Atangazwa Amefariki, Awekwa Kwenye Jeneza, Azinduka Kabla ya Kuzikwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atangazwa Amefariki, Awekwa Kwenye Jeneza, Azinduka Kabla ya Kuzikwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Aug 16, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Monday, August 10, 2009 4:50 AM
  Mtoto mmoja wa nchini Paraguay ambaye alizaliwa kabla ya muda wake alitangazwa kuwa amefariki, mwili wa mtoto huyo ulikabidhiwa kwa baba yake masaa manne baadae ukiwa kwenye jeneza lakini wakati maandalizi ya mazishi yakifanyika mtoto huyo alizinduka
  Baba wa mtoto huyo, Jose Alvarenga, alipewa taarifa na madaktari kuwa mtoto wake alifariki dakika chache baada ya kuzaliwa.

  Wafanyakazi wa hospitali ya serikali katika mji mkuu wa Paraguay, Asuncion, alikozaliwa mtoto huyo, walimkabidhi baba wa mtoto huyo mwili wa mtoto wake ukiwa kwenye jeneza masaa manne baadae.

  Jose alilichukua jeneza hilo lililokuwa na mwili wa mwanae na kurudi nalo nyumbani kwake kujiandaa na taratibu za mazishi.

  Wakati akiwa katika kuombeleza nyumbani kwake, Jose alilifungua jeneza hilo ili amuage mwanae kwa mara ya mwisho.

  "Nililifungua jeneza ili niuangalie mwili wake na ndipo nilipogundua kuwa mtoto wangu alikuwa bado akipumua" alisema Jose na kuongeza "Nilianza kulia".

  Jose alimwahisha hospitali mtoto wake huyo ambaye alikuwa bado hajapewa jina akiwa amembeba mikononi na kuwakabidhi manesi ambao walimweka mtoto huyo kwenye chemba ya oxygen kwenye chumba cha watu mahututi.

  Hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri hivi sasa.

  Uchunguzi kuhusiana na tukio hilo umeanza huku madaktari wakilaumiwa kuwa hawakumfanyia uchunguzi wa kutosha mtoto huyo kabla ya kumtangaza kuwa amefariki.

  Hata hivyo dokta Aida Notarioo wa kitengo cha uzazi cha hospitali hiyo, alisema kuwa madaktari walijaribu kumzindua mtoto huyo kwa zaidi ya lisaa limoja na vipimo havikuonyesha chochote kama alikuwa hai.

  Kwa mujibu wa rekodi za hospitali hiyo, mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa gramu 500 tu.

  Rekodi ya mtoto aliyezaliwa na uzito mdogo kuliko wote duniani inashikiliwa na mtoto mmoja wa Marekani ambaye alizaliwa akiwa na uzito wa gramu 280 tu wiki 22 kabla ya muda wake wa kuzaliwa.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2775358&&Cat=2
   
Loading...