Ataka ndoa ivunjwe baada ya kubaini mkewe ni kikongwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ataka ndoa ivunjwe baada ya kubaini mkewe ni kikongwe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Che Guevara, May 19, 2010.

 1. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Mwananchi, Tuesday, 18 May 2010 21:36

  Anna Kinkande na Naomi Maeda, MSJ


  DUNIANI kuna mambo. Ukishangaa ya Mussa, utayaona ya firauni.

  Ndivyo unavyoweza kujisemea moyoni mara baada ya kusikia mkasa wa mkazi mmoja wa jijini Dar es salaam ambaye jana alifika mahakamani kutaka ndoa yake ivunjwe kwa madai kuwa amebaini mkewe ni kikongwe.


  Mkazi huyo, Peter Nyoni, 39, amefungua kesi Mahakama ya Mwanzo ya Buguruni akitaka chombo hicho cha sheria kimruhusu kumpa talaka mkewe, Sara Kweka, akidai kuwa mwanamke huyo alimdanganya wakati wakioana.


  Nyoni anadai katika kesi hiyo kuwa mbali na mwanamke huyo kumdanganya, pia amekuwa akitishia kumtoa uhai kila anapomueleza suala la kumpa talaka.


  Kesi hiyo ya aina yake na nadra kwa mwanamke kuiomba mahakama imruhusu kutoa talaka, ilivuta hisia za wengi jana wakati ilipofikishwa mbele ya Hakimu Anthony Sanchole wa mahakama hiyo.


  Nyoni aliiambia mahakama hiyo kuwa mwanamke huyo, ambaye alimuoa mwaka 2002, alimweleza wakati wanakutana kwa mara ya kwanza kuwa yeye bado ni mbichi na hakuwahi kuzaa.


  Mume huyo alidai kuwa baada ya miaka minane aligundua kuwa mkewe hakuwa kigori na kwamba alishazaa na tayari ana wajukuu watano na hivyo akaamua kuachana naye.


  Lakini Nyoni alisema amekuwa akishindwa kutekeleza azma yake ya kumpa talaka nyumbani kwao kwa kuwa mwanamke huyo amekuwa akimtishia kumuua kila wakati suala
  hilo linapoibuka.

  "Amekuwa pia ananiambia kuwa nikimwacha atanifanyia kitendo kibaya cha kunitoa duniani," Nyoni alidai mahakamani hapo.


  Awali karani wa mahakama hiyo, Mwanabibi Ramadhani alisema kuwa mtuhumiwa alitishia kumuua mumewe Mei 14, mwaka huu wakati wakiwa maeneo ya Buguruni Chama.


  Alisema Sara amekuwa akitoa vitsho hivyo baada ya mumewe kutaka kumpa talaka baada ya kugungua kuwa mkewe si mkweli katika ndoa
  yao.

  Hakimu Sanchole aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 28 mwaka huu itakapotajwa tena.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Makubwa!! Lakini sijui sheria inasemaje juu ya hilo maana kama kudanganywa mbona wengi tu wamedanganya ili wapate wakipendacho?? au hapa kosa ni kudanganya umri??
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ndoa ni mkataba, na kama mkataba wowote ule mistake of the subject matter inaweza kufrustrate mkataba, sasa kama kweli jamaa alidanganywa basi ridhaa yake ya kuingia katika mkataba wa ndoa haikuwa halali, jamaa ana option ya kuvunja ndoa au kuiacha iendelee.,ingawaje kweli ni kesi ya aina yake maana ni nadra sana kuona kitu cha dizaini hii.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ngoja nami nikimbilie mahakamani, nilidanganywaga kuwa ananipenda zaidi ya kitu chochote humu duniani na due to that nikaingia a life time mkataba- sasa mbona anapenda wengine??? si alinidanganya?? na tena basi anapenda hata visivyo na uhai mfano chupa ya therengeti!!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hapa kweli aliingizwa mkenge, yeye ana 39yrs, akadanganywa na mtu mwenye wajukuu tayari, kweli mapenzi kuwahiana.....
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Jamani unakaa na mtu ana wajukuu bila kujua hii kali
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kichekesho hiki!!! Hivi mwanamke akikuzidi umri si utamwona tu? Na kama ameshazaa si utamgundua tu? Huenda huyu Bwana Nyoni hakuona uzee wa huyo mke bali pengine mama wa Kichaga huyo alikuwa ana change a.k.a mapesa na akaolewa na zile hela!!! Kwa sasa pengie kipato kimepungua na ameshapata shangingi lingine la kumhifadhi hivyo anataka talaka!!! Hebu wazee wa mahakama fanyeni kazi yenu mchunguze hili suala mtakuta kuna walakini umejificha???!!! Unajua yale makaratasi a.k.a affidavity wanazowasilisha watu mahakamani hasa masuala ya ndoa ni fake contents ile mbaya na ni ngumu sana kuwa na ushahidi, hasa unaposema alinitishia kuua tukiwa chumbani!!!!! Huyo mama Kweka ni Mkibosho au Mmachame a.k.a Mpalestina??? Hawana mchezo hawa!!!
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  nimecheka mpaka machozi...dunia ina ammbo kweli.
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Cheka dada yangu maisha yenyewe haya mafupi...... ndio na kuna waliodanganywa ni watoto wa vigogo ah when it comes to love bwana uwongo kidogo lazima utumike. So nashangaa au kwa vile alodanganywa ni mwanaume?? wangapi walidanganywa kuwa ni mameneja? ah naona nadata tu mie hapa
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mwanzo wa hili game bwana uctegemee kuambiwa ukweli wa kila kitu....mengine ndio ya kuja kujionea mbeleni kama ilivyomtokea mbaba hapa.
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  Lakini naona mwanamme ana haki kabisa ya kwenda mahakamani mwanamke alikosea sana penzi ni kitu cha ajabu ..kinaweza kukinai ghafla na kwa hali kama ya huyu jamaa aliyedanganywa ..uongo ni sumu ya penzi
   
 12. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ......napita kimya kimya kwa kunyata:painkiller:
   
 13. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Inawezekana huyo bibi ni Kungwi mwenye UTAALAM wa kumpagawisha mtu, na jamaa alifia maufundi na maujuzi...
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hapa sheria itambana mke kwa kuwa kadanganya kitu ambacho kinatakiwa kiwe wazi ambacho hakina utata. hawezi kwenda mahakani akasema 'sikujua kuwa nina wajukuu au nina umri mkubwa' wakati mwanamme/ mwanamke anaweza kusema kuwa 'hakujua kama hakupendi kuliko vituvyote duniani aliposema anakupenda kwa sababu mapenzi hayana SI Unit'
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  cjui nimuelezeeje huyu baba, tangu 2002 leo hii ndio anagundua kama mke ana mpaka wajukuu? haa kweli ka game kalichezwa vizuri, pole zake kwa kweli.
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  wapate washauri wakayamalizie nyumbani tu....
   
 17. m

  muhanga JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mh makubwa haya, tena apenda hadi chupa? lakini ukweli mie ningekuwa na uwezo ningebadili kile kipengele "mpaka kifo kitutenganishe", ingekuwa "mpaka mapenzi yatakapokwisha"! lakini huyu kaka aseme kamchoka tu mkewe, kugundua kuwa ana wajukuu isiwe sababu kwani alipoanza kuishi nae kabla ya kugundua kuwa mkewe ni bibi mambo yote yalikuwa sawa, lakini kwa kuwa mapenzi yamepungua ndio anaanza kuziona hata hizo kasoro za ubibi! mbona wanaume wengi tu hudanganya wake zao kuwa wanawapenda, wakiwaoa mambo huwa tofauti, na baadae kuanza kuleta watoto wakubwaaa eti wote hao ni wale waliozaa kabla ya ndoa na bado ndoa zinaendelea?? lakini mke akijulikana aliwahi kuzaa tu basi nongwa!!!??? jamani kunya anye kuku akinya bata oooh kahara!!
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sio kupungua yameisha kabisaaaa....hicho kipengelee mwenzio nina mpango wa kukiandamia kibadilishwe kwa faida ya kizazi cha sasa, mana mtu upo tu unasubiriaga kifo na mpaka kifike cha moto umekiona.
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Na hiki ndicho kinachowafunga wengi. Hivi waliokitengeneza hawakuweza kuforesee jamani? Mbon awengi wanaumia na haya maneno 3 tu? ah
   
 20. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli siku hizi wachaga si wakuchezea! ujuzi ukiupata unautumia ipasavyo....Ila usivunje ndoa na mkeo kama amezeeka anunulie make up tuu atarudia kijana...maisha yanasonga mbele...
   
Loading...