Athari mbaya za Bongo Movies kuwa na Vilaza wengi ndani ya jamii

Ila chadema Ni Kama mna bonge la kamasi kichwani badala ya ubongo
Bongo " mavi" ndio jina lao halisi ni wapumbavu flan na mataga wa ccm hivi chadema wakiwa na kamasi kichwa ccm na mwendazake watakuaje!?? Hebu tuwe serious
 
ATHARI MBAYA ZA BONGO MOVIE KUWA NA VILAZA WENGI NDANI YA JAMII

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Wapo watu wataona nimewaandama hawa ndugu zetu, lakini lazima ukweli tuuseme. Hatuwezi sema kuwa hakuna athari chanya walizotupatia Bongo Movies ndani ya nchi yetu, zipo faida kadhaa, kama vile, kutoa ajira kwa watanzania, kuwa chanzo cha mapato kwa serikali, kutoa elimu kwa jamii kwa baadhi ya filamu, kumahasisha baadhi ya kampeni kama vile kutumia chandarua, uzazi wa mpango, janga la Ukimwi, malaria na magonjwa mengine. Kwa mazuri tunawapongeza.

Lakini leo tunazungumzia suala zima la athari za Bongo Movie ndani ya jamii yetu zinazotokana na uwepo wa vilaza wengi kwenye tasnia hiyo;

Athari hizo ni kama ifuatavyo;

1. Kupotosha na kuiharibu Jamii
Kama kuna Tasnia zilizopotosha jamii na kuzidisha mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii yetu basi ni Tasnia ya Filamu na Muziki. Leo Nitajikita zaidi huku kwenye filamu huku.
Mambo ambayo Bongo Movies wamepotosha kwenye nchi yetu tangu mwaka 2005 - 2021;

i/ Kupotosha jamii kuwa Maisha ya chuo ni Bata.
Hakuna tangazo lililowahi kutolewa kuwa maisha ya chuo ni bata isipokuwa maisha hayo tuliyaona kupitia filamu na maigizo kwenye Luninga. Bahati nzuri nchi yetu haina vyuo vikuu vingi hivyo wengi wetu habari za chuoni tulizisikia kwenye Luninga kipindi hicho tupo vijijini huko, Makanya,
Waigizaji wa wakati huo, hata wakati huu pia wakiigiza huigiza kana kwamba maisha ya chuo ni bata, kuvaa vinguo vya uchi, kusuka rasta, kunyoa viduku, yaani wakiigiza wanaigiza kana kwamba chuoni hakuna kusoma, unakuta scene nyingi zinaonyesha wakiwa kwenye vimbweta au night Club n.k

Bongo Movie wakiigiza mambo ya chuo kikuu unaweza ukadhani hakuna mambo ya maandamano, hakuna mambo ya Bodi ya mikopo, siasa, Rushwa, unyanyasaji, uonevu huko vyuoni wao wanachojikita zaidi ni ishu ya mapenzi tuu.
Hii imepotosha jamii, na wote tuliofika chuo tutakubaliana kuwa hakuna maisha ya bata huko chuoni zaidi ya kuhenyeka na shule. Hii pia imeathiri vjana wengi wanapofika shule wanajikuta wakitaka kuishi maisha ya bongo movies kama walivyokuwa wanayaona enzi wakiwa shule ya msingi na sekondari huko vijijini. Wengi hupata mimba, wengine hufeli kabisa, miongoni mwa athari zingine. Pia wameathiri wa sehemu kubwa kuwa kijana akitoka chuo basi kinachofuata ni kuajiriwa tena katika nafasi nyeti za Umeneja, Filamu nyingi zinaeleza jambo hilo. Chache sana zinaonyesha uhalisia kuwa kijana akitoka chuo basi atasota kitaa.

ii/ Kuharibu Nguvukazi ya taifa kwa jinsi ya kiume (Umario).
Filamu nyingi za kitanzania tangu miaka ya 2005 mpaka sasa, zinakuwa na maudhui yanayoonyesha kuwa Mdada wa kitajiri anampenda kijana wa masikini, anampa pesa, anampeleka kwenye nyumba yake(ya mwanamke), kisa kijana huyo ni handsome boy au mtanashati. Au jimama linatoka na kakijana kadogo, basi maisha huwa hivyo. Filamu hizo zimeharibu sana vijana wengi ndani ya jamii; hasa wanaoishi mjini. Vijana wamekuwa mario, wakiwaiga waigizaji wanaogiza kwenye filamu, utakuta kijana anasuka nywele, au anavaa hereni, wengine wale wenye sura ngumu hujikoboa ili nao waonekane. Ili tuu wanawake wa mjini wenye mapesa wawepende.
Nimeishi maeneo ya Sinza na Kinondoni, na kidogo Tabata maeneo ambayo wasanii hao ndio wapo wengi. Nimeshuhudia vijana wakienda mpaka kwa waganga ili tuu wapendwe na madada au majimama yenye pesa; Wakishawapata hao wa mama iwe kwa nguvu za giza au kwa ujanja wa mdomo(kipaji), kinachofuata ni kula tunda. Hapa vijana wengi wa mjini kutokana na mitindo yao ya maisha kuwa migumu wanajikuta pia wapo kwenye mtihani kwani miili yao haina nguvu ya kutosha, hivyo wanatafuta connections ya vumbi la Kongo, Mundende ganzi mujarabu, musinula mwinula, na madawa mengine ili waweze kusustain kwenye game, wasiachwe. Nisiongee sana upande huu sio lengo langu kwa leo.
Mwisho tunaona vijana wakiishia kujiremba kama wanawake na kukaa ndani kama wari wakisubiri kuletewa na majimama hayo au wanawake hao. Hii yote ni chanzo chake ni athari za filamu zenye maudhui ya umarioo.

iii/ Kuifundisha jamii maisha bandia.
Filamu nyingi hazina uhalisia, nyingi wasanii huigiza wakiwa kwenye maofisi makubwa na majumba manene, magari ya kifahari, simu ya maana n,k, Ukipeleka filamu ya kitanzania Marekani, kwa mtu asiyeijua Tanzania anaweza akadhani Tanzania ni moja ya nchi Tajiri duniani na watu wake wanauchumi wa kati au mkubwa kabisa, lakini kiuhalisia mambo sio hivyo. Sikatai uwepo wa movie za namna hiyo, ila ziwe chache, zile zenye maisha halisi ya kitanzania ndio ziwe nyingi zaidi. Hayo maofisi na magari wanayoigizia ni Watanzania wachache sana wanaoyatumia nina uhakika hawafiki milioni mbili nchi nzima.

Maisha bandia tunayaona pia katika matamasha na matukio wanayoyaandaa hao hao wasanii, unakuta msanii ati anaandaa tukio bandia kwenye Birthday yake ati anapewa Gari la kifahari, sijajua lengo la hayo ni nini, ila ni kiwango duni cha elimu na uchambuzi wa mambo ndio hupelekea wasanii wetu kufanya hayo. Mambo hayo yamefanya vijana wengi kufikiri maisha ni rahisi kiasi hicho, wengi wamejikuta wakichukia shule na kuiona haina maana kwa maigizo bandia ya waigizaji vilaza.

Nikiri wazi kuwa sijawahi ona Wasanii ninaowaheshimu wenye akili njema, na wenye uwezo mkubwa wakifanya hayo. Niwapongeze, najua wamebanwa na wingi wa vilaza na hawawezi kufurukuta.

2. MMOMONYOKO WA MAADILI
Hapana shaka kuwa Tasnia ya Bongo Movie na Muziki zimechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu taswira nzima ya maadili ya Mtanzania.
Filamu nyingi waigizaji huvaa viguo visivyoeleweka, kwa upande wa Dada zetu. Upande wa Mabraza hupaka rangi nywele wengine nyeusi wengine kijani basi ilimradi, wengi wanasuka wengi kubandika sticker masikioni kama hereni. Hii inapelekea vijana kwenye jamii kuiga mambo hayo.
Miaka 2005 Ilikuwa ni nadra sana kumuona mwanamke kavaa suruali akapita mtaani, kijijini ndio ilikuwa huwezi kuona kabisa mambo hayo. Lakini kupitia Bongo Movie na muziki mambo hayo yalichochewa kwa kiasi kikubwa, kwa saasa suruali sio agenda tishio tena, mtu anaweza kuvaa hata chupi akapita nayo barabarani. Hiyo ndio shida ya kuwa Kilaza.

Sijajua ni kigezo gani wanatumia kusajili hawa Wasanii, bila shaka ni kutokana na kuwa wengi ni Vilaza hivyo vigezo vyenye mantiki havizingatiwi. Kuna Msanii wa Bongo Fleva aliwahi kusema kuwa Bongo Movie ndipo walipo Wadangaji akimaanisha Malaya. Kwa maana neno Malaya kwa sasa limepewa hadhi nyingine na kuitwa UDANGAJI.
Sio ajabu kuona kwa sehemu kubwa waigizaji hasa wakike wakionyesha kwa sehemu kubwa maungo yao, nafikiri ni biashara, na hiyo haipo Tanzania tuu bali karibu nchi nyingi.

3. KUUA SOKO LA FILAMU NCHINI
Moja ya athari hasi za vilaza kuwa wengi kwenye Tasnia ya Filamu ni kuua soko la filamu hapa nchini. Unajua miaka ya 2005 ni tofauti na miaka ya sasa, na miaka ya sasa ni tofauti na miaka kumi ijayo au ishirini.
Zamani nchi yetu ilikuwa na wasomi wachache sana 2005, hivyo hata uelewa na exposure ya mambo ya filamu ilikuwa chini kabisa. Miaka 2005 kilichokuwa kina matter zaidi ni mtu kuonekana kwenye Luninga basi, bila kujali atasema nini basi watu watamheshimu. Miaka ile Tv zilikuwa chache, hivyo kumuona mtu kwenye Kioo/Luninga ilihitaji jitihada. 2005 hapakuwa na Smartphone, zilikuwepo Motorola, Nokia, na nyingi zilikuwa mkonga.
Hivyo waigizaji wa kipindi kile hata wasingekuwa na elimu kubwa bado wangesikilizwa kwani jamii ilikuwa gizani. Hivyo kuigiza ilihitaji akili ndogo sana, filamu simple zilipendwa kutokana na akili za wakati ule. Elimu haikuwa lazima sana wakati ule.

Uwezo wa Kanumba kwenye tasnia ya filamu mbali na kipaji chake pia ulichangiwa na elimu yake, Kanumba alikuwa Smart hata shuleni, alifika Kidato cha sita, na kwa miaka hiyo kufika kidato cha sita basi lazima kichwani lazima ziwemo. Ndio maana watu walimuona Kanumba kama mtu anayeigiza kwa namna tofauti.

Sasa kinachoua Tasnia ya Filamu hapa nchini ni kuwa kizazi kimebadilika, watu wengi sasa wamesoma, wanaulewa na wana Exposure, karibu kila nyumba kuna Luninga, watu wana Smartphone wanaouwezo wa Ku-access taarifa nje ya taifa letu. Kuigiza sio kuonekana tuu kwenye Tv bali unafanya nini kwenye Tv. Siku hizi kila mtu anaweza kuonekana kwenye Tv kupitia Simu janja za mkononi, watu wanauwezo wa kujirekodi na kuposti video mtandaoni.

Kizazi kimebadilika lakini wasanii hawajabadilika, automatik lazima Tasnia ife kifo cha asili. Watu wanauwezo wa kuangalia mambo katika angle tofauti tofauti, upeo wa watu ni mkubwa hivyo mwigizaji anapaswa awe naye pia anauwezo kumzidi anayemtazama. Muigizaji ni kama mwalimu, anafundisha au anaujumbe anataka kuufikisha kwa Mtazamaji/mwanafunzi. Mwalimu lazima awe zaidi ya mwanafunzi kiuwezo na kiuelewa. Mwigizaji anapokuwa na uwezo mdogo kuliko Mtazamaji automatik filamu yake haiwezi kuangaliwa, labda waangalie watoto wadogo.

Baada ya kusema hayo; sasa nimalize kwa kutoa hints chache za kuwa msanii katika zama hizi

JINSI YA KUWEZA KUWA MUIGIZAJI KATIKA ZAMA HIZI
1. Lazima uwe na elimu kuanzia ngazi ya shahada katika fani yoyote ile. Ukibisha endelea kubisha lakini huo ndio ukweli
2. Lazima uwe na Exposure ya dunia inaendaje
3. Lazima uwe na kipaji iwe cha asili au chakufundishwa
4. Lazima uongozwe na mtu mwenye Elimu
5. Lazima uwe na uwezo mkubwa wa Akili kuliko 80% ya watazamaji wa filamu zako. Uwe na uwezo wa kuzibadilisha akili zao na kuziendesha vile utakavyo, wasijue mwisho wa filamu. Labda wachache ambao lazima wawepo.
6. Lazima Mtunzi na Mtayarishaji awe na Elimu zaidi ya shahada moja
7. Lazima mchukua Kamera awe na elimu zaidi ya shahada moja
8. Lazima Cast unaoigiza nao 80% wawe na elimu ya juu kama wewe

Hapo ndipo mambo sijui ya vifaa na mambo mengine yafuate, lakini unatafuta mtaji alafu mwenyewe kilaza, robo tatu yenu ni vilaza, nani awepo mtaji huyo?

ZINGATIA: Muigizaji ni mwalimu wa jamii, hivyo lazima awe na content ya kutosha kuzidi waliowengi ndani ya jamii yake. Hata darasani mwalimu asiye na content na sio competent lazima wanafunzi wamchukie, na wala somo lake haliwezi kufaulisha.

Ulikuwa nami Nyota ya tibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Katavi
Nakuunga mkono kwa 100%
 
Nilikuwa na ndoto ya kuwa muigizaji na director nikiwa mdogo sana, kilichonikatisha ndoto zangu ni jinsi bongo movie ilivoshikiliwa na makahaba na mashoga, nilighairi kabisa, hata daftari langu la stori sijui liko wapi, Bongo movie umeiongelea kidogo sana ukiichimba vizuri itakutia kichefu kichefu.
 
Bado unanafasi Mkuu. Wewe ndio unaweza kuwa sehemu ya kuleta matokeo chanya kwenye Tasnia hiyo
 
Nilikuwa na ndoto ya kuwa muigizaji na director nikiwa mdogo sana, kilichonikatisha ndoto zangu ni jinsi bongo movie ilivoshikiliwa na makahaba na mashoga, nilighairi kabisa, hata daftari langu la stori sijui liko wapi, Bongo movie umeiongelea kidogo sana ukiichimba vizuri itakutia kichefu kichefu.
Sasa wenda industry ilikuwa inakusubiri wewe ulete mabadiriko.
 
Ukiangalia bongo movie za kina Ray na wema sepetu unaweza kusema watu wa dasilamu wote Wana maisha mazuri na wanatembea na gari kali

Ndo maana hata vijana wengi wa mikoani wanakimbilia daslamu mwsho wa siku wanaharibikiwa zaid
Tanzania uigizaji ni wa kiwango cha chini mno mno. Kwanza wanaigiza vitu ambavyo hawana uwezo navyo. Wangejifunza sana kama wangekuwa wanajaribu kufuata nyao za watu kama akina Mzee Jongo na Jangala. Hawa walikuwa wanaigiza michezo ya redio na maigizo yao yali-base kwenye matukio yanayotokea kwenye jamii.
 
wacha wivu!! hao wenye bachelor degree wako wapi?? hayo ndo mavilazaaaaa!!! Mond ako juu!! ana mihela kuliko wanamuziki wenye bachelor wako hao!! hata kuwa Msanii tu!! kipaji chako kinakupa Masters degree! tatizo ni karatasi tu huna!

Kingine wanavijiji mna shida kubwa sana sana ya uelewa.....ku-act wakiwa na Magari makubwa. Majumba nk! ndo maana ya Neno usanii!......weye unataka wafanye km mnavo jadiliana na wanakijiji wenzako!!

wewe nawe ingia kwenye tasnia ufanye unavohisi ni sahihi!! hujakatazwa hutaki waache km walivo.... kwani lazima kutizama movie zao?? km inakuuma saana si ujikate kivyako tuuu?....ivo wanavyo act ndo vijana walivyo km kwenu kijijini wameanza 2000 kuvaa suruali basi walichelewa sana!

la mwisho ...jifunze kuheshimu kazi za watu wenzio!! labda km hujui film actors manake nini!
 
Ulipoambiwa usome uliona wazazi wako Wajinga ona sasa unavyodhalilika, sasa umeandika kitu gani hapa.

Rudi shule Kwanza ili uweze kujadili Kwa kutumia Akili.
 
Ulipoambiwa usome uliona wazazi wako Wajinga ona sasa unavyodhalilika, sasa umeandika kitu gani hapa.

Rudi shule Kwanza ili uweze kujadili Kwa kutumia Akili.
Acha wivu wa kike huo!! na roho mbaya za kiswahili hizo!...shule gani za UPE hizo ulizo soma weye ndo nikasome mie Thubutuu!!!!?? ndo maana uko hivo!! hizo shule za Bongo nazo shule??? kabisaaa zee zima unatamba niende darasa ya chini ya Mwembe?.....shule ambazo huajiliwi popote Duniani?? Pwiii!
download.jpg
kwa hasira hizi wewe ni matokeo ya hii shule hapo pichani kabisaa wala hamjifichi.....umeshindwa kuwa km wasanii. sasa unalalama tu.

unadhani km umetokea mahali hapa utakuwa na ubongo mzuri kweli? unaona ya wengine tuuuu unaumia moyo!! fanya yako mazuri tuone!! ..........halafu nakushauri utoke humu Jf! siyo jukwa sahihi kwako.... jiuzuru tu! hufai!! ....!
 
Acha wivu wa kike huo!! na roho mbaya za kiswahili hizo!...shule gani za UPE hizo ulizo soma weye ndo nikasome mie Thubutuu!!!!?? ndo maana uko hivo!! hizo shule za Bongo nazo shule??? kabisaaa zee zima unatamba niende darasa ya chini ya Mwembe?.....shule ambazo huajiliwi popote Duniani?? Pwiii!View attachment 2247553kwa hasira hizi wewe ni matokeo ya hii shule hapo pichani kabisaa wala hamjifichi.....umeshindwa kuwa km wasanii. sasa unalalama tu.

unadhani km umetokea mahali hapa utakuwa na ubongo mzuri kweli? unaona ya wengine tuuuu unaumia moyo!! fanya yako mazuri tuone!! ..........halafu nakushauri utoke humu Jf! siyo jukwa sahihi kwako.... jiuzuru tu! hufai!! ....!

😀😀😀

Sasa unalia nini?
Mimi sio Baba yako, wewe shule Kama ulikimbia shule ukaenda kuigiza upuuzi subiri wataangalia wenzako ambao walikimbia umande.

Mtu asiyesoma kitu kizuri kwake ni aonekane kwenye Luninga😀😀😀
 
Tasnia ya filamu ya Bongo movie ni takataka kabisa huwezi angalia ujinga ujinga tu.

Ukitaka kustaajabu ya Bongo mavie angalia scene mfano za udaktari na character wake mtu anajifanya daktari wakati huo ajui a,b,c Wala d kuhusu utabibu

Elimu Elimu Elimu
 
Alafu watakuambia kipaji, kipaji au upuuzi,
Kuna Dani zinahitaji elimu ili kipaji kiwe Bora,
 
wacha wivu!! hao wenye bachelor degree wako wapi?? hayo ndo mavilazaaaaa!!! Mond ako juu!! ana mihela kuliko wanamuziki wenye bachelor wako hao!! hata kuwa Msanii tu!! kipaji chako kinakupa Masters degree! tatizo ni karatasi tu huna!

Kingine wanavijiji mna shida kubwa sana sana ya uelewa.....ku-act wakiwa na Magari makubwa. Majumba nk! ndo maana ya Neno usanii!......weye unataka wafanye km mnavo jadiliana na wanakijiji wenzako!!

wewe nawe ingia kwenye tasnia ufanye unavohisi ni sahihi!! hujakatazwa hutaki waache km walivo.... kwani lazima kutizama movie zao?? km inakuuma saana si ujikate kivyako tuuu?....ivo wanavyo act ndo vijana walivyo km kwenu kijijini wameanza 2000 kuvaa suruali basi walichelewa sana!

la mwisho ...jifunze kuheshimu kazi za watu wenzio!! labda km hujui film actors manake nini!
Kwahili povu itakua ushajaribu bongo movies ila mpaka leo unaelekea uzeeni haijakutoa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom