Astronaut Neil Armstrong Dead at 82 mtu wa kwanza kukanyaga Mwezi

mwezini watu hawashuki!!wanatoka tu nje ya rocket wakiwa wamening'inia na kufanya uchunguzi huku pilot akiendelea kuendesha mpaka wanamaliza kazi yao ndiyo wanarudi.kinachoongelewa ni kuingia ktk anga ya mwezi(lunar surface) wala sio kwamba wanashuka wanaanza kutembea kama tunavyofanya huku duniani.
Ndio hichi hapo Pichani?

022-apollo-11-AS11-40-5875-Aldrin-bei-fahne-ohne-schatten-55pr.jpg

Apollo 11, foto no. AS11-40-5875. Aldrin is said to be on the moon here next to a flag which has no shadow. So, this picture is not possible.
 
mwezini watu hawashuki!!wanatoka tu nje ya rocket wakiwa wamening'inia na kufanya uchunguzi huku pilot akiendelea kuendesha...............................
Mkuu kwa hii post hauitendei haki avatar yako. Hebu fuatilia hii link na nyinginezo utakazozikuta ndani ya hiyo page na uje ufute hiki ulichoandika.
 
[h=2]Neil Armstrong afariki akiwa na umri wa miaka 82[/h]Posted on August 26, 2012 by Mahmoud
0,,16194063_401,00.jpg

Risala za rambirambi zinaendelea kutolewa kufutia kifo cha mtu wa kwanza kufika mwezini, mwana anga wa Marekani Neil Armstrong. Armstrong mwenye umri wa miaka 82, alifariki kutokana na matatizo ya moyo
0,,16194036_402,00.jpg

Armstrong alisema kwamba alichokifanya, ilikuwa ni hatua fupi kwake kama binadamu mmoja, lakini ilikuwa ni hatua ndefu mbele, kwa binadamu wote duniani.
Alikuwa kamanda wa kikosi cha safari ya Apollo 11 – pamoja na mwanaanga mwengine Buzz Aldrin. Mamilioni ya watu duniani kote waliweza kufuatilia kwenye televisheni mnamo mwaka wa 1969, jinsi Armstrong alivyotua mwezini, umbali wa kilometa 400,000 kutoka kwenye sayari ya dunia.
Armstrong alisema wakati huo kwamba alichokifanya, ilikuwa ni hatua fupi kwake kama binadamu mmoja, lakini ilikuwa ni hatua ndefu mbele, kwa binadamu wote duniani. Rais Barack Obama amemsifu mwanaanga huyo kuwa ni shujaa mkubwa kabisa wa Marekani ambae kamwe hatasahaulika.
Armstrong aliefariki kutokana na matatizo yaliyoyababishwa na maradhi ya moyo, baada ya kuifanyiwa upasuaji mapema mwezi huu, amesifiwa kwa utayarifu wa kuzikabili na kuzishinda changamoto zilizoonekana kutoweza kushindika. Rais Obama aliyasema hayo wakati akiongoza katika kuwasilisha rambirambi pamoja na mwanaanga Buzz Aldrin. Obama amesema Armstrong alikuwa shujaa wa kweli.
0,,16133729_402,00.jpg

Picha za Armstrong akitembea mwezini zilionyeshwa moj kwa moja kwenye televisheni
Obama ameeleza kuwa wakati Armstrong na wanaanga wenzake walipoanza safari yao katika chombo cha Apollo 11 mnamo mwaka wa 1969, waliyabeba matumaini ya taifa lote la Marekani. Wakati huo Obama alikuwa bado ana wiki mbili ili kutimiza umri wa miaka minane. Obama amesema, alipotembea kwenye eneo la mwezini kwa mara ya kwanza ,Neil Amstrong alianzisha kipindi cha mafanikio ya mwanadamu ambacho kamwe hakitasahaulika.
Mwanaanga mwenzake, aliefuatana naye katika safari ya mwezini,Buzz Aldrin amesema ana uhakika kwamaba mamilioni ya watu wameungana naye katika kuomboleza kifo cha shujaa huyo wa Marekani. Buzz Aldrin amesema atamkumbuka rafiki yake Armstrong kama jinsi wananchi wengine wa Marekani na wote duniani watakavyomkumbuka mwanaanga huyo maarufu. Licha ya mafanikio yake makubwa yaliyotokana na safari ya Apollo11 Armstrong hakuwa mpenda sifa wa vyombo vya habari na wakati wote alijaribu kuviepuka.
0,,16194064_402,00.jpg

Mondlandung 1969 Neil Armstrong Fußabdruck
Armstrong hakuhisi kujitoa hadharani na kuvitumia vyombo vya habari. Hayo ameyasema mwanaanga mwengine wa Marekani John Glenn aliekuwa Mmarekani wa kwanza kuizunguka sayari ya dunia. Wajerumani pia wametoa rambi rambi zao juu ya kifo cha mwanaanga huyo wa Marekani na wamesifu mafanikio yake.Mkuu wa Shirika la utafiti wa anga la Ujerumani Profesa Johann-Dietrich Wörner ameliambia shirika la habari la dpa, kwamba Armstrong aliyawakilisha mafanikio ya maalfu ya wahandisi waliofanya kazi kuifanikisha safari ya chombo cha Apollo 11.
Profesa huyo amesema Armstrong alikuwa ishara kwa binadamu ya kuonyesha kwamba juhudi zao za kutafiti mambo mapya zitahifadhiwa daima bila ya kujali iwapo utafiti huo utakuwa na faida kifedha.Profesa Wörner amesema Arsmstrong ataacha urithi utakaokumbukwa daima duniani kote hata baada ya kifo chake.


 
Mkuu kwa hii post hauitendei haki avatar yako. Hebu fuatilia hii link na nyinginezo utakazozikuta ndani ya hiyo page na uje ufute hiki ulichoandika.
Naweza kukubaliana kwa kiasi fulani na hoja za conspirancy theories,kuna mwalimu(engineer professor,mtaalamu wa control science) mmarekani,ndiye amenifundisha hivyo; Desineni Subbaram Naidu Home Page
Desineni Subbaram Naidu Home Page
Sasa sidhani kama huyu mwalimu ametulisha tangopori,yaani hata hapo penye Red chini?
[FONT=Tw Cen MT, Helvetica, sans-serif][FONT=Tw Cen MT, Helvetica, sans-serif]Brief Biography of the Speaker: Desineni “Subbaram” Naidu received MTech and PhD degrees in Electrical Engineering (Control Systems Engineering), from Indian Institute of Technology (IIT), Kharagpur. Dr. Naidu taught, visited and/or conducted research at IIT; [/FONT][/FONT][FONT=Tw Cen MT, Helvetica, sans-serif][FONT=Tw Cen MT, Helvetica, sans-serif]Guidance and Control Division at NASA Langley Research Center[/FONT][/FONT][FONT=Tw Cen MT, Helvetica, sans-serif][FONT=Tw Cen MT, Helvetica, sans-serif]; Old Domain University; Center of Excellence in Advanced Flight Research at United States (US) Air Force Research Laboratory; Center of Excellence for Ships and Ocean Structures at Norwegian University of Science and Technology; Measurement and Control Laboratory at Swiss Federal Institute of Technology; Nantong University, China; the University of Western Australia in Perth, Center for Industrial and Applied Mathematics at the University of South Australia in Adelaide; Jiangsu College of Information Technology, Jiangsu, China; Center for Applied and Interdisciplinary Mathematics at East China Normal University, Shanghai, China; Institute of Systems Science, Academy of Mathematics and Systems Science, Chinese Academy of Sciences, Beijing, China; Shanghai Jiao-Tong University, Shanghai, China. Since 1990, Professor Naidu has been with Idaho State University, where he is Director of School of Engineering and Director of Measurement and Control Engineering Research Center. Professor Naidu received twice the Senior National Research Council Associateship award from the US National Academy of Sciences, and is an elected Fellow of the Institute of Electrical and Electronic Engineers (IEEE) and an elected Fellow of the World Innovation Foundation, UK. He has over 200 journal and conference publications including 6 books. He has been on the editorial boards of several journals including the IEEE Transactions on Automatic Control and Optimal Control: Applications and Methods. [/FONT][/FONT]
 
R. I. P. ... The Supper Hero, the first human being to walk on the moon.

You Know you did it ... !!!! AND Indeed ..thats all it matters!!
 
Hawakufika. Kama wali wangerudi tena. miaka zaidi ya 40 sasa wala hawataji kurudi. Mwonja asali huchonga mzinga. Ile ilikuwa filamu ya holiwood tu ilipigwa katika jangwa la Nevada ndiyo maana ukaona kivuli cha jua kiko mbele ya astrounaut.....totally against all the laws of physics.
 
Hawakufika. Kama wali wangerudi tena. miaka zaidi ya 40 sasa wala hawataji kurudi. Mwonja asali huchonga mzinga. Ile ilikuwa filamu ya holiwood tu ilipigwa katika jangwa la Nevada ndiyo maana ukaona kivuli cha jua kiko mbele ya astrounaut.....totally against all the laws of physics.

OMG ... So you are totally convinced that .. Explanations justifies the FACT?

1. Hawajarudi tena.

2. Kwamba Directors wa filamu za Hollywood hawahui Kanuni za Object and shadow?
 
walifika,wakatua,wakashuka,wakatembea,wakasimika bendera,wakachota udongo wa huko kwa ajili ya sampling na mengineyo. hii siyo issue ya kuamini au kutoamini ni fact na inabaki kuwa fact hata kama kuna watu fulani wanapinga.tatizo la mTZ anapenda ligi kwa kila kltu,hata vitu ambavyo ni completly scientific tuna viingizia udini.tubadilike jamani.
 
pamoja na wasifu wake wote,watu wa consipiracy theory wanadai yalikuwa ni majigambo tu ya wa-US kudai kufika mwezini ili washindane na wapinzani wao wa wakati huo-wa SOVIET.ni kwamba jambo hilo halina ukweli wowote.alale pema peponi.
 
Namimi nakubaliana na huo wasi wasi wa kisayansi unaoneshwa katika picha zinazodaiwa kufotolewa mwezini, Kuna bendera ya amerika inaonesha kupepea. Je mwezini kuna upepo sawiya na wa huku duniani? pia kuna picha inaonesha kivuli cha mwana anga. Je setup ya Mwezi ni kama ya dunia ilivyokaa hata tupate kitu na kivuli chake?

Hukuna hewa mkuu, sasa upepo utatoka wapi? nilipo kuwa mtoto niliwahi kuona picha za rangi zinazo onyesha mandhali kama ya mwezini, lakini zilipigwa hapa hapa aridhini kwenye jangwa la New Mexico (mwenzangu kanikumbusha nafikili ni Nevada) kama sikosei, na walionekana ma-astronauts wakiwa mazoezini wamevaa space suit.

Nilikuwa na interest ya mambo haya nikiwa na umri mdogo kutokana na Baba yangu kuniletea kitabu kilichokuwa kina julikana kama "TOMORROW THE MOON" hivyo nilikuwa nawajuwa kwa majina astronauts wote kumi na mbili na project zote kuanzia kwenye Gemin mpaka Appollo.

Kilicho kuja kunishangaza baadae ni pale nilipo angalia senema/movie nikaona kibendela cha Merikani kilicho simikwa kwenye aridhi ya mwenzini (kama ni kweli) kikipepea!! Sasa upepo ulitoka wapi mwezini, kingekuwa kimetengenezwa kwa simaku tungesema labda kinapeperushwa na kimbunga cha geomagnetic kinacho letwa na solar wind shock wave kutoka kwenye SUN (Jua)!!!

Inawezekana walifanikiwa kutua mwezini siku za baadae lakini hii ya mwaka 1969 siamini kama ilikuwa niya kweli! Kumbuka kilikuwa na ushindani mkubwa kati ya Merikani na URUSI katika mbio za nani atatangulia kumfikisha binadamu wa kwanza mwezini, Warusi walikuwa mbele katika hilo lakini kwa bahati mbaya ROKETI yao kubwa iliyokuwa imehundwa mahususi kwa safari ya kwenda mwezini ililipuka kwenye launchingi PAD - Warusi hawakusema kama ma-cosmonuats wao walipona katika ajali hiyo, ajali hiyo ilisababisha juhudi za URUSI kurudi nyuma kidogo; walipo pata habari kwamba wenzao wamefanikiwa, basi wakaona hakuna haja ya kuedelea na project hiyo.
 
walifika,wakatua,wakashuka,wakatembea,wakasimika bendera,wakachota udongo wa huko kwa ajili ya sampling na mengineyo. hii siyo issue ya kuamini au kutoamini ni fact na inabaki kuwa fact hata kama kuna watu fulani wanapinga.tatizo la mTZ anapenda ligi kwa kila kltu,hata vitu ambavyo ni completly scientific tuna viingizia udini.tubadilike jamani.

Hapana mkuu, mtu kama mwana sayansi lazima uchunguze kwa makini mambo fulani fulani - hivi bendera inaweza kupepea vipi kwenye mazingira ambayo hayana HEWA, hatukatahi kwamba Wamerikani hawakufanikiwa eventually kutua mwezini - tunacho sema hapa ni kwamba hii ya mwaka 1969 inatia shaka kidogo. Ndio hicho mkuu.
 
Hivi Yuri Gagarin ana status gani kwenye issue za outer space?

Ndiye alikuwa binadamu wa kwanza kwenda hanga za juu, kuteuliwa kwake hakutokana kwamba alikuwa na akili kuliko wenzake - hapana, Kolarov (designer wa roketi za Vostock) alimuona Gagarin ana wajii wa ufupi na mwili mdogo ndiye angefaa kuingia kwenye capsule ya roketi ya Vostock bila matatizo.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Warusi kurusha viumbe hai hanga za juu, waliwahi kumrusha mbwa aliye julikana kwa jina la Laika kabla ya kufikia hatua ya kurusha binadamu.
 
Hapana mkuu, mtu kama mwana sayansi lazima uchunguze kwa makini mambo fulani fulani - hivi bendera inaweza kupepea vipi kwenye mazingira ambayo hayana HEWA, hatukatahi kwamba Wamerikani hawakufanikiwa eventually kutua mwezini - tunacho sema hapa ni kwamba hii ya mwaka 1969 inatia shaka kidogo. Ndio hicho mkuu.
Kupepea bendera hakuhitaji upepo pekee,kwenye zero gravity bendera haijikunjamani inakuwa free kama vile inapepea. sababu ni nyepesi kuliko hewa ya huko. you get it?
 
nasikia hawa jamaa walitupiga changa la macho hawakufika mwezini.....walikuwa studio wakatengeneza kimovi kile
 
Kupepea bendera hakuhitaji upepo pekee,kwenye zero gravity bendera haijikunjamani inakuwa free kama vile inapepea. sababu ni nyepesi kuliko hewa ya huko. you get it?

Mkuu naona hapo umeteleza kidogo, nafikili kwa bahati mbaya. Nani kakwambia mwezini ni zero gravity!!!! Mkuu (mwezini) lunar gravitational force ni ndogo ukilinganisha na ya hapa DUNUANI - Ndio maana Neil Amstrong alionekana anatembea ana ruka ruka, in other words alionekana akiruka kidogo, mvutano wa gravity wa mwezini unamrudisha chini tena, lakini kurudi kwake chini ni kwa kasi ndogo huwezi kulinganisha na hapa Duniani. Vile vile - chombo kilicho fanikisha watue mwezini, kinaonekana kimetulia kabisa kwenye aridhi ya mwezini, sasa hii inawezekana kivipi under the so-called ZERO GRAVITY!!!! Kama mwezini kungekuwa hakuna uvutano wowote chombo hicho kingeonekan kinaelea tu hangani, siyo chombo tu bali hata Amstrong na mwenzake wangeonekana wamepwelea tu hangani.

Mkuu baadhi ya wana JF pamoja na mimi tunasema kibendera kilionekana kinapepea siyo KUHELEA - hivi ni vitu viwili tofauti - vitu vina helea under zero gravity lakini kitu/bendera mpaka ifikie hatua ya kupepea inahitaji UPEPO mkuu.
 
nasikia hawa jamaa walitupiga changa la macho hawakufika mwezini.....walikuwa studio wakatengeneza kimovi kile

Mkuu siwasemi vibaya Wamerikani, lakini wakiwa katika mambo ya ushindani au wakihitaji kitu kwa udi na uvumba wako tayari kufanya lolote! Kumbuka magari ya matela waliyo onyesha Ulimwengu wakidai ni Mahabara na mengine yameficha silaha za maagamizi ya alahiki yaliyo fichwa na Sadam Hussein jangwani!! Picha zilikuwa zinaonekana in high resolution kabisa malori yakiwa jangwani; kumbe soo lote ni la kutunga TU wapate kisingizio cha kuanzisha VITA. Narudia kusema sikatahi kwamba hawakutua mwezini ninacho bisha ni mwaka walio sema walitua mwezini - hii ya mwaka 1969 ina walakini SANA.
 
Back
Top Bottom