Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,888
- 143,986
Nimewaza sana mpaka kuleta hii mada:
Wakuu,Pascal tunamsoma sana hapa JF na ninafikiri mpaka sasa imekuwa ni vigumu kwa wengi kuelewa huyu mwenzetu anasimamia upande gani ingawa mwenyewe ameshaweka wazi kuwa ni mtu neutral kwa maana ya kuwa hana chama katika siasa za nchi hii ingawa sometimes anatuchanganya sana.
Binafsi naamini mtu unapompima kiongozi inabidi uangalie mazuri yake na mapungufu yake alafu ufanye uamue katika mizani kama kiongozi husika anafaa au hafai ili umchague au uwe unamuunga mkono.
Sasa kwa jinsi tunavyomsoma Pascal alafu tuka-assume tuna electoral college yetu hapa nchini kama ile ya Marekani alafu watu hao wakatakiwa kupiga kura kuamua nani awe kiongozi wa nchi hii,unadhani watu wenye fikra na mitazamo kama ya Pascal juu ya viongozi wetu wanaweza kuchagua kiongozi bora?
Kwa maneno mengine,watu wasio na upande wowote na wanaowapima viongozi kwa kwenda na matukio,wanaweza kuwa wapiga kura wazuri kwa maana ya kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura kuliko sisi wengine?
Karibuni kwa mjadala.