khumbu_peresa
Member
- Feb 11, 2021
- 28
- 105
Habari wana Jamvi,
Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa sekta au tasnia ya usafiri wa anga kwa ndani ya nchi na kimataifa.
Siku ya jana tarehe 21/04/2022 shirika la ndege la Tanzania lilikua na ndege yake Airbus namba TC 210 ambayo inatoka DAR-HAH (DAR-COMORO) ambayo iliruka saa 4 asubuhi kuelekea Visiwani Comoros.
Pia Precision Air walikua wana Charter Flight (Ndege imekodishwa)siku hiyo kutoka Dar kwenda visiwani humo.
Umbali wa kutoka Dar mpaka Comoro ni km 683 sawa na 424.
Precision Air wakitumia ndege yao yenye usajili wa 5H-PWG ambayo ni aina ya ATR 72 yenye uwezo wa kubeba Abiria 70 kwa mpigo na mizigo tani 2.5 waliruka kuelekea Visiwani humo.
Kwa habari toka ndani ya vyanzo vya mamlaka ya ndege vinasema Ndege ya Air Tanzania ilifika kwenye Anga la Comoro na kushindwa kutua kwa kile Captain alichokiita hali mbaya ya hewa na kulazika kurudi tena Dar es salaam.
Watoa habari wanasema hii ni mara ya tatu kwa Rubani wa Air Tanzania kurudisha ndege Dar kutoka comoro hata kwa kitu ambacho kinaweza kuvumilika.
Huku nyuma Captain wa Precision Air aliyejulikana kwa jina moja la Captain Salim aliweza kutua Katika uwanja wa ndege wa Comoro salama kabisa mbali na hali ya hewa kuwa sio nzuri.
Bravo sana kwa Captain huyu wa Precision air hii inaonesha kuwa shirika la ndege la Precision lina marubani wenye uzoefu mkubwa kwenye tasnia hii ya anga pia shirika lina uzoefu mkubwa kwenye usafirishaji wa watu na mizigo yao.
Precision air wamekua kwenye hii biashara toka mwak 1995 na uzoefu huu umewasaidia kuwa extraordinary mbali ya shirika letu la Tanzania lenye ndege za kisasa.
Hongereni sana Precision Air.