Atakaecheza na wasanii,2020 kura za vijana atazisikia kwenye bomba

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,912
Wanasiasa chezeni na kila mtu wakiwemo wanasiasa wenzenu lakini kamwe msithubutu kucheza na wasanii hasa wasanii wa mziki.

Tambueni wasanii hawa wana mashabiki ambao ni wafuasi wa vyama mbalimbali na hata wale wasio na vyama.

Tena tambueni vijana,ambao ndio wengi katika nchii hii,ndio wanaunda sehemu kubwa ya washabiki wa wasanii hawa wa mziki hivyo kucheza na wasanii hawa ni sawa na kuchezea shilingi kwenye tundu la choo.

Kingine mnachopaswa kutambua ni kuwa,shida na mateso vikizidi,watu huweka mbali tofauti zao na kuungana na kuwa kitu kimoja na kuweka mbali tofauti zao hivyo tofauti zao (kama zipo),na kwa haya yanayoendelea tofauti hizo zinaweza kutoweka na wasanii wakiungana,mtakuwa na hali mbaya sana wakati ukifika.

Leo hii mnapomuana Zitto anaongele vyama vya upinzani kuunganisha nguvu bila shaka haya ni matokeo ya utawala huu kuvibana vyama vya siasa na matokeo yake ndio haya ya Zitto kutaka kuunganisha nguvu na wenzake.

Mateso,shida na tabu vikizidi huleta mshikamano.

Najiuliza tu jinsi wimbo wa "viva Roma" ulivyo na mashabiki wengi itakuaje leo hii wakiibuka wasanii wengine na nyimbo za aina hii kina fulani watapona kweli hiyo 2020?
 
Kwa haya yanayoendelea,nakwambia wengi watazinduka maana haijulikani kesho itakuwa ni zamu ya nani.
Wengi watazinduka lakini wataathiriwa na wenzao wachache ambao wamekaa kimaslahi zaidi. Daima adui yako hapaswi kujua udhaifu wako. Sasa serikali ya CCM inajua udhaifu wa hao wasanii na hata wanasiasa wa upinzani. Kukwamuka kwetu nchi hii ni wote kujua thamani ya utu wetu kama taifa na si matakwa yetu binafsi.
 
Mm siamini katika wasanii kabisa.

Ni mpumbavu tuu pekee atakaepiga kura kisa msanii fulani amehongwa ili apigie kampeni mgombea flan.
 
Wanasiasa chezeni na kila mtu wakiwemo wanasiasa wenzenu lakini kamwe msithubutu kucheza na wasanii hasa wasanii wa mziki.

Tambueni wasanii hawa wana mashabiki ambao ni wafuasi wa vyama mbalimbali na hata wale wasio na vyama.

Tena tambueni vijana,ambao ndio wengi katika nchii hii,ndio wanaunda sehemu kubwa ya washabiki wa wasanii hawa wa mziki hivyo kucheza na wasanii hawa ni sawa na kuchezea shilingi kwenye tundu la choo.

Kingine mnachopaswa kutambua ni kuwa,shida na mateso vikizidi,watu huweka mbali tofauti zao na kuungana na kuwa kitu kimoja na kuweka mbali tofauti zao hivyo tofauti zao (kama zipo),na kwa haya yanayoendelea tofauti hizo zinaweza kutoweka na wasanii wakiungana,mtakuwa na hali mbaya sana wakati ukifika.

Leo hii mnapomuana Zitto anaongele vyama vya upinzani kuunganisha nguvu bila shaka haya ni matokeo ya utawala huu kuvibana vyama vya siasa na matokeo yake ndio haya ya Zitto kutaka kuunganisha nguvu na wenzake.

Mateso,shida na tabu vikizidi huleta mshikamano.

Najiuliza tu jinsi wimbo wa "viva Roma" ulivyo na mashabiki wengi itakuaje leo hii wakiibuka wasanii wengine na nyimbo za aina hii kina fulani watapona kweli hiyo 2020?
Wasanii wenyewe kila kukicha mara bangi mara unga,mara kashfa za ufuska ! Hawata athiri mtu yeyote mwenye akili zake timamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom