At the end of the day your value and uniqueness remain as your precious asset

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,458
3,329
Victor Mlakimtoto Wa Wilbard

Mwisho wa siku ni wewe na maisha yako.

Hakuna kitu kizuri kama kuitambua nafasi yako na na kujithamini Duniani kwa sababu hayupo anayeifahamu thamani yako katika kiwango kilekile na vigezo vilevile unavyovitumia wewe kujithamini.

Achilia mbali kuwa na marafiki wengi wanaokuzunguka wakionesha kuwa karibu na wewe ili kukidhi wanachohitaji na kuendeleza thamani yao huku wewe ukibaki na unayoyaona kuhusu wewe "Jithamini".

Hakuna aliyeumbwa kama wewe na anayeona kile ninachokiona kuhusu wewe kama unavyojiona wewe mwenyewe.

Watu wengi wanapokuwa wamezungukwa na marafiki wengi huamini wanathiniwa sana ila uhalisia unaonesha wanaokuthamini ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya thamani yao na hawaifahamu thamani yako kama unavyoifahamu wewe.

Kujithamini huku ukizingatia kiasi ni sifa ya pekee sana inayoweza kuonesha upekee wako kwa wengine na kuwafanya angalau kuona kile unachokiona kuhusu wewe.

Usijilazimishe watu wakuone kama unavyotaka wao kwa sababu "watajiona wao katika wewe na wewe hutajiona katika wewe"(utaelewa taratibu tu usijali).

Hatupaswi kujiona katika viwango na vigezo vya wengine ili kuleta ladha ya maisha ambayo ni upekee.

Kanuni za uumbaji zinaonesha upekee ndiyo ladha kuu inayoweza kumstaajabisha na kufurahisha kwa kushangaza akili ya Binadamu.

"HIvi unafahamu upo wewe tu Duniani na hakuna aliyeumbwa kama wewe licha ya viumbe aina ya binadamu kufukia zaidi ya bilioni saba katika uso wa Dunia?"Jiulize tena na Mimi hapa pia najiuliza hivyohivyo.

Halafu huo upekee wako au wangu kwanza tunautambua?na kama ndivyo je tunauthamini?.

Fuatilia kwa karibu watu waliofikia hatua ya kujithamini kutokana na upekee wao wana hali gani halafu jiangalie wewe upo kwenye hali gani.

Elewa kuna watu ili kulinda thamani yao wao hulazimisha kutambulisha muonekano wako kwa wengine tofauti kabisa na vile unavyijiona wewe jambo ambalo linaweza kuwafanya wengine walazimike kukutafsiri kwa tafsiri yao na sio yako.

Haujawahi kuishi na Mtu au kufanya kazi mahali na kukutana na mtu anayetoa maelezo ya kila mtu wa eneo lake kana kwamba anawaelewa kuliko wanavyojielewa wenyewe? (watu hawa hutumia njia hii ya kujihami kulinda thamani yao)

Hakuna wajibu mkubwa kwa binadamu kama kujithamini,ni wajibu ambao una changamoto nyingi mno lakini bado tunapaswa kuutekeleza ili kujitendea haki katika namna inayostahili.

Kamwe usikatishwe tamaa na yeyote yule kuhusu wewe kutokana na ukweli kwamba hajui kile unachokijua wewe na anachofanya ni kujionesha yeye juu yako jambo ambalo siyo sahihi kabisa ingawa limewaumiza wengi sana mioyoni na kuwafanya wafikie hatua ya kujiona wao ni duni sana kuliko wengine.

Kanuni za uumbaji hazijaacha umbwe katika kumpa kila mtu kila kitu kilicho chake na ni jukumu la mtu huyo kujitambua na kujithamini ili kufanya kilicho chake.

Ukiona unashindwa kusoma andiko hili kutokana na wingi w maneno unaweza kuchukua maneno haya machache,

"Mimi ni wa thamani na thamani yangu ni upekee wangu ambao hakuna anaye ufahamu kama ninavyo ufahamu mwenyewe hivyo basi ni jukumu langu kuwaonyesha wengine nilivyo kwa namna nilivyo na sio wao kunionyesha nilivyo kwa namna walivyo wao".

For my family and friends including you.
 
..."MIMI NI WA THAMANI NA THAMANI YANGU NI UPEKEE WANGU AMBAO HAKUNA ANYEUFAHAMU KAMA NINAVYOUFAHAMU MWENYEWE HIVYO BASI NI JUKUMU LANGU KUWAONESHA WENGINE NILIVYO KWA NAMNA NILIVYO NA SIYO WAO KUNIONESHA NILIVYO KWA NAMNA WALIVYO WAO.

Kuna ulazima gani wa kuwa na jukumu la kuwaonesha wengine ulivyo..!?
 
Kwa sababu maisha ya mtu ni muakisio ambao wengine watauona kupitia wewe na ni vizuri sana kulinda kuonekana huko kusiwe ni kule kwa wao kupitia wao.
 
Kuna ulazima gani wa kuwa na jukumu la kuwaonesha wengine ulivyo..!?
Suala la kuonesha maisha yako kwa wengine sio la kutangaza kwa mdomo au uandishi..bali mwenendo wa maisha yako ya kila siku.
Kiini cha hili bandiko ni, "Ishi maisha yako"

Wako watu wanafanya mambo ili watu wengine wafurahi juu ya alichokifanya..hata kama mwenyewe linamuumiza.
 
We
Suala la kuonesha maisha yako kwa wengine sio la kutangaza kwa mdomo au uandishi..bali mwenendo wa maisha yako ya kila siku.
Kiini cha hili bandiko ni, "Ishi maisha yako"

Wako watu wanafanya mambo ili watu wengine wafurahi juu ya alichokifanya..hata kama mwenyewe linamuumiza.
Well said rafiki nashukuru kwa nyongeza yenye tija
 
Suala la kuonesha maisha yako kwa wengine sio la kutangaza kwa mdomo au uandishi..bali mwenendo wa maisha yako ya kila siku.
Kiini cha hili bandiko ni, "Ishi maisha yako"

Wako watu wanafanya mambo ili watu wengine wafurahi juu ya alichokifanya..hata kama mwenyewe linamuumiza.

Nakubaliana na hili sina tatizo nalo

Ila kama ulifuatilia kiini cha kum`quote jamaa yangu hapo juu ni kutokana na neno Jukumu

Kwanini iwe hivyo..!? Maana naona ni kama aina ya wajibu wa kujivika ili kutimiza kusudi fulani

Nadhani ni vema hata kama ukifa kusiwe na ulazima wa watu kurejelea aina yako ya maisha
 
Waaaao! great Billie
Unajua kuna mstari mwembamba sana kati ya mtu kuchagua aina yake ya maisha anayoitaka kuiishi kwa kuepuka kutumika na watu

Na ile tabia ya ubinafsi ya kujiona upo sahihi kwa kila jambo kwa kuwa wewe ni wewe na si yule mwengine..?
 
Unajua kuna mstari mwembamba sana kati ya mtu kuchagua aina yake ya maisha anayoitaka kuiishi kwa kuepuka kutumika na watu

Na ile tabia ya ubinafsi ya kujiona upo sahihi kwa kila jambo kwa kuwa wewe ni wewe na si yule mwengine..?
Kweli Kaka ndiyo maana ukiangalia andiko langu kuna mahali nimeandika "kiasi"kuwa na kiasi ni muhimu sana Mkuu
 
Nimeamua nicomment na like kabla hata sijasoma Uzi , haedading tu inaonyeza huu uzi una madini ya kutosha .
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom