Asthma

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080




  • Asthma ni ugonjwa katika mapafu unao sababisha shida za kupumua. Mishipa inayopeleka hewa katika mapafu hufura kiwango cha kutopata hewa safi ya oksijeni (oxygen). Shambulio kali la Asthma laweza leta maafa.
Kuna vitu vingi vinavyo sababisha Asthma kushambulia mtu. Visababu ni vingi mfano: Vumbi, moshi, mazoezi, baridi au nyuzi za wanyama kama paka na mbwa.

Ishara za shambulizi la Asthma

  • Shida za kupumua
  • Mkoromo (kupumua kwa shida) na kutoa sauti kwa kifua wakati unapumua
  • Kukohoa
  • Uchovu na wasiwasi
Fuata maagizo ya daktari jinsi ya kutumia dawa za Asthma au muite daktari ikiwa hujui cha kufanya mtoto wako akishambuliwa na Asthma.

Asthma inahatarisha maisha, nenda katika chumba cha dharura ikiwa:

  • Mwanao ana matatizo ya kuhema
  • Midomo au makucha inapogeuka kijivu
  • Ngozi ya sehemu ya shingo ya mtoto inajivuta.
Hakikisha una habari kuhusu afya ya mtoto wako na nambari za daktari na unapompeleka hospitali kwa chumba cha dharura, hakikisha una majina ya dawa zote mtoto wako anatumia.
 
Dawa ya Ugonjwa wa Asthma Au kwa jina la kiswahili inaitwa Pumu Upate kiazi cha figili cheupe uchanganye na Asali Safi mbichi kiazi cha figili kimoja Asali kipimo cha kikombe cha chai ukisage kile kiazi cha figili kwa kutumia mashine ya blender kile kiazi cha figili tia kidogo

sana maji ndani yake kipate kusagika kwa mashine ili kiwe kama uji mweupe kisha sagika kile kiazi cha figlii changanya na ile asali ya kipimo cha kikombe cha chai. Matumizi yake awe anakula kijiko

kimoja kila siku Asubuhi na Mchana na Usiku kutwa mara tatu Kabla ya kula kitu kwa muda wa siku 40. tafadhali kila inapokwisha uitengeneze hiyo dawa na usiache hata siku moja kuto kutumia ile

dawa yaani usiruke hata siku moja baada ya siku 40 matatizo yake yamekwisha huyo hii ni kwa mtu mzima na mtoto mdogo pia inasaidia sana.
 
Back
Top Bottom