ATCL hatarini kunyang’anywa leseni-halina ndege hata moja mpaka sasa

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) liko hatarini kunyang’anywa leseni ya biashara ndani ya miezi sita endapo litashindwa kufanya kazi zake.

Akizungumza na Mwananchi kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa kamai hiyo, Deo Filikunjombe alisema shirika hilo lina wafanyakazi zaidi ya 200, lakini halina ndege hata moja mpaka sasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameitaka serikali na Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), kutafuta wawekezaji ili kulinusuru shirika hilo.“Tumewaita TCAA, lengo ni kuzungumza nao kuhusu ATCL ambayo mpaka sasa haina ndege hata moja, lakini ina wafanyakazi, na leseni ya biashara, jambo ambalo linakwenda kinyume na sheria,”alisema Filikunjombe.

Alisema mbali na shirika hilo, kamati hiyo imetaka kufahamu ni ndege ngapi zimesajiliwa, lakini hazifanyi kazi na pia wameitaka TCAA kufanya uchunguzi wa mikabata ya ndege hizo na serikali.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhili Manongi alisema serikali iko kwenye mchakato wa kutafuta mwekezaji ili kuingia ubia na ATCL kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri wa anga nchini.“Serikali kwa sasa inatafuta mwekezaji ili aingie ubia na ATCL na kutoa huduma hiyo, jambo ambalo tunaamini wakati wowote litafanikiwa,”alisema Manongi.

Alisema ndege zinazosajiliwa na kushindwa kufanya kazi zimetokana na kupanda kwa gharama za mafuta na mikataba mibovu.Alisema kutokana na hali hiyo serikali imeahidi kulishughulikia suala hilo kwa umakini ili kutoa huduma hizo.
 
Back
Top Bottom