Atangazwa amefariki, azinduka ndani ya jeneza, afariki tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atangazwa amefariki, azinduka ndani ya jeneza, afariki tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 24, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Alizunduka ghafla na kujikuta akiwa ndani ya jeneza watu wakiiaga maiti yake kabla ya kuzikwa, alikumbwa na mshtuko mkubwa baada ya kuambiwa kuwa madaWakati ndugu na jamaa huku wakiombeleza wakipita mbele ya jeneza lake ambalo liliachwa wazi kwa juu, Fagilyu Mukhametzyanov alizinduka na kuanza kupiga kelele baada ya kusikia watu wakisali kuiombea maiti yake iwekwe mahali pema peponi.

  Fagilyu Mukhametzyanov mwenye umri wa miaka 49 wa mji wa Kazan nchini Urusi alitangazwa kimakosa na madaktari kuwa ameiaga dunia wakati alipokumbwa na shambulio la moyo nyumbani kwake na baadae kupoteza fahamu kabisa.

  Mume wa Fagilyu, Fagili Mukhametzyanov, 51, aliambiwa na madaktari kuwa mkewe ameiaga dunia kutokana na shambulio la moyo.

  Taratibu za mazishi zilianza na wakati watu wakiliaga jeneza, Fagilyu alizunduka ghafla na baada ya kugundua yuko ndani ya jeneza alipiga kelele.

  Alikumbwa na mshtuko mkubwa uliopelekea apatwe na shambulio la moyo, aliwahishwa hospitali ambapo alilazwa kwenye chumba cha watu mahututi lakini safari hii aliweza kuishi kwa dakika 12 tu ndipo alipoiaga dunia kikweli kweli.

  "Nina hasira sana na nataka majibu ya mambo yaliyojitokeza, hakuwa amefariki wakati alipotangazwa amefariki, wangeweza kuyaokoa maisha yake", alisema mumewe kwa hasira.

  Msemaji wa hospitali, Minsalih Sahapov alisema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hili.ktari walishaitangazia familia yake kuwa amefariki, kwa mshtuko huo alifariki kweli.
   
 2. amygdala

  amygdala JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2016
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 1,081
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 280
  duh hio hospitali ina kesi ya kujibu
   
Loading...