Athari za kutotumia walimu katika senza zaanza kuonekana kabla ya sensa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athari za kutotumia walimu katika senza zaanza kuonekana kabla ya sensa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inkoskaz, Aug 22, 2012.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Kwa miaka mingi zoezi hili la sensa ya watu na makazi limekuwa likifanywa na walimu hapa nchini,kwa uzoefu wao wa kufundisha,kutunga na kusahihisha mitihani imekuwa ni rahisi kwao na pia udhibiti wao ni rahisi kwani wanafahamika vema na vituo vyao vya kazi vinafahamika
  Mzozo uliokuwapo baina ya serikali na walimu uliopelekea walimu kugoma ulisababisha serikali bila kufikiri athari za mbeleni kutangaza zoezi hilo halitakuwa la walimu pekee na hivyo kushirikisha wadau wengine mbalimbali
  Matokeo yako yanaanza kuonekana kuwa kumbe wengi walikuwa ni vijana wa vijiweni ambao wengi nia yao ni kuvuta mshiko na wala hawana wito wa kufanya hilo zoezi...wengine wakiwa ni wale ambao hata ile ZANA kuu ya sensa yaani kalamu na karatasi ni vitu walishavisahau hata sura yake ipo vipi
  bora Zimwi likujualo halikuli likakwisha...haya tena
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  WE acha tuone mchezo utakavonoga,ila kwa kuwa tu taifa la bora liende wala hakuna atakayeshtuka,lakini ukweliu ni kwamba hili zoezi tumeshapoteza pesa bure kabisa!watu hawaju kusoma wala kuandika lakini wamekuwa makarani,serikali inajitetea imewapa magraduates lakini si kweli wahitimu wa vyuo ni wachache sana kulinganisha na hao waliowaweka,hivi kweli hakuna yunaloweza kulifanya kwa usahihi hata kama kweli tunaitwa ni dhaifu,kweli tunashindwa kujipanga kiasi hiki?
   
 3. C

  CHOMA Senior Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maamuzi yaliyofanywa na Serikali ni ya kukurupuka.Ni vema sasa watajifunza matokeo yake kwani kitendo cha Walimu kugoma kwa ajili ya kudai haki zao kimeonekana kuwakera sana Serikali.Hata wajitetee vipi ilikuwa hakuna maana kubadili Mihula ya Shule kwa mwaka huu kama walikua na nia ya kuhusisha watu mchanganyiko kwenye zoezi hilo.Mheshimiwa Waziri Mkuu alikana hilo Mjengoni bila ya kuwa na takwimu zozote zile.Hembu atumie vyombo vyake vya Dola ili atuletee takwimu za idadi ya Walimu walioshiriki ili tuamini kuwa ni Walimu wachache tu wasioshiriki sensa ndio tumwamini aliyozungumza Mjengoni.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ipo siku walimu watathaminiwa tu
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Watu wamepandikizwa wakachukue posho....eti mtu anakuona baba mwenye nyumba lakini bado anakuhoji kama wewe ni mwanamke ama mwanamme....
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Kama tulishakuwa na wanafunzi waliofaulu kujiunga na sekondari huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika hatutashangaa kuwa na makarani wa sensa wasiojua kuandika
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Yeah sure...one day Yes...kama muasis wa taifa alivyouenzi ualimu hadi kuitwa Mwalimu JKN
   
 8. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,785
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  viongozi waliona ni nafasi ya kuwaingiza vijana wao
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Tena kuna watu wameambiwa watashikishwa buku 20 kwa siku 15 unamuachia aliyekuunganisha tempo
   
Loading...