Atembea na Mke wa Mtu, Akumbwa na Haya.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atembea na Mke wa Mtu, Akumbwa na Haya..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Felixonfellix, May 12, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Hali aliyo nayo Akram hivi sasa bada ya kumwagiwa tindikaliWednesday, May 12, 2010 3:55 AM
  Hizi ni picha za kusikitisha za mwanaume mwenye umri wa miaka 25 wa nchini Uingereza ambaye alipewa kipigo na kisha kumwagiwa tindikali baada ya kutuhumiwa anamchukua mke wa mtu.Awais Akram alijeruhiwa vibaya baada ya kumwagiwa tindikali na hata baada ya matibabu makubwa mwili wake umebaki na majeraha yanayotisha kuanzia kichwani mpaka miguuni.

  Sura ya Akram imeharibika vibaya sana wakati nywele zale zinamea kwenye sehemu ya mbele tu ya kichwa chake ambayo ilinusurika na tindikali.

  Majeraha zaidi ya tindikali yapo pia sehemu mbalimbali za mwili wake kama vile kifuani, tumboni, mgongoni, miguuni na mikononi.

  Yote haya yaliyomkumba Akram yalisababishwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 24 aliyefahamiana naye kwenye FaceBook aliyejulikana kwa jina la Sadia Khatoon.

  Kaka yake Sadia aliyeitwa Vakas aligundua uhusiano wao baada ya kuwaona pamoja mitaani na alipogundua wanawasiliana kwa kutumia mtandao wa FaceBook alithibitisha kuwa dada yake anaisaliti ndoa yake.

  Mume wa Sadia, Shakeel Abassi na yeye alipogundua uhusiano wa Akram na mkewe kwenye FaceBook, alikula njama na kaka yake Sadia wamteketeze Akram kwa kuingilia ndoa za watu.

  Sadia alilazimishwa na kaka yake aliyeshirikiana na mumewe amlaghai Akram afike kwenye eneo ambalo wao walipanga kufanya shambulizi lao.

  Akram naye bila kujua hili wala lile alijitosa kwenye eneo la tukio akijua anaenda kukutana na Sadia.

  Alipofika kwenye eneo la tukio, Akram alijikuta akipewa kipigo cha nguvu kabla ya kumwagiwa tindikali iliyomuunguza sehemu kubwa ya mwili wake.

  Akram alinusurika maisha yake lakini hadi leo bado anaendelea kupatiwa matibabu.

  Sadia na mumewe walifanikiwa kutoroka Uingereza na kukimbilia kwao Pakistan ambako inasemekana wanaendelea kujificha huko.

  Kaka yake Sadia, Vakas alikamatwa na jana ndio ilikuwa hukumu yake kwenye mahakama ya Old Bailey jijini London.

  Vakas alipatikana na hatia ya kufanya jaribio la kuua mtu na alihukumiwa kwenda jela miaka 30.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii habari niliiona jana kule kwenye jamvi la malavi davi.
  naona imerudiwa tena huku.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmmh huu ni unyama! badala ya kumtia addabu dada yako anaetembea nje ya ndoa unamvamia kaka wa watu! pengine hata hajui kama mtu kaolewa! aggggr


  note: sifurahii wanaume kutembea na wake za watu
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine mtu unaweza kufanya jambo then akili ikitulia unajiona mjinga kabisa. Huyo bwana mwenye mke ni mpuuzi kabisa kwani nina uhakika kwa kitendo alichofanya huenda na yeye huyo mkewe akamkosa pia. Maana once akikamatwa maana yake anakwenda lupango na mke unamuacha nje watu wanaendelea kutumia...ndio mambo ya akili za kuambiwa haya unashindwa kuchanganya na zako angalau uwe na busara.. Sipendi kumlaumu huyu jamaa aliyeumizwa maana hapa kuna mawili..aidha hakuambiwa na huyo dada kama ana mume au aliambiwa lakini bado wakajijengea mazingira ya kujiamini na kuendelea na uhusiano wao...
   
Loading...