ATCL imeanza kupaa sana kimapato. Mbunge Zungu Ashauri serikali iige inachofanyiwa Ethiopian Airline na Serikali yao

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,889
Toka bunge hili lianze mbunge ninayeona katoa hoja nzito ni Zungu Kaeleza vizuri sana kuhusu ATCL NA NAMNA YA KUIFANYA IWE NA FAIDA KUBWA

Kasema kabla ya Magufuli Mishahara yote ya wafanyakazi wa ATCL KWA ASILIMIA 100 ilikuwa ikilipwa na serikali sasa hivi serikali inalipa asilimia 17 tu kiasi kilichobaki wanalipa wenyewe

Kashauri serikali kuondoa vitu kama landing fee ,navigation fee na parking fee nk

Msikilize kuanzia dakika ya 4

Bado tu mnapigia debe hizo ndege ilihali zimeleta loss ya zaidi ya billion 100+ toka mzipokee! Hivi huu ushamba mtaacha lini ccm??

Acheni kuchezea kodi za wananchi hivyo mkidhani wanafurahia hizo siasa zenu..
Hpo ndipo anapembua source ya hiyo loss inakotokea na sio loss as such ukitazama sababu mlipwaji ni serikali

Mfano vitabu vya hesabu vinaonyesha shirika lilipata mapato ya jumla ya shilingi bilioni 100 halafu ikalipa serikali parking fee shilingi bilioni 120.Utasema hilo shirika linaendeshwa kwa hasara linakula hela za walipa kodi sababu limepata hasara ya bilioni 20? Wakati hizo bilioni 120 zote zimeenda serikalini ambaye ndie mumiliki asilimia 100 WA SHIRIKA LA NDEGE HIYO HASARA NI YA WASIOJITAMBUA WAHASIBU NA CAG WAO.

ATCL sio kampuni private ni ya serikali asilimia 100.Kwa hiyo kujua kama ilipata hasara hutakiwi kuangalii vi book keeping vya form one vya profit and loss account!!!!! ANGALIA hayo yanayoitwa matumizi ni shilingi ngapi kapeleka serikalini pia.U take into account kabla ya kusema ohhh ATCL NI LOSS making compay .Inakula tu pesa za walipa kodi!! Imekula kodi za walipa kodi wapi hizo bilioni 120 kwenye huo mfano zimekwenda wapi si ni serikalini? Kwani Magufuli kaenda nazo kaburini au kazipeleka uswisi kuzificha? Na bado kuna ma VAT kibao serikali imelipwa na ATCL hujayajumlisha mikodi kibao ya tiketi na ya ATCL YENYEWE AMBAYO SERIKALI IMELIPWA NA ATCL

Mbunge Zungu yuko sahihi anajaribu kumuonyesha CAG NA SERIKALI KUWA HICHO KINACHOITWA LOSS siri yake imejificha wapi ambako hata CAG na kukariri kwake double entry book keeping hakuona sababu alichokisoma alikariri
 
Tatizo wenye maamuzi hawana elimu ya ujasiriamali, ushauri wangu, waangalie nini kifanyike kufanikiwa kwenye zama mpya za upinzani wa kibiashara,kufanya utafiti wakina, nini wapinzani wanafanya kwa mafanikio 'competitive analysis and that internatinal trade should be competitively harmonized'
 
Mimi sitaki kuongelea ndege hapa maana biashara ya faida na hasara inajulikana tu hata ukificha japo naunga mkono kuwa na ndege hasa safari za ndani nje huko mitihani soko gumu sana.

Nataka niongelee alichoongea kuhusu madini, serikali haiwezi kufanya biashara ya madini au biashara yoyote haya ndio masharti ya WB na IMF tatizo hapa kubwa ni PSA je huu mkataba wa miaka mingapi na operating cost je tunakuwa makini kuhakikisha hawaibi maana katika suala la operating cost au CAPEX katika mradi wowote ni lazima serikali watu wake kuhusika na kujiridhisha na budget ya kampuni hizi serikali lazima ifanye review kila mwaka kama operating cost inashuka na wapi sehemu ya kubana.

Kawaida ya PSA mkataba unakuwa na muda wa kuisha sijawahi kuona mkataba wa almasi huko ukiwekwa wazi lini PSA ilikuwa iishe maana toka mimi mdogo almasi inachimbwa tu.

Hili jambo wala sio gumu tatizo usiri mkubwa mimi naongea haya sababu nimefanya katika hii mikataba ya PSA na najuwa nchi nyingi zimenufaika baada ya PSA kuisha.
 
Kumbe serikali huwa inajikata kodi kwenye mali zake yenyewe mpaka zinashindwa kujiendesha, kwani CAG alitoa maoni gani ili hilo shirika lijiendeshe kwa faida? au nae alisema tu ndege ziuzwe kama sisi laymen wa mtaani.
 
Tatizo wenye maamuzi hawana elimu ya ujasiriamali, ushauri wangu, waangalie nini kifanyike kufanikiwa kwenye zama mpya za upinzani wa kibiashara,kufanya utafiti wakina, nini wapinzani wanafanya kwa mafanikio 'competitive analysis and that internatinal trade should be competitively harmonized'
Tangu walipo wafukuza Fast Jet kwa hila nikajua hawa watu wanaishi maisha ya kuigiza tu na hizo ndege wamezinunua kwa kutafuta sifa yu wala siyo kwa nia ya kufanya biashara.
 
Hpo ndipo anapembua source ya hiyo loss inakotokea na sio loss as such ukitazama sababu mlipwaji ni serikali

Mfano vitabu vya hesabu vinaonyesha shirika lilipata mapato ya jumla ya shilingi bilioni 100 halafu ikalipa serikali parking fee shilingi bilioni 120.Utasema hilo shirika linaendeshwa kwa hasara linakula hela za walipa kodi sababu limepata hasara ya bilioni 20? Wakati hizo bilioni 120 zote zimeenda serikalini ambaye ndie mumiliki asilimia 100 WA SHIRIKA LA NDEGE HIYO HASARA NI YA WASIOJITAMBUA WAHASIBU NA CAG WAO...
Zungu ana nini cha kumkosoa CAG?

Zungu na wewe tofauti yenu ni majina tu.
 
Bado tu mnapigia debe hizo ndege ilihali zimeleta loss ya zaidi ya billion 100+ toka mzipokee! Hivi huu ushamba mtaacha lini ccm??

Acheni kuchezea kodi za wananchi hivyo mkidhani wanafurahia hizo siasa zenu..
150 b +
 
Toka bunge hili lianze mbunge ninayeona katoa hoja nzito ni Zungu Kaeleza vizuri sana kuhusu ATCL NA NAMNA YA KUIFANYA IWE NA FAIDA KUBWA

Kasema kabla ya Magufuli Mishahara yote ya wafanyakazi wa ATCL KWA ASILIMIA 100 ilikuwa ikilipwa na serikali sasa hivi serikali inalipa asilimia 17 tu kiasi kilichobaki wanalipa wenyewe

Kashauri serikali kuondoa vitu kama landing fee ,navigation fee na parking fee nk

Msikilize kuanzia dakika ya 4

Wewe ni hasara kwa familia yako
 
Huyu zungu ni mtanzania? na kama ni mtanzania ni ukoo wa nani? wahindi, waarabu na wasomali wanajificha kwenye CCM na huku siyo raia wa Tanzania, utasikia Nondo na ndugu zetu wengine wa Kigoma wanahojiwa uraia badala ya hawa wakimbizi.
Wahindi na waarabu ndio wanaendesha kwa asilimia kubwa uchumi wa nchi hii.Miji mikubwa yote katikati ya miji wajenzi ni hao .Viwanda vyote vikubwa ni hao .Ajira nyingi za viwandani ni wao wanatoa.Mabilionea wakubwa wote Tanzania ni wao wahindi na waarabu.Walipa kodi wakubwa ni wao.Makampuni makubwa ya mafuta na ya usafirishaji nk ni wao

Sasa tuulizane hao wa kigoma mfano akina Nondo uliowataja cha maana wanachochangia nchi hii ni nini? Zaidi ya kutuletea majambazi na kupiga domo tu toka utawalinganisha na wahindi na waarabu ? futa kauli yako
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom