Athari ya kutumia majina ya viongozi (watu maarufu) katika shule zetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athari ya kutumia majina ya viongozi (watu maarufu) katika shule zetu.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Magehema, Apr 27, 2009.

 1. M

  Magehema JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wadau kuna athari yoyote (+ au -) ya kutumia majina ya viongozi au watu maarufu katika shule zetu. Mfano shule inaitwa St. Marian Secondary, St Peters Academy, Benjamin Mkapa High School, Mr. Bean Academy, Lowassa Sec School etc..:confused:
   
 2. moza

  moza Member

  #2
  Apr 27, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Athari zipo kotekote yaani positively and negatively, kwani km shule ikifanya vizuri,its a +ve effect, na ikifanya madudu, obviouslly -vity inakuwepo tene inakuwa strong kweli compared na +vity as far as matokeo are concerned.
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Majina mengine yana laana so shule nazo zinabeba laana. Hujasikia au kuona majambo yanayo wakuta watoto wanaitwa majina ya utata utata? Matatizo, Majonzi, Sikitiko, Majuto na mengine yanayofanana na hayo. Kuna mapepo ambayo yanaambatana na majina, kama mtu alikua na lipepo la wizi hata jina lake linasimamiwa na pepo la wizi, sasa tatizo mtoto wako akisoma katika hiyo shule anakua anavutwa na hilo pepo na kama familia na yeye mwenyewe ajasimama na Mungu basi tena lipepo linamkamata.
   
 4. M

  Magehema JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I do concur with you. Kuna mambo ya msingi ambayo hatujayaangalia kwa makini kabla ya kutumia majina ya viongozi au watu maarufu katika shule zetu. Mfano St Peter, huyu alikuwani mtakatifu, aliishi maisha ya kitakatifu ambayo inaweza kuwa ni chachu ya kusukuma maendeleo ya kitaaluma katika shule husika. Kina St. Teresa walikuwa ni role model, wanajali utu, wana ubinadamu na pia walikuwa tayari kujitolea kwa manufaa ya jamii. Kuna haya majina mengine kidogo haipendezi kuyatumia katika shule zetu. Haifai hata kidogo kutumia jina la kiongozi ambaye anatuhumiwa kwa ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi, mabavu, uonevu, kiburi nk. Ni vizuri wamiliki wa shule wakawa waangalifu katika kuchagua majina ya shule zao, vinginevyo ile lagacy na falsafa ya yule jina lake lililotumika ndo vikawa driving motive ya wanafunzi.
   
Loading...