SoC01 Athari za hospitali kujengwa kwenye maeneo tunayoishi

Stories of Change - 2021 Competition

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Saalamu wanaJF,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika

Zahanati hapa Tanzania nyingi zimekuwa zikijengwa sehemu ambazo ni karibu tunapoishi . Hii ni nzuri kwa sababu ya ‘easy access’ pale mtu anapopatwa na tatizo la kiafya linalohitaji uangalizi wa haraka hiyyo anaweza kupata msaada huo kwa haraka na kupona.

Na pia zahanati zimekua ‘useful’ kwa nchi yetu yenye uhaba wa rasilimali za afya’ low medical resources’; kwa mfano zahanati zinapunguza uhitaji wa magari ya wagonjwa (ambulances), zinapunguza pia uhitaji wa kwenda hospitali kubwa,hivyo kupunguza msongamano katika hospital hizo, hii inapisha njia kwa wenye uhitaji wa uangalizi wa hospitali kubwa kupewa uangalizi huo wanaouhitaji (specialised care), Pamoja na kwamba zahanati zina ‘tusevu’ sana hasa sisi watu wa kipato cha kawaida, lakini uwepo wao karibu na makazi kuna athari kwa binadamu, kwa mfano kuwa hatarini ‘exposure’ kwa makelele, uchafu wa kibailojia (biological waste),u chafu wa kikemikali (chemical waste) na takataka za mionzi (radioactive waste).

Leo ningependa tuzungumzie athari za kuwa na zahanati karibu na tunapoishi, hususani athari za takataka za hospitali (hospital waste) katika mazingira yetu. Nimechagua topic hii sababu hali ama ‘status’ ya udhibiti wa uchafu unaotoka hospitalini kwa nchi yetu umepewa daraja la ‘Poor’ na shirika la Afya duniani (WHO). Hii inamaansha uchafu kutoka hospitalini haudhibitiwi ipasavyo, hivyo kuhatarisha afya zetu, Zaidi ya hio zahanati/dispensaries zinajengwa kila leo karibu na makazi watu wanayoishi ambayo kwa tafsiri nyingine ni watu wengi Zaidi wamo hatarini kupata athari za uchafu kutoka mahospitalini (exposure).

Uchafu huu una athari nyingi kwa mfano Magonjwa mengi ya kansa na moyo ni matokeo ya kemikali kukusanyika ndani ya mwili kwa muda mrefu ambazo zinasababishwa na watu kuwa ‘exposed’ na hewa chafu . Magonjwa haya ni gharama kwa mtu na serikali kutoa humuma za kiafya kwa waganjwa hawa(Medical care costs). Hivyo unaweza kuona hata mambo ya uchumi yangeweza kuwa ‘managed’ kama uchafu hospitalini ungedhibitiwa!

Takataka zitokazo hospitalini zipo za aina nyingi, kuna taka za patholojia/pathological waste ambao ni uchafu unaotokana na tishu za mwili, viungo vya ndani(organs) etc, pia kuna vitu vyenye ncha kali ambavyo vimeambukizwa ‘contaminated’, na virusi ama bakteria, na pia kundi lingine ni sumu za madawa ya hospitali.

Aidha, Ningependa kuainisha katika taka taka zote zinazotolewa na hospitali ni 15% tu ya takataka ndizo ziko‘classified’ kuwa ni za hatari .Kundi huli linajumuisha uchafu wa kipatholojia ‘pathological waste,vitu vyenye ncha kali ’ nakadhalika. japokua nI kundi dogo athari za hili kundi ni kubwa kwa mfano, 0.3% ya visabishi vya Ukimwi duniani kunasabishwa na vitu vyenche ncha kali mfano sindano!

Njia za kutupa uchafu Tanzania kama ilivyo nchi za kimaskini, takataka za hospitali zinatupwa kwenye mashimo ya taka za kawaida,(30%), kuchomwa moto (50%) na wengi zaidi (60%) kuchoma moto takataka kwenye matanuru spesho yanayojulikana kama’ incinerators’.

Kwa kuwa asilimia kubwa Zaidi ya uchafu wa hospitali ni unachomwa kupitia haya matanuru maalumu, inabidi tuangalie ama tuchunguze zaidi hatari zake kiafya na kimazingira.

Tafiti zinaonyesha kwa mfano kwa wilaya ya kinondoni pekee 70% ya haya matanuru yana kiwango duni kwa matumizi, kwa mfano mengi yamekutwa hayana mfuniko kwenye mlango wa kuingiza uchafu na pia hayana mifuniko katika sehemu ya kutoa majivu ya takataka zilizochomwa, hii inaleta athari hasa kwa mazingira ya karibu yanakua hatarini Zaidi kupata hewa chafu kutoka kwa haya matanuru yasiyokua na mifuniko.

Tafiti pia zinaonyesha takataka zinazokua zinachonwa na tanuru zinatakiwa zichomwe kwa joto kubwa (high temperature),na tanuru liwe na chemba mbili.(double chamber incinerator) Ila tafiti zinaonyesha hospitali nyingi Zaidi nchini zinatumia tanuru zenye uwezo mdogo na zenye chemba moja(single chamber) ambazo sio tu kwamba ni ndogo hazimudu kiasi kikubwa cha uchafu kinachotolewa na hospitalia bali pia zinatumia joto dogo kuchoma uchafu. Kuchoma uchafu katika joto dogo athari zake ni kubwa kwa mfano baadhi ya plastiki zikichomwa kwenye joto dogo zinachafua hewa kwa kutoa vichafua hewa kama ‘dioxins’ na ‘furans’ ambazo kiafya husababisha kansa na matatizo ya homoni

Moja ya mambo ambayo yamekuwa yajirudia rudia katika topic hii(theme), ambazo nimeona ni ishu’ ni ukosefufu wa miongozo ya serikali/guidelines na uchunguzi wa serikali kwa hospitali kama zinafuata hiio miongozo inayowekwa na serikali. Tunalipa gharama kubwa kuponyesha magonjwa yatokanayo na uchafu wa hospitali, serikali ingeweza kabisa ku’sevu’ gharama kwa kulipa umuhimu swala la udhibiti wa uchafu unaotoka hospitali.

Kingine ni ufahamu duni wa wafanyakazi wa hospital ‘staff awareness’ juu ya njia sahihi ya udhibiti wa uchafu kama kugawanya uchafu ullio hatari na usio hatari, njia sahihi za kuhifadhi na kusafirisha uchafu Pamoja na hasara za kuacha uchafu kwa muda mrefu kabla ya kutupa.

Nini kifanyike?

  • Kwa kuwa njia ya kuchoma uchafu kwenye matanuru ndio imekua kawaida ama desturi hivyo nguvu na rasilimali zielekezwe Zaidi kwenye hili eneo kushinda njia nyingine za kudhbiti uchafu, serikali ihakikishe hayo matanuru ni salama kwa matumizi, kwa mfano hayo matanuru yawe na mifuniko, pia kama inawezekana yawe na mifumo ya kudhibiti uchafu hewani (emission control systems/air pollution control devices). Pia ikiwezekana kuwe na sheria kote nchini matanuru yenye chemba mbili kudhibiti uchafu mwingi unaotolewa na hospitali na pia ziwe na uwezo wa kuchoma takataka katika joto kubwa ili kuchoma takataka kabisa
  • Serikali pia ifanye ku Monita kiwango cha uchafu kinachotolewa mahospitalini ambayo inaweza kuitaarifu serikali kiwango sahii na athari za uchafu huu kwa mazingira.(impact)
  • Serikali iweke miongozo sahihi ya kudhibiti uchafu na iweke njia za kuchunguza miogozo hii kama inafuatwa na hospitali nchini. Faini zilitolewe kwa kutofuata miongozo.
  • Kuwe na mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi wote wa hospitali juu ya kubeba na kutupa uchafu kwa njia sahihi.
  • Kuwe na miongozo ya serikali kuhusu hospitali kujengwa katika umbali Fulani kutoka makazi ya watu.

******Kuna mambo mengi ya kuongea kuhusu topic hii kwa mfano athari kwa mazingira;;maji,udongo,hewa n.k ila kwa kuanzia nimeona ni vyema tuanze na ya uchafu hospitalini na matanuru ya kuchomea ya taka hizo sababu nimeona ni eneo linalohitaji ‘attention’ yetu.

Karibuni kwa michango Zaidi…….
 
Back
Top Bottom