Atafute kipato kwanza!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Atafute kipato kwanza!

Wametaka wenyewe, tumewapa! Wanaume wengi tangu watoto wamepitia malezi yanayowafanya kuwa watu muhimu kwa ajili ya kutafuta kipato cha familia.
Hilo ndilo jambo la msingi ambalo familia yoyote au jamii yoyote au tamaduni zozote huhakikisha mtoto wao wa kiume analifahamu jukumu hilo.

Jambo la pili ambalo wanafundishwa ni suala la mahusiano na jinsi ya kuishi vizuri na mke hata hivyo hivi vitu viwili ni kinyume (opposite) kwa mwanamke ambaye yeye huanza kufundishwa masuala ya mahusiano kwanza na baadae suala la kipato katika familia.

Hata hivyo dunia imebadilika sana kwani wanawake nao wanakuja juu kuhusiana na suala la kuchangia kipato katika familia na wapo ambao sasa wao (wanawake) ndio wanashika usukani kuhakikisha familia inasimama imara linapokuja suala la kipato.

Swali ni je, wanaume sasa nao wanabadilika ili kuwa wanaume wazuri linapokuja suala la mahusiano kama ambavyo wanawake wanavyokuja juu na kuwa mstari wa mbele kuhusiana na suala la kipato?

Naamini kila mmoja ana jibu lake
 
jamani kaka, copy&paste zimekuzidi, hebu tupe uhalisia wa thread jamani.
 
unaangalia copy & paste au unaangalia thread iliyotolewa ujadili. Nafikiri ni hali tu imewafanya watoto waingie kwenye ajira siyo kwamba wanataka au wazazi wanapenda. hata mimi niliyeishi kijijini, nikiwa na umri wa miaka kumi nilikuwa naenda kununua vitu sokoni, nachota maji hiyo ni kusaidida.

Tangu uchumi umedidimia sasa hata kazi za kuhatarisha utoto zinafanywa. Kiukweli siyo kwamba hii hali wazazi au watoto wenyewe wanapenda.
 
Mkuu, inakuwaje hapa klorokwini?
Naona unawashukia ma queen,
Wenzio wamebukua unguini,
Na usipende kuuliza kwa nini.
deh deh deh. ma FBI (Female Body Inspectors) hapa inabidi tufuatilie wat iz the rizani bihaindi this. acha nimbipu loya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom