ATCL yakanusha madai ya Safari za Chato kutokuwa na faida

Feb 9, 2021
6
16
Shirika la ndege la Tanzania limesema linaongeza safari za ndege kwenda na kutoka Bukoba na sio Chato kwa kuwa safari za Chato hazina faida.


Msemaji wa ATCL amesema safari hizo hazina abilia wala mizigo hivyo ni safari zisizo na faida ,naona wameanza kumsaliti Magufuli kabla hata 40 bado.

=====
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limekanusha habari zinazosambaa kwamba imesema Safari za Chato hazina faida.

Msemaji wa ATCL Josephat Kagirwa, amekanusha kuongea na Chombo chochote cha habari kuhusu safari za ndege.

Amewataka wananchi kupuuza huo uzushi.

IMG_20210409_144136_512.jpg
 
Kwahio zina faida? Na kama hizi zina faida kwanini kwa miaka mitano tunaendesha shirika kwa hasara ni wapi panavuja?
 
Msoga Clan kazini, mtahangaika sana lakini bado JPM atabaki mioyoni mwetu,majizi makubwa.
Hahaha jiwe kwishaaaaaaaa ni suala la muda tuuu nakupa miezi miwili ndege hazitaenda tena huko subiri utaona tuliwaaambia hiyo ni gbadolite ya Tz hamkuelewa
 
Najulishwa kuwa ATCL imefuta safari zote za kwenda Chato kwa sababu hazina faida kibiashara. Najiuliza kwanini leo? Kwani wakati wa mwendazake hii route ilikua na faida? Kwanini hamkumshauri mwendazake akiwa hai kwamba aimarishe uwanja wa ndege wa Mwanza na Bukoba maana ndipo kwenye abiria wengi? Mmesubiri mabilioni ya hela yakatumika kujenga uwanja leo hamtaki kwenda? Hasara hii atabeba nani? Sasa ule uwanja tupitishe punda au?

Mbona wakati wa mwendazake kila idara ya serikali ilijaribu kuji-position Chato, lakini sasa hivi mnakimbia? TRA walijenga makao makuu ya kanda Chato, hospitali ya rufaa ya kanda ikajengwa Chato, Mbuga ya wanyama Burigi-Chato ikaanzishwa, na Waziri wa Maliasili na utalii akatangaza kitovu cha utalii ni Chato. Uwanja wa ndege wa Chato ukajengwa mkubwa kuliko ule wa Mwanza. Mabenki yakafungua branch Chato.

Sasa imekuaje mbona mnaanza kukimbia? What is not happening? Mwendazake angekuwepo mngekimbia? Kama mnapata hasara, je hiyo hasara imeanza baada ya mwendazake kwenda kumlaki Bwana mawinguni au hasara ilikuwepo tangu zamani lakini mkaogopa kusema?

By Malisa GJ

So Seato is a graveyard

FB_IMG_1618264482212.jpg
 
Haya Madege wataishia kuyauza kama chuma chakavu! Biashara ishawashinda, hakuna abiria wa kupanda ndege Chato!
 
Warekebishe mapungufu ya ATCL hasa kwenye board na management. Zile order za ndege mpya ziwe cancelled immediately.!
 
WAREKEBISHE MAPUNGUFU YA ATCL HASA KWENYE BOARD NA MANAGEMENT. ZILE ORDER ZA NDEGE MPYA ZIWE CANCELLED IMMEDIATELY.!
Inasemekana bodi ya atcl waliyekuwepo hawana utalaam,idea,uzoefu na mambo
Ya ndege

Ova
 
Dahh... Kodi zetu tuu... Watu tumeishi ka digidigi.. All for Nothing..!!
 
Hili neno kumsaliti Magufuli linabadirisha uelekeo wa mama soon.

Nimeona hata bungeni limeanza kutumika ,,hii inawatia hofu waliodhamiria kututoa kwenye utumwa wa shetani.

Mama anatakiwa aweke kauri thabiti haraka na hili neno la kumsaliti jpm lisisikike bungeni.
 
Back
Top Bottom