Athari za Kuagiza nyama ya kuku toka Brazil na Marekani

NDANGA

Member
May 19, 2014
53
27
Wadau wa Ufugaji kuku

Bado jinamizi la Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kutaka kuruhusu kuagiza nyama ya kuku toka Brazil na Marekani lipo , nashauri kila mmoja wetu atumie wabunge anaowafahamu kulizuia japo kuwa tayari wameshasoma bajeti ya Wizara ya Mifugo.

Athari za kuingiza Kuku kutoka nje ni kama ifuatavyo,

1. Wafugaji wataacha ufugaji Kama ilivyotokea Zanzibar. Kuna ajira Zitapotea Hapo.

2. Wazalishaji Chakula cha mifugo watasimama uzalishaji . Kuna ajira Zitapotea

3. Wakulima wa Mahindi Na virutubisho vyote vinavyotumika katika kutengeneza Vyakula Watakosa soko.( Ingawa Hakuna Takwimu Sahihi Asilimia zaidi ya hamsini ya mahindi yanatumika katika mifugo)

4. Watotoleshaji vifaranga Watakosa soko La vifaranga. Hatchery zitafungwa na ajira kupotea.

5. Wenye Mikopo wote Katika sekta hii watashindwa kulipa hivyo kuzikwamisha Benki.

6. Wabeba mizigo watakosa kazi yao ya kushusha na kupakia mizigo.

7. Mama Lishe wote wanaotegemea washusha mizigo kama wateja kipato chao kitapungua.
8. WABEBA MIZIGO WENGINE WATATUMIA NGUVU ZAO KUKABA NA KUIBA.
9. Na serikali itakosa kodi.
 
wanaweza ruhusu,kwa aina ya viongoz tulio nao hakuna kinachoshindikana,kuna mahala kwengine kwenye migahawa inayouza pork ribs ukiagiza ile kitu inaitwa mbavu za kit moto,watoto wa mama mdogo tusamehene kidogo,ukiona c nene bal nyembamba mara nyingi uwa n ribs za brazil.Hapa bongo n kama mnadani kila mwenye bidhaa yake ata kama ndan ina uwezo wa kuzalishwa we lete tu.Ten percent wanazopokea viongoz wetu ndio zinayosabisha haya yote.
 
Lakini hata hivyo tunatakiwa tuwapinge sana kwamaana wanajinufaisha wenyewe na sisi wazawa tunazidi kuumia
 
Mkuu sisi hatuna serkali. tuna majambazi fulani wanatutawala kwa mabavu. Mimi ni mfugaji wa kuku wa mayai. ili niweze kuendelea lazima niuze tray angalau 6000. lakini kuna mayai ya nje yanauzwa 4500 halafu eti kuna waziri wa kilimo. Kichwa kimejaa uchafu wa makalioni. ovyoooo.
 
Wanyama wote hao wa porini bado mnaagiza nyama nje ? Kwani Kinara akishachukua meno nyama inakwenda wapi ?
 
Wakuu hii nchi yetu inatakiwa kila mtu ajue kinachoendelea bila hivyo watu wataumia sana!
 
hii nilikuwa sijui kabisa. Binafsi siungi mkono kama lipo.
Kila kijana mwenzangu ninaekutana nae akifikilia ujasiliamali ufugaji wa kuku umekuwa ukitajwa sana.
Vipi bado vibua tunatoa nje.
 
hii nilikuwa sijui kabisa. Binafsi siungi mkono kama lipo.
Kila kijana mwenzangu ninaekutana nae akifikilia ujasiliamali ufugaji wa kuku umekuwa ukitajwa sana.
Vipi bado vibua tunatoa nje.

Hili suala lipo baadhi ya wadau wa miradi kama hii tumejaribu kukaa na Serikali katika Wizara husika lakini bado kuna tetesi kuwa wanataka kuingiza mzigo nchini.
 
Kuishi Tanzania inataka moyo

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Kuku wa Brazil, wamejaa Zanzibar .....Kilo 2000/=

Sijui wana ubora au ndio yale yale
 
Kaka hawanaubora wowote ni ili mradi tu nao wanfanya hiyo biashara.
 
Back
Top Bottom