ATCL yashtakiwa Marekani kwa kuvunja Mkataba; kulipa karibu bilioni 10

This is not a joke anymore...Tuna Dowans, Rites na sasa ATCL...hahahaha! Hii ni balaa....
 
Yaani habari ni za kulipa watu tuuuu............................, lakini sioni ni nani anawajibishwa kwa kusababisha huu uozo... kweli hii nchi imeoza.
 
nA MIMI lazima nifikirie jinsi nitakavyoidai Tanzania, hivi lile dege lao si ndio lilikuwa bovu? sasa koasa nini tena hapa, halafu huyu Nundu huyu...hana maana kabisa
 
Mtalipa/tutalipa hata madeni ya nguo za ndani za watawala ili mradi tumekubali mtego wao wa udini uciokuwepo ili wapate huruma tucungane dhidi yao
 
Kwanini wasim-sue na huyu anayetuharibia nchi yetu?

EO 12958 DECL: 07/30/2010
TAGS PREL, PGOV, TZ
SUBJECT: TANZANIA PRESIDENT'S SON HOSTS QATARI DRUG DEALERS
Classified By: DCM David R. Burnett

(SBU) Embassy Dar es salaam learned July 30 that Tanzania's sitting president's son XXXXXXXX was reportedly hosting a special party for foreign drug dealers in Masaki Dar es salaam. The persons flew into Tanzania from London as opposed to flying DIRECTLY FROM Qatar to disguise their trail. At the party lot of money exchanged hands. The party was organized to congratulate XXXXXXXXX for having facilitated the passage of the consignment through Dar to a major distribution hub in Europe. All in all, XXXXXX was paid $ 5million and a ML Mercedes SUV in this deal.

However, high ranking government officials were also involved in the business, and they may have participated or assisted the passage of the drug shipment from IRAN which entered Tanzania as carpets. The consignment was later re-parked and shipped to Europe as coffee consignment. The Prime Minister's office was contacted by our intelligence personnel, to inquire whether it could shed some light on the matter and was told by PM office staff that they were not aware of the issue but would look into it.

The officer then contacted Internal Affairs Minister, Lawrence Masha's office but the Minister's office declined to make him available to discuss the matter. Masha's staff later informed Embassy that Masha would be hosting Foreign dignitaries.
 
Kwanini wasim-sue na huyu anayetuharibia nchi yetu?

EO 12958 DECL: 07/30/2010
TAGS PREL, PGOV, TZ
SUBJECT: TANZANIA PRESIDENT'S SON HOSTS QATARI DRUG DEALERS
.

This has not been substanciated.... kama kuna mwenye proof azilete tuzipeleke panapohusika
 
Ilianzia IPTL, sasa dowans, tena ATCL.. sitoshangaa magari ya ikulu nayo yakikamatwa kwa breach of contract.... nadhani sasa muda wa kuamka umefika tuseme hapana, na tuwe tayari kuitetea nchi kwa gharama zozote!!!!
 
DUH!!! Mkuu sasa this is too much.!!
Kila kona wanatubana mbavu....hizi nchi matajiri ipo siku tutaambiwa tumenunuliwa na kulazimishwa kubadilia pasport na vitambulisho sasa.
Mi acha ninyamaze jamani nimechoka.
 
should ppl not take to streets,haya mambo yataendelea,Tz imegeuka shamba la bibi na viongozi hawajali utafikiri sio wa-tz...Tanzanians wake up
 
ATCL yashtakiwa Marekani Send to a friend Wednesday, 23 February 2011 20:00 0diggsdigg

nundu.jpg
Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omar Nundu

Ramadhan Semtawa
JINAMIZI la taasisi za serikali kushtakiwa nje ya nchi na kudaiwa mabilioni ya shilingi, limehamia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ambalo limeburuzwa kortini na Kampuni ya Celtic Capital Corporation ya Marekani likidaiwa sh 1.6 bilioni huku Shirika la Ndege Afrika Kusini (SAA) likidai Sh6.3 bilioni, kutokana na kuvunja mkataba.

Mpaka Desemba 31, mwaka jana, deni la ATCL lilikuwa Sh 75.99 bilioni, ambazo kati ya hizo, Sh 24.34 bilioni zilikuwa deni la ndani na Sh 51.65 bilioni, deni la nje likiwamo la SAA na Celtic Capital Corporation.

Kati ya madeni hayo, ya nje, zipo dola 24.72 milioni (sawa na Sh 37 bilioni), ambazo ni za Kampuni nyingine ya Wallis Trading Inc, linalotokana na kukodi ndege ya Air Bus A320.

Taarifa ya hali ya utendaji ya ATCL kwenda kwa Kamati ya Bunge ya Miundimbinu, ambayo gazeti hili, imefanikiwa kupata nakala yake jijini Dares Salaam jana, inaonyesha tayari mahakama,nchini Marekani imetoa kibali cha kukamatwa mali za shirika hilo, kwa ajili ya kufidia deni.

Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omar Nundu,alifafanua kwamba hadi sasa, licha ya kupata kibali cha mahakama cha kukamata mali za ATCL, bado wadai hao hawajaweza kukamata mali yoyote ya shirika.

Kwa sasa nchi inatikiswa na kesi ya Dowans ambayo Mahakama ya Usuluhishi ya Kibiashara ya Kimataifa (ICC-Court), imetoa hukumu kwa kuagiza Tanesco kuilipa kampuni hiyo, Sh 94 bilioni, hatua ambayo inapingwa kwa nguvu na Watanzania wengi.

Ukiacha ya ICC dhidi ya Tanesco, tayari pia Kampuni ya City Water, iliwahi kuishataki serikali katika mahakama hiyo ya kimataifa, lakini ilibwagwa, huku pia Kampuni ya Richmond nayo iliishtaki Tanesco na kushindwa.

Kuhusu sakata la ATCL, ripoti hiyo, inaonyesha deni la shirika hilo, hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana lilifikia Sh75.99 bilioni, ambazo deni la ndani na Sh24.34 bilioni, Sh 51.65 bilioni ni deni la nje na kati ya madeni hayo ya nje, dola 24.72 milioni (sawa na Sh37 bilioni) ni deni la Kampuni Wallis Trading Inc, litokanalo na kukodi ndege ya Air Bus A320.

Mhandisi Nundu Waziri mwenye dhamana ya usafiri wa anga, alisema madai ya Celtic Capital Corporation yanahusu kukodisha ndege na la SAA linatokana na kuvunjwa mkataba huo, mwaka 2006.

ATCL ilifunga ndoa na SAA Novemba 2002, baada ya kubinafsishwa lililokuwa shirika la Ndege Tanzania, ambalo shirika hilo la kigeni lilinunua hisa asilimia 49 za serikali ndani ya ATC, hata hivyo ubia huo, ulikabiliwa na matatizo ya kiundeshaji na kulazimika kusitishwa Agosti, 2006 na shirika hilo, kurejeshwa serikalini.

Wakati mzigo huo, ukiwa juu ya ATCL ambalo liko taabani, Kampuni ya China Sonongol International Limited (CSIL), imejitoa katika ununuzi wa hisa za ATCL na hivyo, kuondoa ndoto ya shirika hilo kufufuka kwa kupata mtaji wa zaidi ya sh 500 bilioni.

Nundu alifafanua kwamba , Machi 2007 serikali ilifanya mazungumzo na CSIL na kusaini hati ya makubaliano (MoU) ili kuendeleza shirika hilo, na kampuni hiyo, ilikubali kusaidia mpango wa muda mrefu uliopaswa kuanza mwaka 2007/08, kwa kuahidi kutoa kiasi hicho ambacho ni dola 507.7milioni na kwa kuanza ilitoa dola 20 milioni (sh 23bilioni).

"Mpango huo, ungewezesha ATCL kununua ndege tisa za kisasa. Kwa kuanzia utekelezaji CSIL ilitoa zaidi ya dola 20.21 milioni (takribani Sh30 bilioni) kwa ATCL ikiwa ni pamoja na kununua ndege mbili aina ya Bombardier Dash8- Q-300 ambazo ni mali ya ATCL,"alisema. Mhandisi Nundu.

Alisema CSIL ilikubali kununua asilimia 49, ya hisa za serikali ndani ya ATCL na serikali ya Tanzania iwe na hisa asilimia 51.

"Hata hivyo, kwa sasa CSIL imebadili msimamo wake kuhusu ununuzi wa hisa za ATCL. CSIL imeeleza haiko tayari tena kuwa mwanahisa katika Kampuni ya Ndege Tanzania," alifafanua Nundu.

Alisema kutoka na msimamo huo, wizara ilishindwa kuendelea na majadiliano na CSIL na imependekeza kusitisha mazungumzo na kampuni hiyo ya China.

Kuhusu hatua nyingine za kutafuta wawekezaji

Waziri Nundu alisema serikali, imeanza mazungumzo ya awali na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na Kampuni ya Borodino kutoka Urusi.

"Majadiliano ya awali na Turkish Airlines yalifanyika Oktoba 2010, ambayo kimsingi, Uturuki imeonyesha ingependa kuanzisha kampuni mpya kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania badala ya kuwekeza kwenye ATCL,"alisema.

"Kimsingi kampuni ya Borodino inapendekeza ianzishe kampuni mpya ya ndege hapa nchini ambayo itamilikiwa kwa asilimia 100 na Borodino. Majadiliano na kampuni mbili, yataendelea,''alisema.

ATC imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya kifedha tangu ilipofunga ndoa na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ambayo ilivunjika katika mazingira tata na kuacha shirika hilo, likiwa taabani.
 
ATCL yashtakiwa Marekani Send to a friend Wednesday, 23 February 2011 20:00 0diggsdigg

nundu.jpg
Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omar Nundu

Ramadhan SemtawaJINAMIZI la taasisi za serikali kushtakiwa nje ya nchi na kudaiwa mabilioni ya shilingi, limehamia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ambalo limeburuzwa kortini na Kampuni ya Celtic Capital Corporation ya Marekani likidaiwa sh 1.6 bilioni huku Shirika la Ndege Afrika Kusini (SAA) likidai Sh6.3 bilioni, kutokana na kuvunja mkataba.

Mpaka Desemba 31, mwaka jana, deni la ATCL lilikuwa Sh 75.99 bilioni, ambazo kati ya hizo, Sh 24.34 bilioni zilikuwa deni la ndani na Sh 51.65 bilioni, deni la nje likiwamo la SAA na Celtic Capital Corporation.

Kati ya madeni hayo, ya nje, zipo dola 24.72 milioni (sawa na Sh 37 bilioni), ambazo ni za Kampuni nyingine ya Wallis Trading Inc, linalotokana na kukodi ndege ya Air Bus A320.

Taarifa ya hali ya utendaji ya ATCL kwenda kwa Kamati ya Bunge ya Miundimbinu, ambayo gazeti hili, imefanikiwa kupata nakala yake jijini Dares Salaam jana, inaonyesha tayari mahakama,nchini Marekani imetoa kibali cha kukamatwa mali za shirika hilo, kwa ajili ya kufidia deni.

Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omar Nundu,alifafanua kwamba hadi sasa, licha ya kupata kibali cha mahakama cha kukamata mali za ATCL, bado wadai hao hawajaweza kukamata mali yoyote ya shirika.

Kwa sasa nchi inatikiswa na kesi ya Dowans ambayo Mahakama ya Usuluhishi ya Kibiashara ya Kimataifa (ICC-Court), imetoa hukumu kwa kuagiza Tanesco kuilipa kampuni hiyo, Sh 94 bilioni, hatua ambayo inapingwa kwa nguvu na Watanzania wengi.

Ukiacha ya ICC dhidi ya Tanesco, tayari pia Kampuni ya City Water, iliwahi kuishataki serikali katika mahakama hiyo ya kimataifa, lakini ilibwagwa, huku pia Kampuni ya Richmond nayo iliishtaki Tanesco na kushindwa.

Kuhusu sakata la ATCL, ripoti hiyo, inaonyesha deni la shirika hilo, hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana lilifikia Sh75.99 bilioni, ambazo deni la ndani na Sh24.34 bilioni, Sh 51.65 bilioni ni deni la nje na kati ya madeni hayo ya nje, dola 24.72 milioni (sawa na Sh37 bilioni) ni deni la Kampuni Wallis Trading Inc, litokanalo na kukodi ndege ya Air Bus A320.

Mhandisi Nundu Waziri mwenye dhamana ya usafiri wa anga, alisema madai ya Celtic Capital Corporation yanahusu kukodisha ndege na la SAA linatokana na kuvunjwa mkataba huo, mwaka 2006.

ATCL ilifunga ndoa na SAA Novemba 2002, baada ya kubinafsishwa lililokuwa shirika la Ndege Tanzania, ambalo shirika hilo la kigeni lilinunua hisa asilimia 49 za serikali ndani ya ATC, hata hivyo ubia huo, ulikabiliwa na matatizo ya kiundeshaji na kulazimika kusitishwa Agosti, 2006 na shirika hilo, kurejeshwa serikalini.

Wakati mzigo huo, ukiwa juu ya ATCL ambalo liko taabani, Kampuni ya China Sonongol International Limited (CSIL), imejitoa katika ununuzi wa hisa za ATCL na hivyo, kuondoa ndoto ya shirika hilo kufufuka kwa kupata mtaji wa zaidi ya sh 500 bilioni.

Nundu alifafanua kwamba , Machi 2007 serikali ilifanya mazungumzo na CSIL na kusaini hati ya makubaliano (MoU) ili kuendeleza shirika hilo, na kampuni hiyo, ilikubali kusaidia mpango wa muda mrefu uliopaswa kuanza mwaka 2007/08, kwa kuahidi kutoa kiasi hicho ambacho ni dola 507.7milioni na kwa kuanza ilitoa dola 20 milioni (sh 23bilioni).

"Mpango huo, ungewezesha ATCL kununua ndege tisa za kisasa. Kwa kuanzia utekelezaji CSIL ilitoa zaidi ya dola 20.21 milioni (takribani Sh30 bilioni) kwa ATCL ikiwa ni pamoja na kununua ndege mbili aina ya Bombardier Dash8- Q-300 ambazo ni mali ya ATCL,"alisema. Mhandisi Nundu.

Alisema CSIL ilikubali kununua asilimia 49, ya hisa za serikali ndani ya ATCL na serikali ya Tanzania iwe na hisa asilimia 51.

"Hata hivyo, kwa sasa CSIL imebadili msimamo wake kuhusu ununuzi wa hisa za ATCL. CSIL imeeleza haiko tayari tena kuwa mwanahisa katika Kampuni ya Ndege Tanzania," alifafanua Nundu.

Alisema kutoka na msimamo huo, wizara ilishindwa kuendelea na majadiliano na CSIL na imependekeza kusitisha mazungumzo na kampuni hiyo ya China.

Kuhusu hatua nyingine za kutafuta wawekezaji

Waziri Nundu alisema serikali, imeanza mazungumzo ya awali na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na Kampuni ya Borodino kutoka Urusi.

"Majadiliano ya awali na Turkish Airlines yalifanyika Oktoba 2010, ambayo kimsingi, Uturuki imeonyesha ingependa kuanzisha kampuni mpya kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania badala ya kuwekeza kwenye ATCL,"alisema.

"Kimsingi kampuni ya Borodino inapendekeza ianzishe kampuni mpya ya ndege hapa nchini ambayo itamilikiwa kwa asilimia 100 na Borodino. Majadiliano na kampuni mbili, yataendelea,''alisema.

ATC imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya kifedha tangu ilipofunga ndoa na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ambayo ilivunjika katika mazingira tata na kuacha shirika hilo, likiwa taabani.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #8 Time yetu TZA. 2011-02-24 10:49 Maoni yenu wote ni ukweli mtupu. Umoja huu ndiyo nguvu za marekebisho. Sote tuna Amini kuwa kuna upungufu mkubwa.
Tatizo kubwa humu kuna kuogopana na kufunika mambo. kwa kuwa Tanzania hatuna utamaduni wa KUWAJIBIKA mambo yetu yana haribika kuanzia ngazi za chini na kuelekea juu. " msingi mbovu "
Quote

0 #7 issa moshi 2011-02-24 10:49 hawa jamaa wamesha uza kila kitu nchini hakuna kitu wananchi walicho pata zaidi ya umaskini wa kutupwa kilcho baki kidogo ni ardhi ambayo sasa hivi inauzwa kwa watu ambao hawajuwi hata kuimba wimbo wa taifa sisi sikama tunapinga uwekezaji tunacho pinga sisi ni uwongozi mbovu wa ccm ambao nadhani baada ya kipindi kifupi kijacho kama wananchi wasipo amka kwa sasa watajikuta wote wanafanya kazi za vibaruwa kwa wageni nahicho ndicho kinacho kuja tanzania sijuwi kama hawa mnao waita waheshimiwa wanakiona kitu hicho kwanza nani kawapa jina la waheshimiwa mtu jiheshim kwanza wewe ndio watu wengine wakuheshim
Quote

+2 #6 Mwananzengo 2011-02-24 10:30 Guys, Inakuwaje kila kitu kinafeli tu? Inakuwaje kila kitu cha watanzania kinafeli tu? Does it mean hakuna watu wanaoweza kusimamia vizuri Parastatals? Hakukuwa na haja ya ATCL Kufilisika wakati hawakuwa na competitors nchini. Hakukuwa na haja ya TRL kuanzishwa wakati Reli yoote ni ya kwao tu..Au ndo " La kuvunda halina ubani?" Na kama tutaishi kwa kutegemea wawekezaji on everything, we are getting NO Where..!
Quote

0 #5 JAMES 2011-02-24 10:11 ACHENI U[NENO BAYA] NYINYI WATANZANIA MSIOKWENDA SHULE. MNA UFINYU WA KUWAZA NA KUFANYA ANALYSIS. TATIZO LA TANZANIA KILA KITU KIMEKUWA SIASA. MAJIRANI WENU WA KENYA, UGANDA, RWANDA NA HATA BURUNDI WANAWACHEKA NA JINSI MNAVYOTAKA KUENDESHA NCHI. KATIKA STAILI HII TUTAACHWA MBALI. SASA LUGHA IMEKUWA UFISADI UFISADI. INAONYESA JINSI GANI BABU SLAA NA CHADEMA KWA UJUMLA WAMELETA SUMU KATIKA MAWAZO FINYU YA BAADHI YA WATANZANIA. BABU SLAA ANA NDOTO ZA KUINGIA IKULU KWA NJIA YA MKATO KAMA ILIVYOTOKEA HUKO NCHI ZA KIARABU. SASA ANAANZA KARATA YAKE HUKO MWANZA. KILA MKIANGALIA KULIA KUSHOTO MNAONA UFISADI, HAKUNA ANLYSIS NZURI INAYOFANYIKA. WATANZANIA WAPEWA SUMU KUFIKIRI ETI MALI YOTE YA NCHI IPO CHINI YA ROSTAM, LOWASSA, CHENGE. JARIBUNI KUELEWA KIINI CHA MATATIZO YENU BADALA YA KUTAFUTA SCAPEGOATS.Quoting KB,mississippi:
kila kitu kinamwisho wake, nawasihi wote wenye ushahidi wa ufisadi katika mashirika ya ndege, reli na umeme tafadhali hifadhini ushahidi wenu vizuri. SOON IT WILL BE OVER.
trust me​
Quote

+1 #4 MKWELI 2011-02-24 09:02 KWA KWELI CCM? KWA NINI MLIAMUA KUUZA HAYO MASHIRIKA? SASA BADO KWENYE MADINI SASA HIVI TUTASIKIA TUMEPELEKWA MAHAKAMANI KWA MADINI YETU WENYEWE. JAMANI NCHI IMEWASHINDA LAKINI HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA NA NCHA HAIPO MBALI. SISI SIO WATU WA KUDHALILISHWA KILA SIKU KWA MALI ZETU WENYEWE, NANI KATUFIKISHA HAPA? FIKIRIA MNAKODISHA MADINI HALAFU SERIKALI INAPATA 3% MUWEKEZAJI 97% JE UNATEGEMEA UNAWEZA KUFUFUA CHOCHOTE KILE. HALAFU MNATUDANGANYA NA KILIMO KWANZA, MMEFILISI KILA KITU MNATUDANGANYA NA KILIMO, WATANZANIA WA LEO SIO WA JANA IPO SIKU YENU TU. KESHO MTAWANYANGANYA ARDHI YA KILIMO WANANCHI MUWAUZIE MABWANA ZENU HILO NDILO MNALOFIKIRIA KWENYE KILIMO KWANZA KWANI KILA KITU MMEUZA NA NCHIIMEKUWA MASIKINI YA KUTUPA. CCM,CCM,CCM!!! CHAMA HATARI KABISA.
Quote

+3 #3 Derek Msuya 2011-02-24 08:04 Hapo kuna kauongo flani kutuka kwa Bw. Nundu.CSIL walitaka kuleta watu wao kuhead cheo cha DG,Director of Operations,na chief wa finance.Serikali ikagoma ndo maana wakaamua kuachana na mpango wa kuwekeza.Mtu gani akupe fedha nyingi halafu awaache mcontrol kampuni wakati anajua ishu zenu nyingi za kifisadi
Quote

+2 #2 KB,mississippi 2011-02-24 04:58 kila kitu kinamwisho wake, nawasihi wote wenye ushahidi wa ufisadi katika mashirika ya ndege, reli na umeme tafadhali hifadhini ushahidi wenu vizuri. SOON IT WILL BE OVER.
trust me
Quote

+1 #1 Mhifadhi 2011-02-24 04:53 Hivi ina maana kila shirika hapa nchini linadaiwa na litashitakiwa. Sasa viongozi wetu walikuwa wapi hadi mirundikano yote hii inatokea bila kuiona? je wanasheria wa mashirika haya na wale wa serikali walikuwa hawaoni giza mbele pale mikataba inaposainiwa na inapovinjwa bila utaratibu? ama walishauri? na kama walishauri nani aliyetengua ushauri wao huo? Hii ni kasumba ya sisi watanzania ya kutokuwa makini na vitu na tunapopelekwa nje kuangalia uwezekano wa ubia huwa hatuwi makini zaidi ya kwenda kufanya manunuzi/shopping zetu binafsi
Quote
 
Hili linajulikana JF muda mrefu Mwanakijiji alifichua kama mwaka umepita kama sikosei another Dowans hiyo utasikia tumeambiwa tulipe hizo bilioni cha kusikitisha.
 
Wana JF, kama kwamba maafa ya mabomu GOM hayatoshi, Jeshi letu la Ulinzi limetanda haya. Chanzo HabariLeo.
SIKU takriban tisa baada ya Dar es Salaam kutikiswa na milipuko ya mabomu na makombora katika kikosi cha Jeshi cha 511 ambacho ni Ghala Kuu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongo la Mboto, askari zaidi ya 30 wa kikosi hicho wanadaiwa kupiga raia.

Askari hao inadaiwa waliwapiga raia hao usiku wa kuamkia jana kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya mwenzao kupigwa na raia wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa wakazi hao, tukio hilo lilitokea saa 6.45 usiku, ambapo walishuhudia kundi la askari hao likipita kuanzia mwanzo wa eneo hilo na kumpiga raia yeyote waliyekutana naye barabarani.

Waliokumbwa na shambulizi hilo na kujitambulisha kwa waandishi wa habari kwenye kambi ya waathirika wa milipuko ya mabomu, eneo la Mzambarauni jana, ni Mazoea Nassor, Mohammed Selemani, Rashid Abdallah, Kassim Mango, Andrea Mbezi na bondia maarufu nchini, Mada Mauggo, wote wakazi wa eneo hilo.

Raia hao walioonekana kuwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao, walidai kuwa mbali na kupigwa pia waliwaporwa simu na fedha mbalimbali pamoja na kumwaga vyakula vya mama lishe, wakati wakiendelea na mashambulizi.

"Wametupora simu na fedha huku wakitupiga mateke, mikanda na ngumi. Wanadai kuwa wamefanya hivyo baada ya mmoja wao kupigwa na raia kwenye kituo cha mabasi cha Gongo la Mboto," amesema Mauggo na kuendelea:

"Mimi nilikuwa nimeshuka kwenye gari langu baada ya kuliegesha, lakini ghafla niliona kundi la wanajeshi wakipita huku wakipiga wananchi. Nikatoa simu kutaka kutoa taarifa Polisi, lakini kabla sijasema lolote nikashitukia nimepigwa mkanda mkononi na kuporwa simu na askari hao," amedai Mauggo.

Kwa mujibu wa Mauggo, baada ya tukio hilo, walikwenda kituo cha Polisi Gongo la Mboto kutoa taarifa, lakini hawakukuta askari kwani nao walikimbia kutokana na tukio hilo na kukiacha kituo wazi.

Amesema, walikwenda kituo cha Sitaki Shari na kufungua jalada namba STK/RB/3030/11 na jalada hilo kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi ambako walitoa maelezo zaidi.

Msemaji wa Jeshi hilo, Luteni Kanali Kapambala Mgawe, alipoombwa na gazeti hili kuzungumzia tukio hilo, alisema wakati huo hakuwa na taarifa za tukio kama hilo na kuahidi kuzifuatilia.

"Bado sijapata hizo taarifa. Lakini nakuahidi nitafuatilia baada ya taarifa yako hii,” alisema Mgawe.

Milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa na nyumba kadhaa kubomoka.

Tukio hilo limekuja huku baadhi ya raia wakiwa bado hawana makazi, wengine wakiugulia majeraha na baadhi yao wakiendelea kuomboleza kupoteza ndugu zao
 
Feb 25, 2011

DAR ES SALAAM, Tanzania (eTN) - Tanzania's dying national airline, Air Tanzania Company Limited, is facing legal suits in the United States and South Africa after failing to to settle its debt amounting to US$5.9 million to Celtic Air Corporation and South African Airways.

Senior officials from the airline's head offices in Tanzania's capital city of Dar es Salaam said the two legal counts were registered in the United States and South Africa after Air Tanzania breached contracts with the said air companies.

Celtic Capital Air Corporation is claiming US$1.7 million, while South African Airways (SAA) is claiming a total of US$4.2 million, basing their claims on contract breaching by Air Tanzania Company Limited (ATCL).

Celtic Capital Air Corporation had leased two Boeing 737-200 planes to ATCL, but the Tanzania's national airline stopped flying them.

ATCL leased two planes from the corporation, but as time went by it stopped using one of them, senior officials from Celtic Air Corporation said.

The contract for the second aircraft lapsed in March 2010 following the plane crash at Mwanza airport. South African Airways is suing ATCL for failing to pay US$4.2 million.

The Tanzanian government has been funding the loss-making airline to rescue from labor or industrial crisis and debts to its creditors, including local and foreign suppliers.

Since its parting from SAA, the airline has been experiencing a series of problems, while in December 2008, the Tanzania Civil Aviation Authority revoked its operation license over faulty documentation, terming it air-worthless.

Source: eTN
 
hii mijamaa kama inajiona ina nguvu sana si iiende kufanya kazi za ujenzi wa taifa.
 
Back
Top Bottom