Athari za Kupandisha Bei ya Umeme: Logic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athari za Kupandisha Bei ya Umeme: Logic

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Jan 4, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Umeme ni independent function.

  Ukipandisha bei ya umeme kama serikali yetu ya kifisadi ilivyofanya yafuatayo hayaepukiki:

  Wenye vituo vya mafuta wanatoa huduma kwa kutumia vifaa kwa umeme ambao wanaulipia, iwe kwa luku au kwa analog meter. Hawa wamiliki wa vituo vya mafuta wakipandishiwa bei ya umeme wa kuendeshea pampu zao, automatically watapandisha bei ya nishati ya mafuta. Wenye magari yao wakipandishiwa mafuta tutarajie kuwa wale wenye daladala watapandisha nauli na wale wenye magari binafsi watakuwa na hasira...watatunyima lifti sisi waenda kwa miguu (yaani nitoke kuchomolewa 50000 asubuhi-asubuhi halafu atokee mwenda kwa miguu ananiomba lifti? nampotezea tu).

  Hiyo ni mifano michache tu.

  Watanzania tusidanganyike. Nishati ya umeme si ya kuzungushana kama biashara ya kahawa na kashata. Leo hii watu wa vijijini wanaweza kujifariji kuwa wao hawaathiriki na kupanda huku kwa bei ya umeme kwa kisingizio kwamba wao hawautumii. Lakini fikiria viwanda vinavyotengeneza mbolea, chumvi, sukari, unga, majani-chai....vyote hivi vinategemea umeme. kupanda kwa bei ya umeme maana yake bidhaa hizi nazo zitapanda bei vilevile.

  Ni maumivu ya nchi nzima.

  Nawasilisha.
   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,989
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Hii kaka wenyewe wanaiitaga "exponentiation effect".

  Inakula kwa kila mtu, kutoka kila angle na kila wakati!!
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nchi ya amani
   
 4. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana, yaani Kiongozi mzima wa nchi ana support na kuona kuwa hakutakuwa na mfumuko wa bei!! unajiuliza mpaka unachoka!!! ata control vipi mfumuko wa bei za bidhaa nyingine baada ya kupandisha umeme??
   
 5. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bidhaa zote zinazotengenezewa hapa tanzania zitapanda bei automatically. Hii ni fursa nzuri kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi, hivyo kupelekea thamani ya sarafu ya tanzania kuzidi kuporomoka.
   
 6. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Cha moto tutakiona mwaka huu,haina cha itikadikila mmoja ataufeel huu moto....tulipokuwa tunawaamsha wanaCCM walidhani mambo kaka haya yatatugharimu tusiokuwa wanaCCM tu...,
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Tatizo viongozi wetu wanaona mwisho wa pua zao kwa hiyo ni vigumu kutafakari outcome ya ongezeko la bili ya umeme bila kuzingatia ni sehemu ngapi zinategemea nishati hiyo kujiendesha.
   
 8. njiwamanga

  njiwamanga Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni fursa nyingine ya kuing'oa ccm,nadhani hapo tutaona akili za wanaccm kama ni "matabulalasa" au la
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kila bidhaa itumiayo umeme kuzalishwa itapanda bei wakati mshahara upo pale pale.
  Kifuatacho ni kuwa ela yetu itakuwa haina dhamnai na kutakuwa na high cost of living na bila shaka standard of living itashuka as maisha yatazidi kuwa magumu daily.
  Kwa mafisadi ni shega tuu bse wanamijihera
   
 10. e

  ejogo JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani wamesubiri wameingia Ikulu ndipo wamepandisha bei!! Waliogopa kupandisha kabla ya uchaguzi. Yaani hata kabla ya kupandishwa bei maisha yalishakuwa tough, sasa sijui hawa jamaa wanataka tufe! Sasa tukifa watamtawala nani!!! Eti mfumuko wa bei umeshuka!! My pants!!!
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  lakini waziri ngeleja alikaririwa hivi karibuni akiwananga wanaolalama (alidai kisiasa) kwamba kupanda kwa umeme kutafanya maisha kuwa magumu pale aliposema "umeme haujapanda kiasi cha mtu kushindwa kabisa kulipia".

  ivi hawa mawaziri wetu walisoma wapi? yaani waziri mzima anaangalia umeme kama umeme badala ya kuangalia sector mbalimbali zinazotegemea umeme?

  waziri muadilifu na mchapakazi.

  5 years more? kikwete! really?
   
Loading...