ATCL kufufuka kisasa zaidi, kwa nguvu zaidi -- na kutawala tena soko!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Lile Shirika letu la Ndege, ATCL, lililokuwa mkao wa kifo, baada ya kuwa hoi bin taaban huku jeneza la kuizika rasmi likiwa limeishaandaliwa, hatimaye sasa litafufuka, kwa kuibuka kisasa zaidi, kwa nguvu zaidi na kurejea katika utawala wa soko la biashara ya ndege nchini (regain the past glory) katika kipindi kifupi kijacho.

Hayo yamebainishwa leo asubuhi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa ATCL, Bw. Paul Chizi, katika mahojiano ya kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa hewani na TBC.

Huku akihojiwa na Mtangazaji mahiri kabisa wa TBC, Marine Hassan Marine, Bw. Paul Chizi amesema, baada ya ATCL kupewa mtaji mpya na serikali, sasa itajitegemea yenyewe na kwa kuanzia, itaanza na ndege zake mbili, moja ambayo ilikuwa kwenye matengenezo makubwa sasa imeshapona na imesharejea, na ya pili inakwenda kwenye matengenezo.

Bw. Chizi alitoa historia fupi ya ATCL tangu shirika lilipoanzishwa baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwaka 1977, ATC ilikuwa na ndege 7, zikiwemo ndege mbili alizozirithi toka EA Airways, mwaka 1978, ilinunua ndege zake 5.

Akielezea kilichoiua ATCL ni zoezi la ubinafsishaji kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini, SAA, ulioliacha shirika hilo na madeni makubwa.

Marine Hassan alimbana zaidi Bw. Chizi, kuwa hata mara baada ya ubia huo na SAA kuvunjwa, mbona ATCL ilizidi kuzama, bwana Chizi alijibu majibu ya kichekesho eti kuwa "ni kawaida kwa baadhi ya mashirika ya ndege kufa, na kutolea mfano shirika la ndege la Uswissi, Swissair na lile la Italia, Alitalia kuwa yamekufa, hivyo sio ajabu kwa ATCL kufa!.

Marine alimbana zaidi kuwa kwa vile mashirika hayo aliyoyataja yamekufa, hivyo ndio sababu kweli ya shirika letu kufa!?. Bwana Chizi alisisitiza ndio, kama mashirika haya makubwa yamekufa, hiyo ni sababu tosha kwa nini ATCL isife!.

Mtangazaji Marine akazidi kubanana na Chizi, kuwa Tanzania sasa tuna mashirika binafsi ya ndege yenye mafanikio makubwa, akauliza, iweje mashirika binafsi yaliyokuwa hayana kitu, yafanikiwe, na shirika la umma lenye kila kitu life?!. Bwana Chizi alijibu kuwa hayo mashirika yaliyofanikiwa, yameweza kufanikiwa tuu kwa vile ATCL ilikuwa imekufa, maadam sasa imefufuka, sasa ATCL itarejea kwenye hadhi yake ya zamani!.

Marine Hassan akamdodosa bwana Chizi, jee ATCL itaweza vipi kuwarejesha abiria wake iliyowapoteza. Bwana Chizi amesema anaamini Watanzania wanalipenda shirika lao, hivyo mara watakapo rejea hewani, Watanzania watawaunga mkono kama zamani.

Mtangazaji Marine ilizidi kumbana bwana Chizi kwa kumsukumiza kabisa kwenye kona, alipomuuliza kuwa kama ATCL itaweza kuhimili ushindani wa soko dhidi ya mashirika mengine ambayo tayari yameisha imarika, Bwana Chizi, sio tuu alitoa kichekesho kingine, bali piauvunjwaji wa sheria za biashara huria, alipojibu kuwa ATCL itaiomba serikali kutoa waraka maalum, utakaowalazimisha watumishi wote wa umma, ni lazima waitumie ATCL, na wataweza tuu kutumia ndege za mashirika mengine pale tuu ambapo ATCL haiendi!.

Hili pia lilimshtua Marine Hassan alipomuuliza, hili la waraka, jee, halitasababisha ukiukwaji wa misingi ya soko huria na ushindani wa haki?!. Bwana Chizi, akasisitiza, hizo ndizo mbinu zinazotumiwa na mataifa mbalimbali kuhakikisha mashirika yake ya ndege, yana survive na kutolea mfano Uingereza, kuwa watumishi wa umma wa Uingereza, lazima wazitumie ndege za British Airways kila wanaposafiri, na endapo watakosa nafasi, ndipo wanaweza kupanda ndege za mashirika mengine. Kipindi kikaisha!.

MY TAKE
Japo habari hizi za kufufuka kwa a national flag carrier ni good news kwa Wazalendo, lakini ni bad news kwa private flights operators wa sekta binafsi kama Precision Air, maana ATC ikiimarika ni kifo kwao!.

Ila kama Bw. Paul Chizi anayekaimu u-CEO wa ATCL ndiye huyu niliyemuona na kumsikia leo, na kama ndiye yeye anayesubiria kuidhinishwa na Bodi ya ATCL kuwa CEO kamili, then, ATCL ni Bye Bye jumla, kaburini kabisa!, hivyo Precision Air Air itaendelea kupumua.

Mungu Ibariki ATCL!
Mungu Ibariki Tanzania!

Pasco.
 
Tatizo tunaangalia tulipoangukia na si tulipojikwaa, ndiyo maana ATCL inawweza kuanguka tena na tena. Serikali itaendelea kutoa pesa za walipakodi kuliinua shirika bila kutatua chanzo cha kufa kwake. Tatizo ni overheads zimezidi kwenye mashirika ya umma (yote ukiangalia..TANESCO, TRL, ATCL etc).

Overheads ni gharama ambazo hazichangii moja kwa moja kwenye utoaji huduma au uzalishaji wa bidhaa. Hizi gharama ili uzifidie inabidi uwe na faida kubwa sana. Kwa mfano, ATCL walikuwa na policy ya kuwasafirisha wafanyakazi wao kwa bei pungufu ya bei ya soko. TANESCO wana units za umeme za bure/bei pungufu kila mwezi kwa wafanyakazi wake.

Gharama kama hizi hazina uhusiano wa moja kwa moja na uzalishaji lakini zinapunguza faida au kupelekea hasara kwa kwampuni. Hii ni mifano tu, kuna gharama nyingi sana ambazo hazina tija kwa kampuni. Tena gharama hizi unakuta ni kubwa kuliko gharama halisi za kuzalisha huduma au bidhaa.

Tujaribu kuiga kidogo kwenye makampuni binafsi. Makampuni haya yatafanikiwa iwapo yatapunguza matumizi yake yasiyo ya lazima na kujikita kwenye matumizi ya lazima tu. Mfanyakazi anapewa mshahara mzuri, lakini hakuna pesa nyingine atakayoipata hovyo hovyo bila kuifanyia kazi ipasavyo. Mfano wanaweza kutoa bonus kwa wafanyakazi kutegemea na utendaji wa wa kazi. Bonus zinaweza kuwa katika mfumo wa fedha au huduma au bidhaa husika.
 
Hahaha!! Haya! Tutangoja! Maybe after 15years! Biashara ya usafiri wa unga imepanuka sana! Kwanza uwanja wenyewe tu wa ndege dar JK ni disaster!

Anyways let's hope words will turn to reality!
 
Nakumbuka wakati Mataka ameingia alipokuwa anaongea strategy zake mtu ulikuwa unahisi within two years ATCL will be in the next stage matokeo yake ikawa worse more than ever anyways lets see how it works this time around.
 
Mashirika ya umma ATCL ikiwa mojawapo yanaingiliwa sana utendaji wake na wanasiasa na hilo ni tatizo kubwa.Wanasiasa maslahi pamoja na maafisa watendaji wa mashirika haya wanapelekea kufa kwa mashirika kutokana na kufanya matumizi mengi yasiyo na tija huku mikakati ikiwa hakuna ya kuongeza mapato.

Suluhisho pekee ni kubadilisha namna ya uteuzi wa Maafisa watendaji wa mashirika ya umma na pia namna wajumbe wa board za mashirika haya wanavyopatikana. Kwa uteuzi wa boards kufanywa na wanasiasa kunaharibu sana mustakabali wa mashirika ya umma.
 
Mh! Isije ikawa nguvu za soda. Anyway we hope for the best. Atleast tutaanza kuwa proud again kama miaka ileeeee kabla ya ufisadi.
 
Mh..isijeikawa nguvu za soda..anyway we hope for the best.Atleast tutaanza kuwa proud again kama miaka ileeeee kabla ya ufisadi.

Mkuu, kweli ila kama alivosema Pasco apo juu, am very Pessimistic..sio mara ya kwanza hawa jamaaa kuwa injected na cash lakini hela hazijulikani zinaishia wapi...at one time, kuna wachina walitaka kuinvest apo nadhani wakaona hapa hapafai wakasepa

HAkuna namna ATCL eti itasurvive kama the so called Chizi analeta uchizi wake wa kutemper na soko huria kulazimisha watu wapande ndege hizo...not least wakati akiwa na mawazo kwua kwa vile Swissair na Alitalia zimekufa, baso na ATCL kufa si ajabu...unakuwaje na kiongozi wa namna hiyo?? Hayo mabilioni si yataishia kwneye 'matengenezo' tu?

Wajiulize inakuwaje Precision Air wanafanya vizuri.,..siku hizi kuna hadi flight 540 yaani watu wanaona potentials...yeye Chizi hazioni, anaziona ktk kuwalazimisha watumishi wa Umma wasafirie ATCL. Sikatai....lakini wka ndege Mbili? I mean moja manake nyengine ipo kwen matengenezo?

Ni kwa vipi wangeweza kutumia hizo billions walizopewa kuliweka shirika kwenye uwezo wa kukopesheka, wakaagiza ndege nyingine mpya walau 3 hivi ili pamoja na hizo mbili, waweze kucover destinations nyingi zaidi? Rwanda wameweza, sisi tunalalia mawazo ya Swissair na Alitalia....
 
Hao ni siasa tu miaka 50 hawana lolote lile; si unaona rwanda wao wanafanya kwa vitendo lkn sisi ndo inageuka ajenda kwenye kampeni na kuandika makaratasini. Sitegemei mabadiliko yoyote ndani ya nchi hii ya tanzania chini ya CCM na ikiwa basi mi nahamia Rwanda.
 
Mimi nafikiri hapo wanamwandalia mwekezaji mazingira, ili aje achukuwe shirika likiwa linabebeka. Si unajua sisi kazi yetu kubinafsidha vyenye nafuu. mashirika yalio hoi hutasikia yanabinafsishwa
 
Pasco

Unajua pale kinondni kuna makaburi ya aina mbili ya walalohoi kule juu na kule chini ya walibahatika kuishi kwa neema humu duniani sasa kilichofanyika david mattaka aliamua kuizika pale kwa matajiri kule chini na inapoelekea chizi amekataa kuzika kule anarudisha kwenye makaburi ya walalahoi ambayo kelele zake kama ushawhi pita pale ni kubwaa.

Kweli nilivyomssikia kwa leo siwezi acha sema

r.i.p atcl
 
mkuu...kweli ila kama alivosema pasco apo juu, am very pessimistic..sio mara ya kwanza hawa jamaaa kuwa injected na cash lakini hela hazijulikani zinaishia wapi...at one time, kuna wachina walitaka kuinvest apo nadhani wakaona hapa hapafai wakasepa

hakuna namna atcl eti itasurvive kama the so called chizi analeta uchizi wake wa kutemper na soko huria kulazimisha watu wapande ndege hizo...not least wakati akiwa na mawazo kwua kwa vile swissair na alitalia zimekufa, baso na atcl kufa si ajabu...unakuwaje na kiongozi wa namna hiyo?? Hayo mabilioni si yataishia kwneye 'matengenezo' tu?

Wajiulize inakuwaje precision air wanafanya vizuri.,..siku hizi kuna hadi flight 540 yaani watu wanaona potentials...yeye chizi hazioni, anaziona ktk kuwalazimisha watumishi wa umma wasafirie atcl. Sikatai....lakini wka ndege mbili? I mean moja manake nyengine ipo kwen matengenezo?

Ni kwa vipi wangeweza kutumia hizo billions walizopewa kuliweka shirika kwenye uwezo wa kukopesheka, wakaagiza ndege nyingine mpya walau 3 hivi ili pamoja na hizo mbili, waweze kucover destinations nyingi zaidi? Rwanda wameweza, sisi tunalalia mawazo ya swissair na alitalia....

Mkuu kaizer
Niko nyuma yako 101% hayo maneno ya alitalia na swissair yamenishtusha sana kwanini ukimbilie kwenye uzaifu usikimbilie kwenye mifano yakinifu rwanda wamefanya hiki na saasa tumepanga kuleta ndege hii na ile binafsi nimeona amewaweka wazi watanzania shirika linapoelekea ili siku likifa msimuulize alishaweka wazi kinabagaubaga..nimeona huko juu aidhinishwe na bodi bodi ipi??atcl bodi imekufa tangu apr wakagaiana za mwisho mwisho may na june dollr 500 kila kikao ndio sijasikia kama wanateua bodi nyingine tena
 
Pasco, anachokisema ni kweli kabisa, hata mimi leo nimebahatika kuona hicho kipindi.

Kwa jinsi alivyokuwa anajibu na kutoa maelezo kwa kweli ni ndoto hata kuwafikia Ethiopian Airlines, ambao wana 62 destination worldwide.

Mimi nadhani bodi yote wangewakabidhi wataalam kutoka nje, sisi ni maneno tu action hakuna.
 
Huyu Jamaa kweli Chizi! Nani kamteua hapo?

Paul chizi si chizi kama unavyodhani, akiwa Markerting Manager/Director wa ATC in Johanessburg ATC ilionekana shirika tishio, alifukuzwa ATC kwa sababu hakutaka ATC ijiingize kwenye mkataba wa Alliance.
 
Paul chizi si chizi kama unavyodhani, akiwa Markerting Manager/Director wa ATC in Johanessburg ATC ilionekana shirika tishio, alifukuzwa ATC kwa sababu hakutaka ATC ijiingize kwenye mkataba wa Alliance.

hoja za leo mkuu ndo zimemfanya aonekane Chizi kweli!
 
Yeye bado anaendelea kuamini kuwa serikari inavyofanya kazi sasa hivi itabakia hivyo hivyo milele na wataendelea kulipana hizo posho na hizo safari za ndege za Dodoma, na wanadhani labda threat yao ni Dr. Slaa, Mbowe, Prof. Lipumba, Mnyika nk bila kujua kuwa hizo ni rasharasha tu za mabadiliko. Muda si mrefu huenda wananchi wakaamuru wafanyakazi wa serikari wasafiri kwa basi labda!

Any way, ukijiuliza jinsi serikari ilivyokaa na kufanya brainstorming na kuishia kumpata CEO mwenye 'vision' kama hii ili aje kushindana na akina Titus Naikuni-KQ, si ni bora (kama ni point ya UTANZANIA) tukarivise memorandums za Precisionair ili kama kuna elements za 'uchaga' (kama wengi wanavyodhani) wazirekebishe ili waongezewe huo mtaji maana wameshaonyesha uwezo (kwa kiasi chake) wa kutupeleka huko tunakofikiria kwenye biashara ya usafiri wa anga!

Binafsi najilaumu kwa kutokuwa wa kwanza kwenda Mnazi Mmoja, Karimjee, Viwanja vya NMC Arusha au Viwanja vya Bunge Dodoma nk na petroli kisha kujichoma moto ili watakaobaki nyuma waone hasira juu ya maamuzi ya namna hii.
 
hoja za leo mkuu ndo zimemfanya aonekane Chizi kweli!

Ni kweli mkuu, but the guy is smart, I know him. Shida ni kuwa wamemkabidhi papai lililooza alimenye na kuwapa watu wale. lakini laiti wasingempa mataka, nina hakika ATC isingekuwa na hali mbaya kiasi hiki.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom