Athari ya muungano kuwa hoja ya viongozi

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,007
Hoja hii iliondoka kutokana na kuanzishwa wakati JF ikiwa katika marekebisho:
sammosses said:
Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi kuwa Tanzania ni nchi moja na Jamhuri ya Muungano ambayo ni sheria ya 1984 Na.15 ibara ya 6 ambayo nayo ina sema "Katika sehemu hii, isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo,neno "serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya serikali yoyote.

Ukiendelea kusoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utaona tena kwamba,ibara ya 8-(1) ina sema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote,na tena Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii.
(b) Lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za serikali yao kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.

Imenibidi kuanza na nukuu za ibara ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na hoja husika kutaka kupotoshwa na kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kutaka aina ya Muungano wautakao.

Muungano si hoja ya viongozi wanavyofikiri kiasi cha kuamua kuwekea mipaka ya kuujadili MuuNGANO TUUTAKAO.

Wakati mwingine na kubaliana na Watanzania wenzetu walioo huko visiwani kupinga mipaka ya kujadili Muungano.

Kwa mantiki hii kwanini serikali inataka kusababisha mgogoro mkubwa ambao mwisho wake ni umwagaji wa damu kwa kuzuia misingi ya mamlaka yote kwa wananchi kwa kuamua aina ya Muungano wautakao.

Utawezaje kuuboresha Muungano bila kujadili kasoro zake,hali kama hii ndiyo iliyopelekea katiba kuvunjwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano kukaa kimya na kuruhusu Zanzibar kujitangaza kama taifa huru.

Sipendi kuamini mwanasheria mkuu,waziri wa sheria na rais wanapoandaa miswaada kama kweli huwa wanaongozwa na katiba,au wanatoa ya kwao kichwani bila kufuata taratibu. Muungano unatakiwa uwe wa makubalianao wa pande zote mbili bila kujali watakachoamu wananchi kiwe, utawezaje kuwalazimisha wananchi waendelee na Muungano wanaoutaka viongozi na si wananchi, labda kuna maslahi binafsi kwa viongozi hao.


Pia ni haki yetu kujua na kuamua sababu zipi zinazotufanya tuungane.

Hizi ni dhama za uwazi na ukweli, makubaliano ya wananchi wa pande zote lazima yaheshimiwe na yasichakachuliwe vinginevyo Tanzania tuitakayo itakuwa ni ndoto.

ANGALIZO:

Tanzania tuitakayo itapatikana tu ikiwa haki ya misingi ya mamlaka ya wananchi itaheshimiwa.

Hatupendi kuongozwa na kupata Muungano utakaosabishwa na umwagaji wa damu,Tanzania ni nchi ya amani,amani hii ili iendelee na iyonekane si ya bandia wananchi wapewe fursa waliyoililia kwa miaka dahari kuamaua Muungano wautakao bila kuingiliwa na viongozi.Mwisho viongozi,kumbukeni cheo ni dhamana,hamto tumia cheo chenu kwa faida yenu binafsi bali kwa manufaa ya umma.


Mkilikumbuka hili amani ya nchi kamwe haitawekwa rehani.
 
Mkuu! Hata huyo aliye tia sahihi sheria ya kuandika katiba Mpya si unajuwa hana muda hata wa kusoma nakuchambua anacho letewa mezani!!! kazi yake ni kuuliza kama wanaomletea wameridhika ili atie sahihi
 
Back
Top Bottom