Athari za kufungiwa ndani vs athari za ugonjwa wa Corona

Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,356
1,799
Wanajukwaa
Poleni na mihangaiko na taharuki inayotukumba kama Taifa.

Kuna mijadala mingi na mirefu humu inayohusu namna serikali inavyochukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa korona .
Wengi wakionekana kutoridhishwa na wengine wakiunga mkono hatua hizo, kuna baadhi wametaka viongozi kuwajibika kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Nimeleta kwenu hoja hii kwa dhumuni la kuisaidia serikali mawazo ya namna ya kukabiliana na janga hili kwani hali inazidi kuwa mbaya mno na watu wanaanza kukimbilia vijijini ambako kuna wazee wengi, na ugonjwa unaenea nchi nzima.

Ingekuwa vyema tuache mihemko na siasa tutangulize Taifa letu mbele
Najua uchaguzi wowote kati ya hayo mawili una madhara na utatugharimu lakini ni lazima tuchague

Unadhani ni sahihi kuacha watu waende vijijini au kufunga mikoa na wilaya kwa muda na kushughulika na tatizo hili
Tatizo hili likisambaa mikoa na wilaya zote nchini, serikali itaweza kumudu kupambana nalo?

Nchi hii ni yetu sote, tusichoke kushauriana, kuelimishana, kukosoana na kuelezana ukweli na ikibidi kuwajibishana kwa maslahi ya Taifa zima.







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue ya lockdown haipo tena, tumeshachelewa! Tuendelee kumuomba Mungu tu! Imeshafika mikoa kadhaa kwa mujibu wa reported cases!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom