ATCL kulikoni?- mkuregenzi na mwenyekiti wa bodi nani mkweli?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ATCL kulikoni?- mkuregenzi na mwenyekiti wa bodi nani mkweli??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 20, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,147
  Likes Received: 5,575
  Trophy Points: 280
  Habari za Kitaifa Habari zaidi!
  ATCL kulikoni?-
  Gloria Tesha
  Daily News; Thursday,March 19, 2009 @19:10

  Siku mbili baada ya gazeti hili kutoa habari za mchakato wa kustaafisha kwa maslahi ya umma wafanyakazi takriban 70 wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Menejimenti ya Kampuni hiyo imewasambazia wafanyakazi hao kwa njia ya mtandao, taarifa ya kukanusha habari hiyo.

  Taarifa hiyo ambayo gazeti hili lilipata nakala yake leo, imesainiwa na Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Alphonce Mkinga na mbali ya kukanusha habari hizo, ilitoa ufafanuzi wa namna hatua za mchakato zitakavyofanyika.

  “Menejimenti inapenda kuwaarifu wafanyakazi kuwa mchakato wa kupunguza wafanyakazi huanzia vikao vya Menejimenti na Chama cha Wafanyakazi (COTWU) Taifa, kwa kupitia chombo maalumu cha Baraza la Majadiliano (CJIC), suala hili halijajadiliwa … hivyo si idadi wala vigezo vijulikanavyo hadi hapo mchakato utakapokamilika,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

  “Wafanyakazi mnahimizwa kuendelea kufanya kazi kama kawaida na kamwe masuala ya kwenye magazeti yasiwayumbishe … tuna jukumu la kuhakikisha kuwa kampuni inasonga mbele kwa kila mmoja wetu kufanya kazi kwa ufanisi, ili ndege zetu zijae abiria na kuongeza mapato ya kampuni.”

  Hivi sasa, mara baada ya kampuni hiyo kurudishiwa leseni ya kurusha ndege baada ya kunyang’anywa mwishoni mwa mwaka jana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kutokana na kuwa na dosari katika nyaraka kadhaa, inajiendesha kwa ndege mbili aina ya Bombadia Dash 8 zenye uwezo wa kubeba abiria 50 kila moja kati ya tano zilizopo.

  Awali iliponyang’anywa leseni, ilikuwa ikipata hasara ya Sh milioni 40 kwa siku, kutokana na kusitisha huduma. Kwa taarifa ya mtandao, gazeti hili lilimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, David Mattaka kuzungumzia taarifa hiyo, ambaye alidai kuwa hawezi kukanusha wala kukubali kuhusu taarifa hiyo na mchakato mzima.

  “I have no comment (sina cha kusema) kuhusu hilo … nasema sina cha kusema, nivumilie tu nikipata cha kusema, nitasema … sina lolote, nimesema naomba unielewe hivyo, nitakapokuwa tayari nitakujulisha, iweje niseme kitu ambacho hakijakamilika?,” alisema Mattaka alipohojiwa leo kwa njia ya simu.

  Kwa upande wa uongozi wa COTWU, taarifa yao ilieleza kuwa hawawezi kutoa uamuzi wala kauli yoyote kuhusu hilo, kwa kuwa utaratibu wa kufuata kanuni na sheria za kazi unafahamika, hivyo wanasubiri suala hilo liwekwe katika meza ya majadiliano.

  “Hatuwezi kusema lolote, tunashangaa tu leo kukuta taarifa hizi katika mtandao, ni ngumu kusema, maana halijawekwa mezani, tunataka menejimenti iliweke mezani ili sheria na taratibu zifuatwe na tukubaliane,” alisema kiongozi wa COTWU ambaye hakupenda kutajwa jina gazetini.

  Awali gazeti hili lilipata taarifa ya kuwapo mpango wa kuwastaafisha wafanyakazi 155 kwa maslahi ya umma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Balozi Mustafa Nyang’anyi alipoulizwa kwa simu Jumanne wiki hii, alikiri kuwapo kwa mpango huo, lakini akasema watakaostaafishwa hawatazidi 70.

  Balozi Nyang’anyi alitoa pia vigezo vya wafanyakazi watakaostaafishwa kwamba ni wale wenye umri mkubwa wanaokaribia kustaafu, wasio na taaluma yoyote, wanaokatisha tiketi, watu wa mapokezi na wahudumu wa ndani ya ndege. Alisema wahandisi na marubani hawataguswa na mchakato huo, ambao kwa mujibu wa Nyang’anyi, tayari mchanganuo wa maombi ya fedha (bila kutaja kiasi) umeshapelekwa serikalini na utatekelezwa kwa hatua nyingine mara fedha zitakapopatikana.
   
Loading...