Athari za kiafya na kisaikolojia mara tu baada ya kujifungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athari za kiafya na kisaikolojia mara tu baada ya kujifungua

Discussion in 'JF Doctor' started by ZionTZ, Jun 6, 2012.

 1. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  [​IMG]Mara baada ya kujifungua mama anaanza ukurasa mpya wa maisha ya malezi. Anaanza wajibu mpya wa kulea, akili yake na mwili wake unakuwa tayari umejijenga kulea mtoto.
  Mama ana kazi ya kumuangalia mtoto kwa karibu ikiwapo kumnyonyesha. Hapa pamoja na mama kuwa na uangalizi wa karibu kwa mtoto naye pia anatakiwa aangaliwe kwa karibu, apewe matunzo mazuri na baba wa mtoto au ndugu wa karibu, afarijiwe na aangaliwe afya yake mara kwa mara. Matatizo ya kiafya ni kama vile magonjwa mfano malaria, kifua na maumivu ya mwili, maambukizi ukeni, kidonda kama alizaa kwa upasuaji, maambukizi kwa njia ya mkojo, kutokwa na damu kwa muda mrefu na maumivu ya tumbo, kupata shinikizo la damu na kifafa cha mimba baada ya kujifungua.
  Shinikizo la damu mara nyingi huanza taratibu na mama anaweza kuwa kwenye dozi ya matatizo haya ya presha ama asiwe nayo. Presha kuwa juu mara nyingi huanzia mimba ikiwa na umri wa majuma 20 na kuendelea. Kitaalamu kama hakukuwa na tatizo hili tangu awali, tunaita “Pregnancy Induced Hypertension” au “PIH”.
  Athari za kisaikolojia baada ya kujifungua hupelekea mama akapata matatizo ya kimwili kipindi hicho cha majuma sita mara tu baada ya kujifungua. Kipindi hiki tunakiita “Puerperium period”. Hapa mama anaweza kuchanganyikiwa “Pueperal pyschosis”, akapata homa kali “Pueperal Pyrexia” na maambukizi ukeni “Pueperal Sepsis”, kwa hiyo kama ilivyo kwa mama anavyomuangalia mtoto, ndivyo anavyotakiwa aangaliwe na atuzwe.
  Chakula bora na cha kutosha kwa mama kutamsaidia apate nguvu, atoe maziwa ya kutosha na arudishe afya yake na pia mwili unapata kinga dhidi ya maradhi mbalimbali.

  Imeandaliwa na Dkt. Chale


  source:Athari za kiafya na kisaikolojia mara tu baada ya kujifungua
   
 2. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Ahsante kwa somo.
   
Loading...