ATCL na hofu ya kupigwa oda ya ndege mpya nne za kisasa

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,476
2,105
===
Tanzania tayari tuna ndege mpya 11 za kisasa zinazoifanya ATCL kuwa mshindani wa Rwanda Airlines,Ethiopia Airline na Kenya Airways katika biashara ya Usafiri na usafirishaji wa anga Africa.

Pamoja na kwamba kimahesabu ATCL inaonekana kutengeneza hasara lakini indirectly ATCL inafaida kubwa sana kwa Uchumi wa nchi yetu, kwamfano hadi kufikia ripoti ya mwisho ya CAG shirika letu la ATCL lilitengeneza hasara ya TZS 153BL ila indirect benefits CAG hakuzitaja ambazo ndio zinathamani kubwa zaidi ya hiyo hasara (Wakati mwingine CAG aje na indirect benefits za ATCL)

Kwamsiofahamu faida za ndege duniani kote sio Air ticketing (tiketi) ila ni indirect Profit yaani faida mbadala mathalani Tanzania tayari inahitaji watalii kutoka Duniani kote na kwamsiojua Watalii wanalipa kuliko hii "Air ticketing " mnazozipigia kelele,

Mfano, Mwaka 2017|18 mapato yetu yatokanayo na Utali yalifikia $2.4BL sawa na Tshs 5.5trilioni wakati rekodi ya Watali ikiwa 2m tu,Lakini tunafahamu duniani kila mwaka kuna zaidi ya Watali 1.5bl wanatafuta wapi waende kula bata,

Kama tulipata TZS 5.5Trilioni kwa watalii 2m waliojileta wenyewe itakuwaje tukiwafuata kwa Ndege zetu wenyewe? Nahasa ya 153BL Ni-nini kwenye mapato ya TZS 5.5 kama ndege hizi zitaleta watalii 2m wapya?

Niulize swali, Kenya Airways inaweza kubeba watalii toka UK ikawaletea ninyi Tanzania mnaopinga kuwa na ndenge zenu? "Jibu ni Hapana" vivyo hivyo kwa mataifa shidani kibiashara toka Africa hawawezi kuwafaidisha ninyi lazima kila nchi ivutie kwake na hii ni miongoni mwasababu inamfanya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza ndege mpya tano za kisasa huku akilipia nne za awali,

Nimejaribu ku-Google bei za kila ndege na hizi ndizo bei za kiwandani japo naamini kunapunguzo,

Bei ya Boing 787-800 dreamliner ni $248M au TZS 570.4BL,Wakati bei ya Boing 767 -300 Freighter ni $220M au TZS 506BL na Boing 737 Max ni $99.7M kwa moja sawa na TZS 458.6BL kwa zote mbili, Bei ya ndege zote nne kwa mujibu wa bei ya kiwandani ni $667.4M sawa na TZS 1.535Trilioni

Puuzeni uzushi, bei ya kiwandani kwa ndege zote mpya nne zilizoagizwa na Rais Samia ni $667.4M au TZS 1.5T na Sio $726M au 1.7T,Watanzania chapeni kazi inchi yenu iko Salama Sana,​

||Jifunzeni kuisemea nchi yenu mema||

photo_2021-11-14_07-25-55.jpg
 
Punguza ujuaji.

Kenya Airways wana Internationa Destinations 27 ambazo zipo active.

Rwanda Air wana international destinations 26 ambazo zipo active.

Tuwaache ethiopians Airline maana wana international Destinations zaidi ya 100. Hivyo ni aibu hata kuwacompare na Air Tanzania.

Air Tanzania wana International Destinations ngapi ambazo zipo active?
 
Punguza kuropoka hata kama unalipwa buku 7.
Hii wala sio hoja yangu,

Hoja yangu ni "Uzushi " wa bei za ndege

Twende kwenye hoja,
 
Air Tanzania wengefanya Ubiya na Emirates or na Qatar hawa ndio wafalme wa anga kwa kipindi hichi unajua hata Emirates walipokuwa wachanga walijifunza kwa PIA .Sasa na sisi tusinganganie tu hizi kazi zina wenyewe tujifunzeni halafu ndio tuingie ktk mashindano tutumie jina letu ndege zao kama Rwanda jina tu lao lkn ndege zote ni za nje.
 
Wazo zuri sana MKUU
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom