ATCL yasaini mkataba wa ununuzi wa ndege mpya aina ya Bombadier

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya kutengeneza ndege kutoka Canada kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya aina ya Bombardier Q400, inayotarajiwa kufika nchini June 2020, yenye uwezo wa kubeba abiria 78.

Mkataba huo umesainiwa leo Oktoba 19, 2019, ambapo Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi, amesema kuwa ujio wa ndege hiyo unalengo la kuhakikisha inakuza huduma za usafiri wa ndege hapa nchini.

''Tunanunua ndege kulingana na mpango wetu wa biashara na kwa hali ya soko la sasa hivi hizo ndege 11 na hizo ndege zingine zilizokuwa zimetumika zinatupa sisi uwezo wa kutoa huduma kutokana na matakwa ya soko, lakini soko linabadilika na kwa makisio yetu hadi 2022 hizi ndege zitatufikisha hapo bila matatizo yoyote'' amesema Matindi.

Aidha matindi ameongeza kuwa hadi sasa ATCL wana jumla ya ndege 6, ambapo hadi mwisho wa mwaka huu kutakuwa na jumla ya ndege 8 na kwamba hadi kufikia mwaka 2021, Shirika hilo litakuwa na jumla ya ndege mpya 11.

Capture.PNG
 
Mkurugenzi mkuu wa ATCL Eng Ladislaus Matindi leo amesaini mkataba wa ununuzi wa ndege mpya aina ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiria 78
Injinia Matindi amesema ndege hiyo itawasili kati ya mwezi June na August 2020.
Source Channel ten!
Hii ni Habari njema sana, ni uthibisho kuwa ATC inazalisha faida kubwa baada ya kuazimwa ndege za serikali, ATC imetengeneza faida, imenunua ndege yake.
P
 
Mkurugenzi mkuu wa ATCL Eng Ladislaus Matindi leo amesaini mkataba wa ununuzi wa ndege mpya aina ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiria 78

Injinia Matindi amesema ndege hiyo itawasili kati ya mwezi June na August 2020.

Source Channel ten!
Wakati mkulima bado anapiga jalamba
 


Hapa Kazi tu

Kwa masafa ya ndani na safari fupi ambazo hazihitaji ndege kubwa inaonekana zinafaa sana hizi Bomberdier. Mmiliki ni Wakala wa ndege za Serikali.
 
Back
Top Bottom