At least 13 US service members killed in Kabul airport attack

Kuna watu humu wanatakiwa watumiwe majibu ya force kutokana na mabaya kutokana matamshi yao, sio wote wanastahiki majibu ya upole, nadhani sio mgeni ww humu ndani, mtu anapokuita gaidi au kumtukana Mtume siwezi kumvumilia lazima apate majibu mkabala
Mtume alipigwa mawe Twaif, hata dua ya laana hakuwatamkia na hakuwatakia dharra. Akisema huwezi jua pengine wanaweza wakatoka(kizazi) wenye heri kwa hao watu.

Mmoja wa mabedui alitaka kumuua Mtume akakamtwa na swahaba na wakamfunga kwenye shina na kumuita Mtume.

Mtume akamuuliza mmempatia chochote kwa maana kinywaji ama chakula, wakajibu hapana! Mtume akawaagiza wamletee chochote huku bedui akaiweka wazi nia yake ni kumuua.

Mtume akamuacha kwa siku 3 huku huduma za kumjali kwa chakula zikiwa zinaendelea, akamfuata akamuuliza unataka kusilimu? Bedui akamjibu hilo halikuwa lengo langu. Mtume akawaamuru maswahaba wamfungulie na wamuache huru.

Alifanyiwa mengi zaidi ya mimi na wewe lakini hakuwatakia wala kuwajibu mabaya. Kuna siku akiwa na Swahaba zake ulipita msafara watu wanaenda kuzika. Mtume alikuwa amekaa. Alipouona akasimama. Maswahaba wakasimama baada ya kuona Mtume amefanya hivyo.

Wakamuuliza aliyeenda kuzikwa unamjua? Akajibu hapana! Wakamjibu ni Myahudi. Akawajibu ni binadamu anastahiki kuheshimiwa.

Hivyo usighadhibike! Pengine wao hawaujui Uislam na pengine wao hawamfahamu Mtume. Hivyo, wakitusi ama kukebehi jukumu letu ni kuwafahamisha kuwa uhakika wa haya masuala yapo hivi!

Nilipokosea nisamehe, nilipokukwaza nisamehe pia!
 
Back
Top Bottom