ATCL itafufuliwa kwa kuipa Ndege pekee?

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
3,851
ATCL Itafufuliwa kwa kuijengea uwezo wa kiutendaji ili iweze kujiendesha kwa faida. Iwe na uwezo wa kukopa na kurejesha kutokana na mapato yake yenyewe.
Imilikiwe na wananchi/wawekezaji na serikali iwe na hisa.

Ndege ni mojawapo ya vitendea kazi vya ATCL lakini haimiliki ndege, ila inapewa ndege na Serikali. Hatujui kama matengenezo ya ndege yatagharamiwa na nani kati ya serikali na ATCL?

Na Je serikali imeona ni bora kununua ndege kuliko kitu kingine chochote katika kukuza utalii na usafiri wa anga?

Na Je serikali ingeamua kujenga miundo mbinu ya usafiri wa anga kama airports kila makao makuu ya mkoa na sehemu za utalii kisha kuwaalika wawekezaji wa usafiri wa anga kuwekeza, isingefikia lengo la kukuza utalii na kuboresha úsafiri wa anga?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom