama namna ambavyo viongozi hawa wamekuwa wakijenga uhasama huo kwani naamini wananchi wengi hayo wanayajua. Naomba nieleze kwa maoni yangu na kwa kuzingatia yale ninayoyaona athari za hatua hii inayochukuliwa na viongozi wa waislamu.

Naamini kama watu wenye akili timamu wanazo sababu zao za kujenga mazingira ya kuikosashe CHADEMA nafasi za kuongoza wananchi. Hilo sina tatizo nalo, ila wasiwasi wangu ni yatokanayo na hatua hizi walizochukua ndugu zetu. Sio sahihi kusema Tanzania hatujawahi kuwa na chembechembe za chuki za kidini, zimekuwepo lakini katika level ndogo isiyo na madhara makubwa (naamini kuna watu wenye maoni tofauti katika hili, nayaheshimu). Hata hivyo katika miaka ya karibuni, kwa kiasi kikubwa watanzania tulikuwa tunaaminiana licha ya kuwa na dini tofauti.

Ni jambo la kusikitisha kuwa chuki iliyojengwa na viongozi wa kiislamu dhidi ya CHADEMA imeanza, tena kwa kasi ya kutisha kurudisha chokochoko na chuki za kidini. Ingawa sio rahisi sana kuligundua hili, lakini siku hizi katika makundi ya watu, tayari kuna asilimia kubwa ambao wanaamini mtu anayeitwa Abdalah ni lazima atakuwa anashabikia chama fulani, na mtu anayeitwa Peter, anashabikia chama fulani. Kwa bahati mbaya zaidi kumekuwa na asilimia inayoongezeka kila kukicha ya watu ambao wanawa-treat watanzania wenzao kwa kuzingatia itikadi zao za kisiasa, ambazo 'wanazijua' kutokana na dini ya mtu. Miaka michache iliyopita ilikuwa ni nadra sana mtu kupewa au kunyimwa ajira, kwa sababu wa dini yake. Amini msiamini, kwa kipindi cha mwaka mmoja tu tangu viongozi wa waislamu walipoanza kuhubiri chuki dhidi ya CHADEMA, ubaguzi wa kidini umeshaanza kurudi tena kwa kasi ya ajabu.

Kwa mfano zipo taarifa za uhakika kuwa siku hizi kuna wahadhiri wa vyuo ambao mwanafunzi mwenye jina linaloashiria dini fulani hawezi kupata A kwenye somo lake. Mbaya zaidi wapo wengine wanadiriki kujitahidi kuwafelisha wanafunzi wanaodhaniwa kuwa wafuasi wazuri wa dini zao ama kwa mavazi wanayovaa, au matendo mengine. Wapo mabosi wengi ambao kama upo uwezekano, basi watajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa mtu mwenye jina linaloashiria dini fulani hatakuwa mfanyakazi wake. Mnaweza mkadhani kuwa naongeza chumvi katika hili lakini kama unaweza kusoma 'mioyo' ya watu, yapo maeneo mengine hata ile kusalimiana kwa 'moyo', kushirikiana kaitka mambo ya kijamii na kadhalika kumeshaathiriwa vibaya sana na itikadi za kisiasa, zinazotokana na udini. Ubaguzi umeshaanza kuota mizizi mahospitalini, mashuleni, wapo wanaoamini hata selection ya wanafunzi inaangalia dini, selection ya wanaokopeshwa kusoma vyuo vikuu inaangalia dini n.k, kisa kwa sababu dini yako ndiyo imefanya mbunge niliyemtaka asichaguliwe na mambo kama hayo.

Tunaweza tusikatane kwa mapanga kwa sasa, lakini athari za tatizo hili endapo likiendelea kufumbiwa macho na viongozi wetu wa dini na siasa, kama ilivyo sasa zitakuwa kubwa zaidi ya kukatana mapanga. Sitaki kuamini hivyo, lakini kama ni kweli kuna kundi moja la dini lililo na nafasi zaidi katika huduma za jamii, basi ni dhahiri kuwa kundi jingine lenye nafasi ndogo katika huduma za jamii litaumia. Kama walimu wakiamua kupendelea wanafunzi kwa imani zao, kama madaktari wakiamua kupendelea huduma kwa waumini wenzao, kama wahadhiri wakiamua kufaulisha au kufelisha wanafunzi kulingana na dini zao, kama waajiri wakiamua kuajiri watu waumini wenzao, mwisho wa siku viongozi wa dini au viongozi wa siasa hawataumia moja kwa moja, bali wananchi na waumini wa kawaida ndio watakaoumia.

Najua waislamu wamekuwa na madai kadhaa wanayotaka serikali iwatekelezee kama waislamu. Sioni namna yeyote ambayo madai hayo yatatekelezwa kwa kuwachukia CHADEMA, japo kwa maoni yangu. Siku zote nimekuwa nikiamini katika diplomasia na mazungumzo. Ni matumaini yangu kuwa ili mengi ya madai ya waislamu yaweze kutekelezwa, yatahitaji kuridhiwa katika vyombo vya maamuzi vya nchi hii, ambavyo bila shaka vinaundwa na watu wenye itikadi tofauti za kisiasa. Sioni sababu yeyote ya waislamu kukata tamaa ya kushawishi na kuamua kutumia mbinu ya kuwagawa watoa maamuzi kwa itikadi ya dini.

Nini kifanyike...
Naamini katika mazungumzo. Hakuna njia ya mkato zaidi ya viongozi wetu wa kiislamu kuamua kuacha kujenga chuki za kisiasa. Lakini pia nadhani viongozi wa CHADEMA wana jukumu la kufanya katika hili zaidi ya kupuuzia. Ni kweli kuwa CHADEMA kinaweza kutimiza malengo yake ya kuchaguliwa kuongoza nchi 'katikati' ya juhudi hizi za kuipaka matope lakini, kwa maoni yangu haitakuwa na maana hata kama wakiingia madarani. Viongozi wa CHADEMA wanatakiwa 'KUWAONYESHA' waislamu kwa maneno na vitendo kuwa sio chama chenye dhamira yeyote mbaya kwa maslahi halali ya waislamu. Simaanishi kuwa kwa sasa CHADEMA inaonyesha kinyume chake, bali nadhani kwa kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA ambao wapo njia panda kutokana na kupewa 'maagizo' au kushawishiwa na viongozi wao kuwa CHADEMA hakifai. Najua ni vigumu kuwaondoa watu katika imani zao ndiyo maana inabidi CHADEMA ikubali kubeba vyote, watu, itikadi zao za kisiasa na imani zao.

Upo umuhimu wa viongozi wa CHADEMA kuonyesha 'heshima' kwa viongozi wa waislamu, sio tu kuwarudhisha viongozi hao, bali pia kutoa ujumbe kwa wanachama na wafuasi wao kuwa CHADEMA kinatambua na kuheshimu imani zao. Viongozi wa CHADEMA wamekuwa 'kimya' au wamekuwa nao wakijibu katika vyombo vya habari baadhi ya shutuma na lawama za viongozi wa waislamu. Sio vibaya, lakini kwa namna fulani inajenga picha ya 'bifu' ambayo madhara yake ndiyo hayo watu kuchotwa kisiasa, kwa imani za dini zao.

Naomba niishie hapa, nikiamini kuwa katika mazingira ambayo tumeshaanza kujengewa, michango 'negative' dhidi ya maoni na mapendekezo ya makala hii yatakuwepo. yapo mengi ya kujadili na kuelezana ili Tanzania iweze kuwa mahali pa amani...

Vipi lile la Askofu Laizer wa kule Arusha na Meya? hili halina athari? au ndo yale kunya anye kuku, akinya bata uharo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom