Atakayegonga basi la Mwendokasi kutozwa faini 300,000!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
UDART imetangaza kwamba atakayegonga basi la Mwendokasi faini yake ni shilingi 300 000 na hakuna mjadala.

Basi likiguswa tu 300 000 baadaye ndiyo ulete sababu zako lakini ile kuligusa tu basi letu, laki tatu pa, baadaye ndiyo ukajadiliane na Mmeo/Mkeo hiyo laki tatu umepeleka wapi!

=======

Mabasi.jpg

Madereva wa magari, bodaboda na bajaji wanaovunja sheria na kuyasababishia ajali ya Mabasi ya Mwendo Kasi (UDART) watatozwa faini isiyopungua Sh300,000.

Meneja Uhusiano wa UDART, William Gatambi alisema wamewasilisha maoni ya kupitishiwa sheria ndogondogo kwa ajili ya barabara zinazotumiwa na mabasi hayo katika wizara husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Sheria hizo zitawabana madereva ambao wamekuwa wakipuuza taratibu na matumizi sahihi ya miundombinu, suala ambalo limekuwa likisababisha ajali za kila siku na usumbufu kwa madereva wa mabasi hayo,” alisema Gatambi.

Aliongeza kuwa mchakato huo uko katika hatua za mwisho kukamilika na baadhi ya sheria hizo zinaambatana na adhabu ya faini ya kuanzia Sh300,000 na kuendelea, kushikiliwa kwa chombo kilichosababisha ajali kwa muda na kifungo gerezani.

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa alisema mabasi 34 yalipata ajali katika kipindi cha siku 20 tangu kuanzishwa kwa mradi huo.

Mgwassa alisema gharama ya kuyatengeneza mabasi hayo ni kati ya Sh2.5 milioni hadi Sh3.5 milioni kwa kila moja.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga alisema takwimu zao zinaonyesha kwamba zimetokea ajali 13 zikihusisha mabasi hayo tangu Mei 10.

Licha ya ajali, mradi huo wa awamu ya kwanza wa UDART umekumbwa na changamoto nyingine ikiwamo ugumu katika upatikanaji wa tiketi kwa abiria.

Chanzo: Muungwana
 
Je Wao basi lao likigonga magari yetu watalipa kiasi gani?? Tuseme kituoni au kwenye junction likaacha barabara likagonga magari yetu na sisi tupange faini yetu ama??
 
Hiyo sheria imetungwa na bunge lipi au bunge la awamu hii siwezi kushangaa.

,,Meneja uhusiano wa Dart, William Gatambi ambaye amesema wamewasilisha maoni ya kupitishiwa sheria ndogondogo kwa ajili ya barabara zinazotumiwa na mabasi hayo katika wizara husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi"
 
Je Wao basi lao likigonga magari yetu watalipa kiasi gani?? Tuseme kituoni au kwenye junction likaacha barabara likagonga magari yetu na sisi tupange faini yetu ama??
Mkuu siyo kituoni tu kuna wakati haya magari yanapita barabara ya kawaida juzi tu jioni yalifanya hivyo.
 
,,Meneja uhusiano wa Dart, William Gatambi ambaye amesema wamewasilisha maoni ya kupitishiwa sheria ndogondogo kwa ajili ya barabara zinazotumiwa na mabasi hayo katika wizara husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi"

Kumbe bado inafanyiwa kazi lakini yeye tayari kapitisha sheria.
 
haya kuna moja limepinduka huko na kugonga kituo cha mafuta. nani atalipa?
 
UDART imetangaza kwamba atakayegonga basi la Mwendokasi faini yake ni shilingi 300 000 na hakuna mjadala.

Basi likiguswa tu 300 000 baadaye ndiyo ulete sababu zako lakini ile kuligusa tu basi letu, laki tatu pa, baadaye ndiyo ukajadiliane na Mmeo/Mkeo hiyo laki tatu umepeleka wapi!

wewewewe!! unasemaje? nani kasema?

yaani unapingana na "sheria" ya "rais mwema" wewe? rais wetu kaagiza kuchomoa matairi ili watu tujiongezee kipato halafu wewe unaleta sheria zako za uchochoroni huku!!

pisha uko!!
 
haya kuna moja limepinduka huko na kugonga kituo cha mafuta. nani atalipa?

Mbona sisi Watanzania ni vilaza sana na wagumu kuelewa namna hii? Umeambiwa ukigonga Basi unalipishwa wewe unakuja kusema likipinduka sasa kupinduka kwa basi ndiyo kuligonga?
 
UDART imetangaza kwamba atakayegonga basi la Mwendokasi faini yake ni shilingi 300 000 na hakuna mjadala.

Basi likiguswa tu 300 000 baadaye ndiyo ulete sababu zako lakini ile kuligusa tu basi letu, laki tatu pa, baadaye ndiyo ukajadiliane na Mmeo/Mkeo hiyo laki tatu umepeleka wapi!
Ili mradi hiyo iwe ni amri ya mahakama. Tofauti na hapo sasa tutaonana wabaya.
 
Ili mradi hiyo iwe ni amri ya mahakama. Tofauti na hapo sasa tutaonana wabaya.

Hauna cha kufanya wee kaa kimya na tii Amri, kama hutaki utakumbana na mkono ya Dola ni rahisi kihivyo tu, muda wa kubembelezana na kuleana umepita!
 
Jamani, kuna gharama yoyote kuishi burundi? Nataka niende huko maana huku kila siku sielewi namna nchi inavyoongozwa!
 
Back
Top Bottom