ATCL kupata ndege mpya Septemba

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,323
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imelipa Sh36 bilioni, sawa na asilimia 40 kwa ajili ya kununua ndege mbili za shirika la ndege la ATCL.

"Kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano tutahakikisha hatua za ununuzi wa ndege mpya zinafanyika kwa haraka ili kuweza kulifufua shirika letu la ndege na kuweza kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga ifikapo mwezi Septemba mwaka huu," amesema

Waziri huyo ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma na kusema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya upanuzi wake.

"Mradi huu umetupa mfano kama tukijipanga vizuri hata kwenye miradi mingine tunaweza kutekeleza kwa haraka na ubora unaotakiwa, kwa upande wetu kama Serikali tutahakikisha uwanja huu unakamilika haraka ili kuruhusu ndege kubwa kuanza kutua," amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Nitachagua kutumia ndege za ATCL dhidi ya ndege nyingine kama mchango wangu wa kufufua shirika. Kwa ndege hizi ndogo Bombadier Q400 bila shaka safari zitakuwa ni za ndani ya nchi na nauli zitakuwa affordable na competitive na watoa huduma ya usafiri wa ndege waliopo sasa kwa safari za ndani!
 
1468335396390.jpg
 
Nina mashaka na hizo ndege 2 kama ni mpya maana ukipiga hesabu hapo ndege moja ni kama bil 45.
 
Hivi huu ununuzi wa hizi ndege na haya maswala ya kusitisha nyongeza za mishahara,kusitisha ajira,kusitisha ulipaji wa malimbikizo na nguvu kubwa ya kuokoa hela za mishahara hewa hakuna uhusiano?

Nauliza tu.
 
Huu mradi ni vision ya mru mmoja. Na sio kama taifa. Sidhani hata kama wameandaa business plan ya huo mradi? Ufanisi unatakiwa kuonekana toka siku zinaanza kufanya kazi.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imelipa Sh36 bilioni, sawa na asilimia 40 kwa ajili ya kununua ndege mbili za shirika la ndege la ATCL.

"Kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano tutahakikisha hatua za ununuzi wa ndege mpya zinafanyika kwa haraka ili kuweza kulifufua shirika letu la ndege na kuweza kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga ifikapo mwezi Septemba mwaka huu," amesema

Waziri huyo ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma na kusema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya upanuzi wake.

"Mradi huu umetupa mfano kama tukijipanga vizuri hata kwenye miradi mingine tunaweza kutekeleza kwa haraka na ubora unaotakiwa, kwa upande wetu kama Serikali tutahakikisha uwanja huu unakamilika haraka ili kuruhusu ndege kubwa kuanza kutua," amesema.

Chanzo: Mwananchi
Wakitupa fair price tutazitumia sana katika safar zetu. They should make sure wanakua smart katika usafir huu, politics waweke pemben maana hii n biashara.
 
Improving Tourism

Publishing news on worldwide travel magazine and pay for posting - tusiwe wavivu

Travel fairs

Photos on Worldwide social media

Inventive on airfares International Airlines like VIRGIN ATLANTIC and more

Waziri Wa FEdha Dr. Mpango ni mchapakazi mzuri...ila amshauri Rais bila woga...

Achukue facts za kweli bila siasa

Tatizo la VAT kwenye utalii ni short notice...Watalii walishapanga budget zao, walishalipia trip/safari zao kuanzia June Mpaka December.....So kuongeza VAT ghafla ni kuwaambia watafute pesa zingine. Destination must be Faithful....

VAT italipwa vizuri sana, ila VAT isogezwe mbele ianze at least January 2017

Tour Operator and Travel Agents hawapingi kulipa VAT, kwanza mlipaji wa VAT ni mtalii sio Kampuni....

WaTanzania tuelewane kwenye hili..upotoshaji tuache...
 
Nina mashaka na hizo ndege 2 kama ni mpya maana ukipiga hesabu hapo ndege moja ni kama bil 45.

Compared to the average Turboprop-powered Narrow-body Commercial Passenger Plane, which costs $12,000,000, the Bombardier Q400 is: $15,000,000 more expensive (a 125% premium) Compared to the average cost for all Commercial aircraft, which is$31,000,000, the Bombardier Q400 costs: $4,000,000 less (a 13% margin)
 
Aircraft

January 2015 Average List Prices

Million US $

Q400

31.3

CRJ700

41.0

CRJ900

46.0

CRJ1000

49.0

CS100

71.8

CS300

82.0
Ndugu yangu ukipiga hesabu kwa hiyo 31 mil usd utapata zaidi ya bil 60 .. napata mashaka kuwa hizo ndege zitakua sio mpya maana pesa wanayo lipa ni kama bil 45
 
Ndugu yangu ukipiga hesabu kwa hiyo 31 mil usd utapata zaidi ya bil 60 .. napata mashaka kuwa hizo ndege zitakua sio mpya maana pesa wanayo lipa ni kama bil 45

Yeah...uko sawa kabisa. Hizi ni bei za January 2015 na ni average price, labda tuendelee kuchunguza
 
Back
Top Bottom